CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 245
- 312
Ujio wa teknolojia mpya ya kupashana habari na kuchipuka siasa taka nchini Tanzania kumeibua jambo ambalo lisipotafutiwa dawa linaweza kuja kutuletea majanga nchini. Kuanzia 2015 kumezuka tabia ya watu kujifanya wanahutubia Taifa. Na katika hali ya kushangaza mwaka 2019 mtu mmoja alijifanya anahutubia taifa kwa kutanguliza wimbo wa Taifa!
Akamalizia tena kwa wimbo wa Taifa. Maana yake halisi watu hawa wanafanya "impersonation"! Wanajifanya wao ni wakuu wa nchi! Sheria ya habari ipo na inatamka wazi nani ndiye anaweza kuwahutubia raia wa Jamhuri inayoitwa JMT.
Mtu mwingine yoyote anahitaji kibali. Ndio maana mfano Dar Es Salaam pakawekwa sehemu maalum kwa yeyote mwenye tangazo. Unatakiwa uombe muda na upeleke script yako pale Maelezo ihakikiwe.
Ujio wa teknolojia umerahisisha watu kuhutubia lakini haujabadili sheria! NI vyema sasa kila anayetaka kufanya press conference kupitia tools mbalimbali awekewe utaratibu. Ama sivyo iko siku atajiamkia mtu atangaze nchi imepinduliwa au mkuu wa nchi amekufa!
Si Idara ya Maelezo bado ipo tena kila mkoa? Si TCRA ipo?
Unaweza kudai je mtu akiwa nje ya nchi? Itakuwa hufahamu Internet inafanyaje kazi! Hawa kina YouTube na wenzao wana miiko. Serikali inaweza kuwataarifu kuwa ikitokea mtu anahutubia wasimruhusu mpake wapate clearance TCRA.
Sisi hatutakuwa wa kwanza kufanya hivyo. Mifano mzuri ni China, Morocco, Japan. Kina Google na YouTube hawawezi kufanya mchezo na wao. Watafungiwa kabisa. Na hawa hawajali kelele za haki za binadamu. Kwao ustawi wa nchi zao ni muhimu kuliko Uhuru wa jitu moja kutukana nchi!
Serikali chukueni nafasi yenu katika hili. Haiwezekani raia wahutubiwe na kila mtu! Tena wahutubiwe kujengeana chuki! Kama Sheria husika ilishafutwa basi haraka rudisheni utaratibu wa kuhakiki hawa "maraisi" feki!
Watakuja sababisha balaa!
Hakuna nchi duniani mtu yoyote anahutubia Taifa! Mmewahi kusikia Kenya, Uganda, Marekani, UK?? Kwa nini Tanzania iwe holela hivi? Kwani YouTube, Google, Twitter na Facebook ziko Tanzania peke yake?
Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe!