Hakuna mwanasiasa anayechoma kadi

Albert Einstein

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
384
560
Maana mwanasiasa wa kweli n yule aliyevuka kiwango cha utoto cha kufikiri

Tatizo LA nchi yetu kila anayejua kuongea ni mwanasiasa, na wapiga kura wetu hawampimi kiongozi kwa mpango alionao katika kupambana na changamoto mbalimbali, Bali humpima kiongozi kwa uwezo wake was kutukana, kudhihaki, kuropoka, kujitapa na hata kupenda vurugu.

Nimesoma vitabu kadhaa vyenye mbinu za kiutawala, kisiasa, kiuongozi na hats propaganda sijawahi kuona mwanasiasa aliyeiva anaamini kuwa kuchoma kadi ya chama kingine cha siasa ni sifa au uzalendo halisi.

Siasa ni dhana pana ambayo inaonyesha jinsi ulivyokomaa katika kulitumikia taifa na kuleta dira ya uongozi wa taifa ikiwa umepewa dhamana.

Mwanasiasa ni tafsiri pana sana , ni fani ambayo unataka kuwatumikia watu wa taifa lako bila kujali itikadi ya chama ilikuwezesha kupata dhamana ya uongozi.

MY TAKE: Hao viongozi wanahama vyama kila kukicha na kuchoma kadi ni vyema wakajifunza siasa safi za maendeleo kwani elimu haina mwisho.
 
Back
Top Bottom