Hakuna mwenye uwezo wa kushindana na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mwenyekiti wa CCM Taifa ndiye Rais wa nchi

Waache waendelee kukumbatia katiba mbovu, atakuja atakayewageukiwa wao ama vizazi vyao zaidi ya JPM. Chuki waliokuwa nayo dhidi ya JPM na maumivu waliopata itakuwa several times akija mwingine.
Busara ya kawaida itumike tupate katiba mpya.
mmmh
 
Mwenyekiti wa CCM Taifa ni fisadi👇🤡🤡🤡
 
Tuliopo ndani ya chama kwa miaka mingi sana hii ndio kanuni, Mwenyekiti wa CCM Taifa yaani Rais wa Tanzania kichama ana mamlaka kuu tatu ndani ya CCM

1.Yeye ndiye sheria
2.Yeye ndiye Taratibu
3.Yeye ndiye Kanuni

Mamlaka haya matatu kichama hujulikana kama ( STK) yaani Mwenyekiti wa CCM Taifa Yeye ndiye mtoa Sheria, Yeye ndiye Mtoa Taratibu na yeye ndiye Kanuni za chama

Muda wowote na wakati wowote anaweza pendekeza chochote kibadilishwe iwe muundo wa sekretarieti ya chama au Taratibu za kuchuja wagombea au Sheria yeyote kuhusu uchaguzi wa chama

Haya mambo siyo kwa bahati mbaya tena kwa sasa yamepungua ukilinganisha na wakati wa chama kimoja ambapo Fikra za mwenyekiti zilidumishwa

Wakati huo fikra na maono ya mwalimu Nyerere ndio ilikuwa fikra na maono ya chama na kila mtu aliunga mkono zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM Taifa, Sisi vijana wakati huo ndani ya ccm tulijibu Zidumu

Rais Samia akiamua kugombea tena nafasi ya Rais kupitia CCM mwaka 2025 ndani ya chama hakuna wa kupiga kelele bali wote tunaufyata, Ana uwezo wa kuita wajumbe wa ccm kwenye mkutano mkuu na wahusika kutamka Mama amepita kwa asilimia 100%.Ndani ya CCM mtu kupita kwa asilimia zote haijaanza Leo,

Zamani tulipiga kura kuchagua mtu mmoja tu au kivuli, Yaani mgombea anakuwa mmoja unaambiwa sema ndio au hapana, Hata ukisema hapana bado mgombea atapita kwa kishindo tu

Wana ccm tuna nguvu ndani ya ccm tu, ukitutoa nje ya CCM nguvu yetu hupungua kama vile samaki umtoapo majini na kumuweka nchi kavu, Samaki atarukaruka kama dakika tatu halafu atazima moja kwa moja akiwa nchi kavu

Tunapiga kelele ndani ya ccm, Mwenyekiti akitangaza kukufuta uanachama wewe ndio Kwaheri hiyo, Hakuna wa kukutetea

Kwa kuwa ni ngumu sana Tanzania kutenganisha nguvu ya mwenyekiti wa ccm Taifa na Mamlaka ya Rais ndio maana neno STK sasa linaonekana kwenye mamlaka ya Rais

Lazima utambue kwa muundo wa ccm ni ngumu kuondoa mamlaka ya mwenyekiti ndani ya mamlaka ya Rais yaani Rais ndie Sheria ya nchi, Rais ndie Taratibu za nchi na Rais ndie kanuni za nchi

Rais kama mwenyekiti wa ccm Taifa ana nguvu na yupo juu ya Katiba

Katiba yetu ya sasa ipo kusikiliza Rais anataka kitu gani na sio Katiba kutoa muongozo Rais aufuate

Tunaweza tukawa na mawazo mazuri sana kuhusu nchi yetu lakini kwa muundo wetu ikawa mawazo yetu siyo mawazo ya Rais wa nchi hivyo yakatupiliwa mbali kabisa

Kwa vijana wa kisasa ambao ndio wanayahitaji Madaraka lazima kila wakati wawe upande wa mwenyekiti Taifa huku wakiheshimu Wengine chini yao bila kuleta dharau, Akiingia mwenyekiti mungine unaendelea hivyo hivyo kuwa upande wake

Tuendelee kusubiri kama Rais wa sasa Mama Samia atakubali kubadili muundo huu wa sasa na kutuletea Tanzania mpya ambayo Mwenyekiti wa chama na Rais wa nchi Yeye hatakuwa Sheria, Wala hatakuwa kanuni za nchi na wala hatakuwa Taratibu

Maono ya kuondoa STK yatawezekana tu pale Mwenyekiti Taifa au Rais kwa maono yake na hisani yake ataamua kuondoa lakini si kwa mawazo ya wananchi
Magufuli yuko wapi? Acha uzuzu
 
Hata Mimi niliamini hivyo hivyo hapo kabla LAKINI Sasa naamini tofauti SANA na mwanzo!!!hayo unayosema inategemea kama the state wameridhika na uongozi wake Basi watamwacha afoji uchaguzi lakini kama hawajaridhika na uongozi watamweka wanaemtaka!!!Binafsi naendelea kumsubiria Franklin D Roosevelt wa Tanzania na miaka yake kumi na mbili ya utawala Wake!!na Binafsi nimeziona dalili zake kushika hatamu soon!!sisi wenye macho ya rohoni tunaomba kabisa!!!2025 ni mbali Sana kabla hayajatimia!!
Si kweli... tz hakuna cha deep state wala nini.. kwa hapa tz rais ndio kila kitu, yeye ndio hiyo state, yeye ndio baba wa nyumba (hata kama ni mwanamke).

yy ndio kila kitu.. subiria hyo state uione
 
Is
Si kweli... tz hakuna cha deep state wala nini.. kwa hapa tz rais ndio kila kitu, yeye ndio hiyo state, yeye ndio baba wa nyumba (hata kama ni mwanamke).

yy ndio kila kitu.. subiria hyo state uione
Wewe hujui kusoma na kuandika nini!!??hebu soma nyuzi zote za Tumia akili halafu uje HUMU!!!
 
Sasa mkuu unatueleza yote hayo yatatusaidia nini sisi tulioko huku nakapanya ambao tunashida ya maji na wala hatuna dawa kwenye mahospitali.
 
Sasa mkuu unatueleza yote hayo yatatusaidia nini sisi tulioko huku nakapanya ambao tunashida ya maji na wala hatuna dawa kwenye mahospitali.
Utakubali show awamu hii! Awamu iliyopita waliotoa kauli kama hii uliongoza kuwakejeli, kuwatusi ukiwaita wapiga dili. Leo nadhani nawe mpiga dili.

Hata maandiko yanasema kila goti litapigwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kwa mantiki ya hoja zako, hapo ndio ujinga katika Nchi yetu ulipo. Kudhani kiumbe mmoja katika Nchi hii ana mawazo maridhawa na akili zaidi ya Watanzania 60+M akuchagizwa na CHAWA kibao kama wewe mtoa Thread.
 
Na kwa mantiki ya hoja zako, hapo ndio ujinga katika Nchi yetu ulipo. Kudhani kiumbe mmoja katika Nchi hii ana mawazo maridhawa na akili zaidi ya Watanzania 60+M akuchagizwa na CHAWA kibao kama wewe mtoa Thread.
Ok
 
Back
Top Bottom