Hakuna mtu rahisi kumdhalilisha kama mwalimu

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,381
2,553
Poleni sana ndugu zangu. Nyie ni watu wapole sana ,nidhamu yenu ni ya juu kabisa sijapata kuona.

Mmepewa jukumu la mhimu la kuandaa taifa huko shuleni. Taifa linawategemea . Kazi yenu ni nyeti mno na ya mhimu sana. Hii inatoka na ukweli kuwa taifa linaandaliwa shuleni ,siyo mitani,sokoni au kwenye baa.

Jambo la ajabu kabisa hivi sasa imeibuka tabia ya kudhalilisha walimu. Huwa sielewi kwa nini jamii yetu hata viongozi inamuona mwalimu kama kiumbe dhaifu asiyestahili heshima .Poleni sana walimu

Naomba niwatie moyo msikate tamaa . Taifa linawategemea . Kazi yenu ni ya mhimu sana kuliko wajinga wachache wanavyofikilia . Mungu anayaona mateso yenu na pia amekisikia kilio chenu. Tuendelee kuwafundiaha watoto wetu iko siku machozi yenu yatafutwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasiasa na watendaji wanawadhihaki walimu. Walimu ni wavumilivu kwa kiwango kikubwa sana, mishahara yao kiduchu, wanaishi mazingira magumu, mazingira ya kazi ni magumu, hawana motisha yoyote kutoka kwa wazazi na viongozi, mishahara yao imejaa makato. Baadhi ya viongozi wanafikiri kumkagua na kumsimamia mwalimu nikumtukana na kumdhalilisha. Viongozi na wadau wa elimu badilikeni kazi ya ualimu inahitaji kujitoa na udhalendo hivyo wekezeni katika kuandaa mazingira mazuri kwa walimu na wanafunzi, boresheni mishahara yao, mjikite katika kusikiliza changamoto zao zaidi kuliko kutoa maagizo, toeni motisha na kuwatia moyo walimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaaaa, narudia tena, tz ya leo kuna tofauti ndg sana kati ya kuolewa na kuajiriwa, sio mwl pekee, kwaio hata wewe hapo kama maisha yako bd yanaendeshwa na sign book au fingerprint usijipe matumain tofaut yako na uliwataja ni negligible, ila umefanya vzr kuwatia moyo.
 
Kila nikikutana na Mwalimu aliyewahi Kufundisha Shule niliyosoma namuombea na kumpatia Nauli.
 
Mambo yameenda chini juu kutona na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii
Hapo kabla walimu walikichaguliwa toka ktk madaraja ya juu ya waliofaulu na ndivyo inavyotakikana na mambo ya nguvu ya soko ktk ajira wakati huo hayakuwapo
Hivi sasa ajira zinaamuliwa na nguvu za soko waliofaulu vizuri wanawindwa na wanaolipa mishahara vizuri na kwakuwa serikali hailipi vizuri basi inabidi ianze kuokoteza mabaki hayo ndio matokeo yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasiasa na watendaji wanawadhihaki walimu. Walimu ni wavumilivu kwa kiwango kikubwa sana, mishahara yao kiduchu, wanaishi mazingira magumu, mazingira ya kazi ni magumu, hawana motisha yoyote kutoka kwa wazazi na viongozi, mishahara yao imejaa makato. Baadhi ya viongozi wanafikiri kumkagua na kumsimamia mwalimu nikumtukana na kumdhalilisha. Viongozi na wadau wa elimu badilikeni kazi ya ualimu inahitaji kujitoa na udhalendo hivyo wekezeni katika kuandaa mazingira mazuri kwa walimu na wanafunzi, boresheni mishahara yao, mjikite katika kusikiliza changamoto zao zaidi kuliko kutoa maagizo, toeni motisha na kuwatia moyo walimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umeongea ukweli mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni sana ndugu zangu. Nyie ni watu wapole sana ,nidhamu yenu ni ya juu kabisa sijapata kuona.

Mmepewa jukumu la mhimu la kuandaa taifa huko shuleni. Taifa linawategemea . Kazi yenu ni nyeti mno na ya mhimu sana. Hii inatoka na ukweli kuwa taifa linaandaliwa shuleni ,siyo mitani,sokoni au kwenye baa.

Jambo la ajabu kabisa hivi sasa imeibuka tabia ya kudhalilisha walimu. Huwa sielewi kwa nini jamii yetu hata viongozi inamuona mwalimu kama kiumbe dhaifu asiyestahili heshima .Poleni sana walimu

Naomba niwatie moyo msikate tamaa . Taifa linawategemea . Kazi yenu ni ya mhimu sana kuliko wajinga wachache wanavyofikilia . Mungu anayaona mateso yenu na pia amekisikia kilio chenu. Tuendelee kuwafundiaha watoto wetu iko siku machozi yenu yatafutwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Waalimu sio wa pole tu..... ila ule umasikini au maisha yao duni yanawafanya kua wapole watu wa kujipendekeza, umbeya unafiki nk wanasiasa wegi wanatumia maisha yao duni kuwadhalilisha nawenyewe wako tayari kudhalilishwa, waalimu wa Tz hawana misimamo hawana umoja hawana malengo....ndo maana unaona wako hivyo walivyo......

Tuwatie moyo ni watu mhimu sana katika taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom