kibananhukhu
JF-Expert Member
- Jul 6, 2009
- 366
- 166
Wana JF, Nisaidieni. Kinachojiri si Mgogoro wa Dini Tanzania. Labda kama Prof. Lipumba ana ushahidi kuwa wale waliolipua Makanisa, walioiba vifaa vya ibada na kujajisi Msahafu ni WAUMINI. Nadhani kama kuna kitu cha msingi cha kufanya Lipumba, ni KUKEMEA Walionajisi Msahafu (Wahuni na wasiofikiri), KUKEMEA Waliolipua Makanisa na kuiba vifaa ndani ya NYIMBA YA MUNGU. Mgogoro unahitaji pande mbili. Aliyenajisi Msahafu wala Wakristo hawamfahamu na hawakumtuma, sheria zipo. Waliobomoa makanisa na kunajisi nyumba za MUNGU, (WAHUNI) hawakutumwa na waislam. Uislam ni undugu na AMANI. Ukristo ni Upendo na AMANI. Kitabu cha Agano la kale na Enjili vinaheshimiwa sana na dini zote. YESU pia anaheshimiwa na dini zote. Kinachohitajika ni kukemea na kuwalaani WAHUNI wote na kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake. Nadhani Profesa Hataeleweka na watu wengi. Hakujatokea Tanzania Mgogoro wa Wakristo na Waislam. Tusiwetete wahuni wanaojituma au kutumiwa na WAHUNI. Sijawahi sikia Tanzania Ugomzi wowote kuwa WAISLAM na Wakristo wamegombana. Waislamu na Wakristo Tanzania tusiingizwe kwenye fujo za Wahuni na watu wanaotaka kutumia mbinu za kigaidi kuchafua vitabu vya ibada na kulipua Nyumba za Ibada. Mwisho wake hautakuwa mzuri kama tukiliendekeza hilo. Sote turejee maana ya neno Mgogoro. Unahitaji pande mbili. Pande hizo hazipo Tanzania. Ninakubali maoni ya Upanda wa pili na kusahihishwa.