Hakuna Mungu, ila kuna nguvu ya asili ambayo haina ukomo wala mwanzo

Hakuna Mungu, ila kuna nguvu ya asili ambayo haina ukomo wala mwanzo

Ibn Unuq

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2020
Posts
5,296
Reaction score
9,656
Kila kilichopo ni matokeo ya nguvu fulani.

Hakuna mtu anayejua mwanzo halisi.

Hakuna chanzo cha mwisho wala Mungu mkuu.

Ila kuna nguvu ya asili isiyoweza kueleweka kihistoria ambayo mtiririko wake huwa hauna kikomo mfano ukitaka kusema chanzo ni kiumbe/kitu fulani utalazimika kuelezea jinsi chenyewe kama chenyewe kilivyoweza kutokea kutoka kusikojulikana.

Na ikionekana inawezekana bhasi lazima tutie shaka kwamba hata Sayari na viumbe wengine(hata sisi) huenda viliweza kutokea kutoka kusikojulikana kama kilivyotokea chanzo hicho.

Hakuna anayefahamu kwasababu wote tumejikuta tu duniani tayari na tupo ndani ya nguvu hiyo.

Hivi mfano ukitekwa, ukafungwa kitambaa kwenye macho kisha ukatupwa katikati ya msitu, ukatelekezwa halafu ukaweza kukifungua hicho kitambaa si;
Lazima uanze kujiuliza uko wapi?
Kwanini uko hapo?
Nini lengo la wewe kuwepo hapo? Ufanye nini ili uweze kuondoka hapo?

Ndivyo ilivyo kwa Binadamu, tumejikuta tu duniani na tukaanza kujiuliza hayo maswali kisha tukaanza kujitafutia majibu ya kujiridhisha tu.

Wengine wakaanzisha dini ili kujibu.
Wengine wakaanzisha elimu ya sayansi.
Wote kwa sehemu yao kuna namna wamefanya vizuri lakini bado hawawezi kujibu maswali ya msingi.

Lakini sisi sote tunaona kuna nguvu ya asili tena kwa ushahidi wa macho inayoendesha Ulimwengu mzima na Maisha.

Nguvu ya Asili ni nini?

Ni mfumo wa nguvu uliopo tangu muda usiojulikana (Kwa maana hatujui sababu tumeukuta).

Huu mfumo wa nguvu unazalisha, hubadilika, huharibu, hujenga.

Sayansi ilifasiri kwamba - "Energy can neither be Created no destroyed but can change in different forms".

Hii nguvu Inaonekana kupitia maisha, kifo, mwanga, giza, mwendo, utupu, Graviti na muda.

Inaweza kupatana na akili kwamba nguvu hii tuliyoikuta huenda ndiyo chanzo cha Uhai na viumbe.
Lakini kwa namna ipi hatujui.

Lakini vipi kama dunia ilianza halafu nguvu ikaja baadaye?
Mmmmh!! Hapana ulimwengu mzima umeshikiliwa na nguvu hivyo inakuja akilini kwamba nguvu ndiyo ilianza.

Tatizo linakuja, Hakuna uwezekano wa kuwepo chanzo chake kikuu cha mwisho kwasababu kila chanzo ni matokeo ya chanzo kingine.

Hakuna kilicho juu ya mfumo wa nguvu kwasababu lazima kitakuwepo cha juu yake tena.

Kila chenye uhai na kisicho hai huenda kikawa ni sehemu ya mfumo huu wa nguvu.

Nguvu ya asili haihitaji kupewa sura au ibada kwasababu hakuna anayejua kuihusu.

Na inajieleza yenyewe kupitia mabadiliko ya moja kwa moja mfano Usiku na Mchana, Hali ya hewa, Dunia kuelea, Miti kukua, Watu kupumua......

Hii nguvu Si nafsi, si kiumbe, si kitu cha kuabudu.

Sayansi haiwezi kuelezea Atom zilizosababisha bingbang zilitokea wapi.

Vilevile dini haiwezi kuelezea Mungu alitokea wapi.

Hii inaunga mkono hoja yangu kwamba hakuna anayejua kwa uhakika na uthibitisho kuhusu chanzo cha kani ya nguvu na uhai yote ni kwasababu ilikuwepo kabla ya upeo wetu.

Je tutawezaje kujua historia ya kilichotutangulia kwa kubuni tu?
Hatuwezi kamwe hata tukijaribu kutumia vitu vilivyotuzunguka bado hatuwezi.

Na kuhusu Maadili.
Maadili hayana msingi halisi kutoka kwenye mfumo fulani.

Usahihi na makosa vinaonekana kwa matokeo yake mfano:

Kuua ni sawa na kuharibu mzunguko wa maisha.

Kusaidia ni sawa na kuimarisha mtiririko wa nguvu.

Hii ni kutambua uwiano wa matokeo.

Hivyo maadili chanzo chake ni sisi wenyewe binadamu kupitia utambuzi wetu.

Kuabudu eti kwakua tu lazima kuna chanzo kikuu cha maadili ni fikra na hisia za binadamu wenyewe katika kujaribu kutafuta maana ya Maisha.

Nguvu ya asili ipo, si kwa sababu ya hadithi za dini wala majaribio ya kisayansi bali kwa sababu ya matokeo halisi tunayoshuhudia.
Jua, mvua, kukua kwa viumbe, usiku na mchana na mengine kedekede.....

Hakuna anayejua chanzo kikuu cha nguvu ya asili, kwasababu kila nguvu itatakiwa kuwa na chanzo chake.

Ikitokea kuna chanzo kinadaiwa hakina chanzo hapo ndipo utalazimika uelezee kwa kina, Iliwezekana vipi?
Na umejuaje hilo?

Hivyo basi Anayeitwa Mungu mkuu chanzo cha ulimwengu hawezi kuwepo, na kama yupo bhasi atalazimika kuwa na chanzo na kama hatalazimika kuwa na chanzo bhasi inawezekana pia kila kitu hakilazimiki kuwa na chanzo tukiwemo sisi.

Je, alitokea sehemu ambayo ipo tayari?
Bhasi hakuumba kila kitu.

Au aliumba pa kutua kabla hajajiumba?
Wakati huo yeye akiwa wapi?
Palipoumbwa na nani?

Au nguvu ya asili ilimuumba?
Bhasi nguvu ya asili imemzidi nguvu.

#Mimi siamini, Naelewa.
#Jenga hoja katika kunielewesha na siyo kuniaminisha.
Ibn Unuq
 
Mpumbavu mwingine kaja,hawezi hata kutambua kwani nini unavidole vinalingana idadi Kila mkono? Kwa nini hukuzaliwa una vidole vitatu mkono mmja?
Hata ningezaliwa na vidole 50 bado ungeniuliza kwanini sifikirii sijazaliwa na vidole 300?

Hilo ni kosa la kimantiki katika kujenga hoja - logical fallacy.

Unatakiwa kuelezea kivipi kuzaliwa na vidole vitatu na siyo vitano kunahusiana mada husika?
 
Hakuna jipya juu ya nvhi. Unayoyanena, wapo waliyoyasema miaka 6,000 iliyopita. Ndiyo maana Mhubiri katika Zaburi, akasema:

Zaburi 53:1
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.

Kuna wakati mwanasayansi mmoha wa Urusi alisema kuwa hakuna Mungu, nao wanaoamini uwepo wa Mungu walimwuliza maswali mengi ambayo mwanasayansi alikosa majibu. Katika kuhitimisha, mwanasayansi yule akasema:

"There must be something, than which nothing can be done". Wale wanaomwamini Mungu wakamwambia kuwa, hicho ndiyo Mungu.
 
Kila kilichopo ni matokeo ya nguvu nyingine.

Hakuna mwanzo halisi.

Hakuna kilicho juu ya kingine.

Hakuna chanzo cha mwisho wala Mungu mkuu.

Kuna tu nguvu ya asili isiyoanzishwa wala kueleweka kihistoria ambayo mtiririko wake hauishi wala hakuna anayefahamu sababu wote tumejikuta tu duniani tayari.

Nguvu ya Asili ni nini?

Ni mfumo wa nguvu uliopo tangu muda usiojulikana.

Huu mfumo wa nguvu unazalisha, hubadilika, huharibu, hujenga.

Hata sayansi ilifasiri kwamba - "Energy can neither be Created no destroyed but can change in different forms".

Hii nguvu Inaonekana kupitia maisha, kifo, mwanga, giza, mwendo, utupu, Graviti na muda.

Hakuna chanzo chake cha mwisho kwasababu kila chanzo ni matokeo ya chanzo kingine.

Hakuna aliye juu ya mfumo wa nguvu.

Kila chenye uhai na kisicho hai ni sehemu ya mfumo huo wa nguvu.

Nguvu ya asili haihitaji kupewa sura au ibada kwasababu Inajieleza kupitia mabadiliko ya moja kwa moja mfano Usiku na Mchana, Hali ya hewa, Dunia kuelea, Miti kukua, Watu kupumua......

Hii nguvu Si nafsi, si kiumbe, si kitu cha kuabudu.

Sayansi haiwezi kuelezea Atom zilizosababisha bingbang zilitokea wapi.

Vilevile dini haiwezi kuelezea Mungu alitokea wapi.

Hii inaunga mkono hoja yangu kwamba hakuna anayejua Chanzo cha kani ya Nguvu na Uhai kwasababu ilikuwepo kabla ya upeo wetu.

Je tutawezaje kujua historia ya kilichotutangulia kwa kufikiri tu?

Kuhusu Maadili.
Maadili hayana msingi halisi kutokea mfumo fulani.

Usahihi na makosa vinaonekana kwa matokeo yake mfano.

Kuua = kuharibu nguvu ya mzunguko wa maisha.

Kusaidia = kuimarisha mtiririko wa nguvu.

Hii si Mungu, ni kutambua uwiano wa matokeo.

Hivyo maadili chanzo chake ni sisi wenyewe binadamu kupitia utambuzi wetu.

Hivyo Sioni haja ya kuabudu nguvu ya asili.

Mfumo wa kuabudu ni fikra na hisia za binadamu wenyewe katika kujaribu kutafuta chanzo cha Maisha.

Nguvu ya asili ipo, si kwa sababu ya hadithi za dini, bali kwa sababu ya matokeo halisi tunayoshuhudia.

Hakuna chanzo kikuu cha nguvu ya asili, kwasababu kila nguvu ina chanzo chake.

Ikitokea kuna nguvu inadaiwa haina chanzo hapo ndipo utalazimika uelezee kwa kina, Iliwezekana vipi?
Na umejuaje hilo.

#Mimi siamini, Naelewa.
#Jenga hoja katika kunielewesha na siyo kuniaminisha.
Ibn Unuq
Inawezekana nguvu isiyo na akili wala uelewa ikaumba vitu vyenye akili na uelewa? Bado kuna kitu hatujui. Binafsi Sikupingi mawazo yako moja kwa moja ila bado haya mawazo hayatoshi kufanya hitimisho. Unless tupate uthibitisho kuwa uelewa na akili haikuwa sehemu ya uumbaji, ni matokeo tu hapo tutakuwa na hitimisho kuwa MUNGU(Hiyo guvu) yupo ila hana akili wala uelewa.
 
Kila kilichopo ni matokeo ya nguvu nyingine.

Hakuna mwanzo halisi.

Hakuna kilicho juu ya kingine.

Hakuna chanzo cha mwisho wala Mungu mkuu.

Kuna tu nguvu ya asili isiyoanzishwa wala kueleweka kihistoria ambayo mtiririko wake hauishi wala hakuna anayefahamu sababu wote tumejikuta tu duniani tayari.

Nguvu ya Asili ni nini?

Ni mfumo wa nguvu uliopo tangu muda usiojulikana.

Huu mfumo wa nguvu unazalisha, hubadilika, huharibu, hujenga.

Hata sayansi ilifasiri kwamba - "Energy can neither be Created no destroyed but can change in different forms".

Hii nguvu Inaonekana kupitia maisha, kifo, mwanga, giza, mwendo, utupu, Graviti na muda.

Hakuna chanzo chake cha mwisho kwasababu kila chanzo ni matokeo ya chanzo kingine.

Hakuna aliye juu ya mfumo wa nguvu.

Kila chenye uhai na kisicho hai ni sehemu ya mfumo huo wa nguvu.

Nguvu ya asili haihitaji kupewa sura au ibada kwasababu Inajieleza kupitia mabadiliko ya moja kwa moja mfano Usiku na Mchana, Hali ya hewa, Dunia kuelea, Miti kukua, Watu kupumua......

Hii nguvu Si nafsi, si kiumbe, si kitu cha kuabudu.

Sayansi haiwezi kuelezea Atom zilizosababisha bingbang zilitokea wapi.

Vilevile dini haiwezi kuelezea Mungu alitokea wapi.

Hii inaunga mkono hoja yangu kwamba hakuna anayejua Chanzo cha kani ya Nguvu na Uhai kwasababu ilikuwepo kabla ya upeo wetu.

Je tutawezaje kujua historia ya kilichotutangulia kwa kufikiri tu?

Kuhusu Maadili.
Maadili hayana msingi halisi kutokea mfumo fulani.

Usahihi na makosa vinaonekana kwa matokeo yake mfano.

Kuua = kuharibu nguvu ya mzunguko wa maisha.

Kusaidia = kuimarisha mtiririko wa nguvu.

Hii si Mungu, ni kutambua uwiano wa matokeo.

Hivyo maadili chanzo chake ni sisi wenyewe binadamu kupitia utambuzi wetu.

Hivyo Sioni haja ya kuabudu nguvu ya asili.

Mfumo wa kuabudu ni fikra na hisia za binadamu wenyewe katika kujaribu kutafuta chanzo cha Maisha.

Nguvu ya asili ipo, si kwa sababu ya hadithi za dini, bali kwa sababu ya matokeo halisi tunayoshuhudia.

Hakuna chanzo kikuu cha nguvu ya asili, kwasababu kila nguvu ina chanzo chake.

Ikitokea kuna nguvu inadaiwa haina chanzo hapo ndipo utalazimika uelezee kwa kina, Iliwezekana vipi?
Na umejuaje hilo.

#Mimi siamini, Naelewa.
#Jenga hoja katika kunielewesha na siyo kuniaminisha.
Ibn Unuq
UMESHA SIBITISHA UWEPO WA MUNGU KWA KUKILI KUWA NGUVU ZA ASILI ZIPO NA SISI BINADAMU NI SEHEMU YA MATOKEO YA HIZO NGUVU.
 
UMESHA SIBITISHA UWEPO WA MUNGU KWA KUKILI KUWA NGUVU ZA ASILI ZIPO NA SISI BINADAMU NI SEHEMU YA MATOKEO YA HIZO NGUVU.
hakika kasema hyo nguvu haiwezi tengenezwa wala kuharibiwa ila inabadilika umbo, hii kama sio sifa ya mungu itakuwa ni nini tena, huna haja ya kukubaliana na mipango na taratibu zake ni sawa, ila tunabidi tu aknowledge uwepo wake
 
Tena ikiwa hiyo nguvu ndiyo imefanya mwanadamu wenye akili na utashi na ufahamu basi ni ushahidi kuwa nguvu ya asili inaweza kufanyika utashi na akili na ufahamu...hivyo hiyo nguvu INA UTASHI INA UFAHAMU NA INA AKILI ...ushahidi wa hayo ni sisi binadamu tulio fanyika kutokana na hiyo nguvu tunayo hayo ...HIVYO UTASHI NA UFAHAMU NA AKILI NI ZAO LA HIYO NGUVU YA ASILI ....HIVYO HIYO NGUVU YA ASILI INAJITAMBUA INA UTASHI NA AKILI..
AND THIS IS THE MEANING OF GOD
 
Back
Top Bottom