Hakuna mtu anaejali maisha yako zaidi yako mwenyewe acha kujishtukia

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,216
HAKUNA MTU ANAEJALI MAISHA YAKO ZAIDI YAKO MWENYEWE ACHA KUJISHTUKIA

Kuna wakati ambapo tunajali sana kuhusu watu wengine wanavyojali kuhusu maisha yetu.Tunafikiri kwamba watu wengine wanatufuatailia kila tunachofanya na hivyo kuhofia watatuchukuliaje hasa kama tutashindwa.

Ukweli ni kwamba hakuna anayejali maisha yako zaidi yako mwenyewe. Hakuna ambaye anakosa usingizi akifikiria wewe unafanya nini.
Hata kama atakuona ukifanya na kukupinga au kukukatisha tamaa, dakika chache baadae atakuwa maeshasahau.

Hakuna anajali maisha yako zaidi yako wewe kwa sababu kila mtu ametingwa na maisha yake. Kila mtu anafikiria matatizo na changamoto anazokutana nazo kwenye maisha yake na hivyo hana muda mwingi wa kukufuatilia wewe kama unavyofikiri.

Fanya kile ambacho unaona ni sahihi kwako. Usiangalie au kufikiria wengine wanasemaje au watakufikiriaje, wao wenyewe wametingwa na maisha yao.
 
Mbona kwetu wanapiga majungu sana kila ukikatiza na gari lako, unaona wanakunyooshea vidole.....
 
Hapo umezungumza kinegative zaidi lakini katika hali halisi ukweli ni kuwa FURAHA ya kweli inakuja baada yakufanya maisha ya wengine kuwa mazuri na yenye furaha tofauti na hapo ni ubinafsi na uchoyo na matokeo yake ni mtu kuwa kichaa unayependeza.....
 
Nimecheka sana kwa falsafa uliyoitumia mkuu.
 
Hapo umezungumza kinegative zaidi lakini katika hali halisi ukweli ni kuwa FURAHA ya kweli inakuja baada yakufanya maisha ya wengine kuwa mazuri na yenye furaha tofauti na hapo ni ubinafsi na uchoyo na matokeo yake ni mtu kuwa kichaa unayependeza.....

Hapo umenena mkuu. Kula like yangu.
 
HAKUNA MTU ANAEJALI MAISHA YAKO ZAIDI YAKO MWENYEWE ACHA KUJISHTUKIA

Kuna wakati ambapo tunajali sana kuhusu watu wengine wanavyojali kuhusu maisha yetu.Tunafikiri kwamba watu wengine wanatufuatailia kila tunachofanya na hivyo kuhofia watatuchukuliaje hasa kama tutashindwa.

Ukweli ni kwamba hakuna anayejali maisha yako zaidi yako mwenyewe. Hakuna ambaye anakosa usingizi akifikiria wewe unafanya nini.
Hata kama atakuona ukifanya na kukupinga au kukukatisha tamaa, dakika chache baadae atakuwa maeshasahau.

Hakuna anajali maisha yako zaidi yako wewe kwa sababu kila mtu ametingwa na maisha yake. Kila mtu anafikiria matatizo na changamoto anazokutana nazo kwenye maisha yake na hivyo hana muda mwingi wa kukufuatilia wewe kama unavyofikiri.

Fanya kile ambacho unaona ni sahihi kwako. Usiangalie au kufikiria wengine wanasemaje au watakufikiriaje, wao wenyewe wametingwa na maisha yao.

Well said mzee...Hapa watu wengi hasa vijana wa mjini panatusumbua..n ujinga wa hali ya juu kufanya mambo ili kulidhisha watu wengine kisa watanionaje..!
 
Back
Top Bottom