Hakuna msafi hata mmoja... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna msafi hata mmoja...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanamageuko, Dec 2, 2010.

 1. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Katika wote wanaohama vyama, kutoka kimoja kwenda kingine woooooote ni waganga njaa. Hawafai kabisa kwani wananuka shombo la uchu wa madaraka na si wapiganaji wa kweli wa ukombozi bali matumbo na malengo yao yaliyojificha. hawapaswi kuaminiwa hata kupewa amana ya kutupa taka.

  Ninyi watazameni na mchunguze kwa makini mtaona wanakoelekea... (nimemaanisha wote na si baadhi hapo naomba nieleweke vema)

  Ni kweli wanasifiwa baadhi yao, lakini wanaowasifu kuna maswali hawawaulizi. Mpiganaji wa kweli anajulikana. vita anaipigania ndani mwake ili kuwe safi. Matope yakiingia kwenye nyumba hatuhami bali tunasafisha nyumba hiyo ili iwe safi. Nguo ikichafuka hatuitupi bali twaifua ili tuendelee kuivaa. Kama tunazikimbia kasoro badala ya kuzirekebisha ina maana hatuna uwezo na majawabu ya matatizo...>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

  Mwanasiasa safi ni yule anaejua kupambana na kutengeneza sehemu yake bila kubabaika, wapo baadhi yao, wanasemwa lakini wamebaki katika misimamo yao HAWAYUMBI WALA HAWAHAMI!

  Hayo ndiyo yangu kwa leo

  Karibuni....
   
 2. ghumpi

  ghumpi Senior Member

  #2
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Asante mkuu, nakubaliana nawe asilimia elfu moja kwa elfu moja
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  :party:
   
Loading...