Hakuna msafi hata mmoja...

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,602
5,569
Katika wote wanaohama vyama, kutoka kimoja kwenda kingine woooooote ni waganga njaa. Hawafai kabisa kwani wananuka shombo la uchu wa madaraka na si wapiganaji wa kweli wa ukombozi bali matumbo na malengo yao yaliyojificha. hawapaswi kuaminiwa hata kupewa amana ya kutupa taka.

Ninyi watazameni na mchunguze kwa makini mtaona wanakoelekea... (nimemaanisha wote na si baadhi hapo naomba nieleweke vema)

Ni kweli wanasifiwa baadhi yao, lakini wanaowasifu kuna maswali hawawaulizi. Mpiganaji wa kweli anajulikana. vita anaipigania ndani mwake ili kuwe safi. Matope yakiingia kwenye nyumba hatuhami bali tunasafisha nyumba hiyo ili iwe safi. Nguo ikichafuka hatuitupi bali twaifua ili tuendelee kuivaa. Kama tunazikimbia kasoro badala ya kuzirekebisha ina maana hatuna uwezo na majawabu ya matatizo...>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Mwanasiasa safi ni yule anaejua kupambana na kutengeneza sehemu yake bila kubabaika, wapo baadhi yao, wanasemwa lakini wamebaki katika misimamo yao HAWAYUMBI WALA HAWAHAMI!

Hayo ndiyo yangu kwa leo

Karibuni....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom