Hakuna mtu wa England anayejishughulisha na Scotland

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Muungano wa JMTZ ni copy & paste ya Muungano wa nchi ya Uingereza ambapo England ndo nchi kubwa, lkn huwezi kukuta hata siku moja mtu wa England akijishughulisha na mambo ya Scotland au sijui Ireland, watu wa huko Scotland ndiyo wanaohangaika kudai haki zao kutoka England, lkn hapa kwetu ni kinyume, watu wa Bara ambao ndio wengi na wanufaika wakubwa wa Muungano ndiyo walalamikaji wakuu wa mambo ya Zanzibar ambayo ina watu ~ milioni 1, ni ajabu Zanzibar inawauma na kuwasumbua kuliko Wazanzibari wenyewe. Tanzania bara watu > milioni 45 vs Zanzibar kama milioni 1.

Swali kwenu Watanzania Bara, hamna matatizo mengine zaidi ya Zanzibar?
 
Nadhani umeongea verse versa, Wazanzibar ndiyo wanalalamika sana kuhusu muungano kuliko wabara.
 
Nadhani umeongea verse versa, Wazanzibar ndiyo wanalalamika sana kuhusu muungano kuliko wabara.

Labda siyo hapa JF, hapa walalamikaji wa Muungano ni Wabara, ndo maana nashangaa, ...
 
Labda siyo hapa JF, hapa walalamikaji wa Muungano ni Wabara, ndo maana nashangaa, ...
Haiwezi kuwa JF kwa sababu JF na yenyewe ni ya Wabara! It's unfortunately kwamba mzalendo.net hivi sasa haipatikani hewani, or else ningekuambia tembelea huo mtandao ambao ilikuwa ndo JF ya Wa-Zanzibari! Ungetembelea huko ukaone Mkoloni Tanganyika anavyojadiliwa!!

In short, hata hoja ya Tanganyika kuwa Mkoloni ni hoja ya Wazanzibari wenyewe!!!
 
Back
Top Bottom