Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu

Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu

belionea

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2014
Posts
1,053
Reaction score
923
Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu hata ungekua umemkosea nini ukijishusha ukanyenyekea analainika labda awe na mapepo ndio unyenyekevu wako hautagusa moyo wake.

Mume hafokewi, mume hagombezwi, mume humfanyii jeuri na kiburi, akinuna na wewe unanuna asipokutafuta na wewe humtafuti, utapoteza ndoa yako. Ni mume wako wa ndoa unaruhusiwa kumng'ang'ania kama ruba.

Asipokutafuta mtafute, asipoongea na wewe ongea naye wewe. Hakunaga mke anaambiwaga anajipendekeza kwa mumewe.

Kunyenyekea hakukugeuzi housegirl na ukapoteza nafasi yako ya kuwa mke, ila kiburi na jeuri ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke haraka sana.
Ujeuri weka pembeni!

[HASHTAG]#ndivyo[/HASHTAG] wanavyofanya waliodumu kwenye ndoa zao#
NOTE: Kuwa mnyenyekevu sio kuwa mpumbavu. Panapotakiwa hekima na akili zitumie!
 
uwe mnyenyekevu na mtiifu kwa mwanaume anaejua thamani ya mke,kuna wanawake wengine walikua wapole Ila ndoaa zimewafanya wawe wajeuri unakaaa kimyaaa weee..

Unajishusha mpk chini mwenzio anakujibu mbovu
Hakuna kinachoumiza katika mahusiano kama usaliti aiseee!!
 
Ulieleta mada bila shaka ni mwanaume, ndo mana unasema hivyo so nakusamehe bure, ungekuwa mwanamke nisingekuelewa
hahahahaha mbona hata wanawake wamesapoti
 
wangekua wanayasikia haya na kuyaweka moyoni ingesaidia ila sasa..................................
 
Back
Top Bottom