Hakuna mgogoro CUF -Seif | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna mgogoro CUF -Seif

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Dec 17, 2011.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Seif akilonga kutumia kodi za walala hoi wa Zanzibar kasema hawana mgogoro na kama kuna mtaka uongozi afuate taratibu za kawaida za Baraza lao KAFU .

  Kuhusu Katiba yeye analia na Zanzibar tu na si Tanzania .

  Source mie mwenyewe kama hutaki acha kuchangia pita .
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ila tu kuna jubile ya ndoa yake na CCM ndio inaendelea hivi sasa.
   
 3. rwamashugi

  rwamashugi Member

  #3
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndoa imekolea na kumziba macho na masikio huyu Mrs c...m
   
 4. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Watu wanatoana ngeu yeye anasema hamna mgogoro!Hizi ni dalili za kushindwa.
   
 5. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Teh teh teh! Mwaka huu mumeingia choo cha kike Watanganyika munajuta kujuana na Wazanzibar! Na Hamad Rashid anataabishwa na radhi za baba yake mzanzi, kwa kauli yake HR alitamka tena mbele ya mkutano wa hadhara na Maalim akiwepo ya kwamba Marehemu baba yake kabla ya kufa alimuusia nini yeye akiwa kama Baba yake mzazi (Mzee Rashid Muhammed R.I.P) juu ya Maalim Seif? Hem litafteni hili JAMBO ndo mutajua nini kinamtesa Huyu mjamaa.
   
 6. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  naona hajui hata kujibu hoja wafuasi na wapenzi wa cuf wamepigana mapanga badouna sema hakuna mgogoro? labda angesema unashughulikiwa au umeisha au ......
   
 7. h

  hamud Member

  #7
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  mpemba mbishi unaongea ukweli mtupu mkuu kuhusu hamad rashid muhamed,kwani mkutano wa ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mkuu,ulifanyika uwanja wa gombani ya kale pale chake chake,:A S 465:alisema usia wa baba yake ni kuhakikisha awe na heshima na adabu kwa seif sharif hamad, muulizeni je amesahau kauli yake ..ajuwe hata akiunda chama atakuwa peke yake huyo,chama cha siasa sio ****** kila mtu anaweza kuwa nayo
   
 8. h

  hamud Member

  #8
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga,cuf ndio muasisi wa mageuzi tanzania
   
 9. P

  PreZ 2B EL Member

  #9
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm ndo mwasisi wa mapinduzi tanzania
   
 10. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Humud mimi nilikuwepo pale Gombani pia maneno yale alikua anayarudia rudia kila alipokua akiwahutubia wananchi wa Jimbo lake la Wawi, mimi huyu Hamad Rashid namjua sana na ni jamaa yangu wa Damu, ndio maana hua nawashangaa sana hawa Watanganyika wanapomuona Kichwa na kufika hadi kumlinganisha na kuona eti anaweza Mapambano na Shujaa wa Zanzibar Maalim Seif!!! Kiufupi Hamad Rashid anateswa na Radhi za Baba yake juu ya Wasia aliopewa dhidi ya Maalim Seif.
   
 11. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Maalim seif anasumbuliwa na hangover ya ulevi wa madaraka aliyopewa na chama cha mapinduzi!hangover ikiisha akili yake itafanya kazi sawasawa kama zamani!
   
 12. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huu ni wivu juu ya Wazanzibar kwa kua wameamua kuungana! Kwa sasa hakuna cha U-CUF wala U-CCM kuna UZANZIBARI kwanza, Wewe hujaona yale makaratasi yenye kinyesi aliyokuja nayo Sitta yalivyoraruliwa! Achana na Hamad Rashid huyu tumeshamfahamu ni kibaraka wa CCM huko Tanganyika wanamtumilia kwa maslahi yao. Mbona kama anaweza Mapambano haji Pemba akasema hayo anayoyadai, thubutuuuuuu!!
   
 13. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kwani cuf ni chama cha wapemba mpaka iwe lazima yeye aje aifanyie hiyo cuf yake huko?cuf iko dunia nzima ndio maana Lipumba ni cuf kuliko wewe lakini yuko marekani!
   
 14. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapa ndio mwisho wako wa kujibu! Si kosa lako bali Serikali yako kwa kutokuimarisha mfumo wa elimu na kupatikana wenye elimu mbovu kama wewe!!!!
   
 15. c

  chama JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mmmh! mpemba mbishi upo uhamishoni UK au Canada? Kwani hapo awali wapemba walipigania nini? Na hadi sasa hivi wamefanikiwa kitu gani? Je usawa kwa wapemba ni kwa Maalim Seif kupata umakamu au wapemba nao wapate haki sawa na waunguja? Hili neno serikali yako umemaanisha kitu gani hebu nipe ufafanuzi kama na wewe ni mtu wa Oman tukujibu ki Oman

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 16. Fatal5

  Fatal5 Senior Member

  #16
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [h=1]Hakuna mgogoro CUF, zilizopo ni chokochoko – M.Seif[/h][​IMG] Na Hassan Hamad
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema miongoni mwa changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi katika marekebisho ya katiba mpya ya Tanzania ni utaratibu wa kumpata Rais wa Jamhuri ya Muungano, ili wazanzibari nao waweze kuitumikia nafasi hiyo.
  Amesema utaratibu uliopo sasa wa kumpata mgombea wa urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaikosesha fursa Zanzibar, na kutaka kuwepo ya utaratibu kwa nafasi hiyo kutumika kwa awamu baina ya bara na visiwani.

  Akizungumzia kuhusu shutuma mbali mbali ndani ya Chama Cha CUF ambazo zimechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari katika siku za hivi karibuni, Maalim Seif ambaye pia ni katibu mkuu wa CUF amesema hakuna mgogoro ndani ya chama hicho bali zilizopo ni chokochoko tu.
  Amesema utaratibu wa chama hicho unaruhusu kukosolewa mtu yoyote kupitia vikao vya chama na sio kupigana madongo kwenye vyombo vya habari.
  kama kuna mtu mwenye hoja aziwasilishe kwenye vikao halali vya chama na sisi tutazijadili kwa kina, kwa hiyo Mheshimiwa Hamad Rashid na wenziwe kama wana hoja tutaonana kwenye vikao, na yeyote mwengine mwenye ubavu tushindane kwenye mkutano mkuu alisema Maalim Seif akionesha kukerwa na suala hilo.
  Kuhusu shutuma za kumuandaa Mheshimiwa Ismail Jussa kuwa katibu mkuu wa Chama hicho siku zijazo, Maalim Seif amekana shutuma hizo na kusema kuwa wanaohusika kupendekeza nafasi hizo ni mkutano mkuu wenye wajumbe kutoka bara na visiwani.
  Chama hiki si Changu, na katibu mkuu kuhojiwa ndani ya chama chetu sio tatizo, anaweza kuhojiwa wakati wowote kupitia utaratibu unaokubalika, na anayetaka nafasi ya ukatibu mkuu aje anakaribishwa wakati utakapofika, aliongeza.
  ......................................................................................................................................................................................................

  vile vile tunahitaji Muengezeko zaidi ya wa waZanzibari kuingia katika jeshi la ulinzi la Tanzania (JWTZ) Na muengezekowa mabalozi

  wa nchi za nje watokee Zanzibar.

  Kama wa Tanganyika hamutakubaliana na vipengele hivyo basi Muungano huu fake utakuwa mwisho Chumbe.:A S 465:
   
 17. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mwasisi wa mapinduzi ni watanzania
   
 18. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama hicho hakimuogopi mwanachama yeyote na kwamba ikibidi kitafanya maamuzi magumu.

  Aidha, amesema asingependa kulumbana wala kujibizana na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed, ambaye amesema Baraza Kuu la chama ndilo litakaloamua kuhusu suala la sasa la mgogoro unaomhusisha mbunge huyo na chama hicho.

  Aidha, Maalim Seif amesema ye yote mwenye ubavu wa kupimana naye, ajitokeze mbele ya Mkutano Mkuu wa CUF ili wanachama waamue.

  Maalim Seif aliyasema hayo jana wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari mjini Unguja, katika mkutano mahususi alioutisha kuzungumzia mwaka mmoja wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ambayo yeye ni Makamu wa Kwanza wa Rais.

  Alisema kwa msimamo wake, CUF ni taasisi yenye utaratibu wake kwa mujibu wa Katiba, na kwa msingi huo, asingependa kuona chama hicho kinaingizwa katika malumbano kwenye vyombo vya habari.

  “Nisingependa kujibizana katika vyombo vya habari, tutaonana katika vikao…ye yote mwenye hoja zake ajipange kuzungumza lolote,” alieleza Katibu Mkuu wa CUF.

  Alisema kama mtu ana matarajio ya kuwa Katibu Mkuu ni haki yake ya kugombea nafasi yoyote katika chama wakati wa uchaguzi ukifika.

  “Sasa kama mtu ana ambition (dhamira) ni haki yake, ni haki ya kila mwanachama kugombea nafasi yoyote muda ukifika. Baraza Kuu limeamua kuwa uchaguzi utafanyika mwaka 2014.

  “Sasa leo ni mwaka 2011, mtu anasema anataka ukatibu mkuu, je, ni njia sahihi? Haki ipi anayotaka?

  Kama nikiamua, sijasema naondoka, kama nikiamua, kama mtu ana ubavu basi tukutane katika Mkutano Mkuu na wanachama wataamua,” alieleza Seif.

  Alisema kwake yeye hakuna mgogoro ndani ya CUF, kwani mwezi uliopita walifanya kikao cha Baraza Kuu ambacho kilikwenda vizuri.

  “Watu wana haki ya kunikosoa, wana haki ya kufanya hivyo, nami napenda iwe hivyo kwa maslahi ya chama, lakini sipendi kulumbana katika magazeti.

  “Vikao vya chama vitumike, sitaki kugombana na mtu, kulumbana wala kujitetea hapa. Tunaendesha vikao kwa ukweli na uwazi,” alisema Maalim Seif.

  Aidha, Katibu Mkuu huyo alisema CUF haimuogopi mtu ye yote na kwamba kitafanya maamuzi hata magumu ikibidi ili kulinda maslahi ya chama hicho.

  Kuhusu kumuandaa Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu kumrithi wadhifa wake, Maalim Seif alikanusha hilo na kueleza kwamba hana sababu ya kufanya hivyo, kwa sababu hata yeye binafsi hajasema kama hatatetea kiti chake.

  “Eti ninamtayarisha Jussa kuwa Katibu Mkuu, nani kawaambia? Kwani naondoka katika nafasi yangu? Hao wanaosema hivyo wana ajenda zao,” alieleza.

  Alisema yote yanayofanywa sasa na Hamad ambaye pia aliwahi kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ni juu ya Baraza Kuu kuamua kama amekosea au yuko sahihi.

  Hamad amekuwa katika mgogoro kwa miezi sasa na uongozi wa CUF unaomtuhumu kwamba anajiandalia mazingira ya kuwania nafasi ya Katibu Mkuu.

  Mgogoro wao umesababisha mgawanyiko kwa wanachama nchini na wiki iliyopita, hali ya hewa ilichafuka katika baadhi ya matawi jijini Dar es Salaam na kusababisha umwagaji wa damu.

  Hamad amekaririwa akisema yu tayari kujitetea mbele ya vikao vya chama akiitwa hata leo, lakini pia ameripotiwa kueleza kuwa atapambana kwa kadri ya uwezo wake ndani ya chama hicho.
   
 19. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  The Citizen Chief Reporter
  Zanzibar. Zanzibar First Vice President Mr Seif Shariff Hamad has asked those eyeing his position as Civic United Front (CUF) Secretary General to hold their horses because he hasn’t made a decision to retire from politics.
  However, Mr Hamad, highly regarded as the doyen of political opposition in Zanzibar who has led CUF for nearly 20 years, maintains that he does not fear to be challenged for the party’s top executive post.He has welcomed whoever wishes to challenge him to do so in the next internal elections scheduled for 2014.
  Speaking at a press conference in Zanzibar yesterday, Mr Hamad said he was perplexed why some people were talking about CUF elections now, while the intraparty polls were three years away.

  This was the first time that the CUF secretary general was reacting publicly to a simmering leadership row sparked off by Wawi MP Mr Hamad Rashid Mohammed, who has dared his boss to step aside from the post.
  Mr Mohammed has launched a campaign to market himself as a suitable replacement for Mr Hamad, in a public show that has irked the party’s hierarchy, that sparked a bloody clash among rival supporters in Dar es Salaam last week.

  The tone of Mr Hamad’s sentiments suggested that the ping-pong over the party secretary generalship was a minor issue, implying that the thrust of the press conference was to sketch highlights of the first year performance of the Government of National Unity (GNU) formed jointly with Chama Cha Mapinduzi (CCM) following the 2010 General Election.
  He was accompanied by at least five GNU ministers and other top government officials during the press briefing session held at the old House of Representatives chamber now serving as an Information auditorium.
  Responding to media queries, and in what was an apparent reference to Mr Mohammed whose move could split the party, Mr Seif said he would refrain from discussing the party’s affairs through the media.

  He however said it was wrong to paint a picture of a succession war within CUF at this moment. “I have not yet decided whether to run again for the post or not. I will do so when time is convenient,” he noted.
  He said all matters concerning CUF, including elections, are discussed by the party’s supreme bodies, including its Governing Council. “During such sessions, we discuss our issues candidly and take hard decisions if need be,” added Mr Hamad.
  The CUF leader refuted claims that he was not challengeable. “Who says I am unchallengeable? If there is a leader who is grilled most during the party’s meetings that leader is me,” said Mr Hamad.

  He also denied reports by those in Mr Mohammed’s camp that he was grooming someone else to succeed him, citing his relative old age as a push-factor.
  The Wawi MP himself says he wants to dislodge Mr Hamad because as Zanzibar’s First VP, he could no longer serve the political interests of the opposition party efficiently.
  House of Representative member for Mji Mkongwe and CUF youthful deputy secretary general for Zanzibar, Mr Ismail Jussa, is among those rumoured to be gearing up to succeed Mr Hamad.Mr Jussa has however distanced himself from any such plot, and on Friday told The Citizen on Sunday that he was contemplating quitting active politics come 2015. He accused Mr Mohammed of allegedly being “selfish and power hungry.”

  At yesterday’s media briefing, Mr Hamad defended himself from the accusations of grooming a successor, pointing out that he could not do such a thing since CUF was not his personal property. He said Mr Jussa was a capable leader in his own right and was elected deputy secretary general through a secret ballot.

  CUF voted to elect Mr Jussa and Mr Julius Mtatiro acting secretaries general for Zanzibar and Mainland Tanzania respectively, following the drafting of Mr Hamad into the GNU.Like Mr Hohammed, a former Cabinet minister and CUF founder member, those agitating for changes argue that the party has lost its political clout because it could not take the government head on, as its leaders were seen as advancing the same cause with the ruling party.

  CUF performed disastrously in the 2010 General Election in the Mainland and was dethroned by Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) as the main opposition party in Parliament.
  CUF had held the position since 1995.

  In an immediate rejoinder, Mr Mohammed yesterday said he was pleased Mr Hamad had reiterated the need for party issues to be discussed in its supreme organs.The Wawi MP reiterated his stand that he will oppose Mr Hamad in appropriately held elections. However, he expressed misgivings over media reports that quoted Mr Hamad as labelling him a traitor, thereby trashing his candidature.

  Meanwhile, Mr Hamad yesterday called on Zanzibaris to air their views when the Constitutional Review Commission starts to collect views from various stakeholders.He said one of the thorny issues that should be raised by Zanzibaris was the need to alternate the Union presidency between the Mainland and Zanzibar. “One term the presidency should go to the Mainland and the other term should be Zanzibar’s turn,” said the First Vice-President.

  However, he said there should be a modality of picking the Union president in Zanzibar because Zanzibar’s Union presidential candidates could not win through the ballot box as Zanzibaris were a minority.

  Mr Hamad catalogued the achievements the GNU had registered during its first year of existence, including the creation of a peaceful and tranquil country.However, he said there were still some challenges facing the GNU, including cross cutting issues such as drug abuse and trafficking, the environment and HIV/Aids.
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Wanajamvi:

  Kwa mtazamo wangu naona Maalim seif ni mnafiki tu kuhusu asemayo kwamba huwa hajibizani katika vyombo vya habari kwani kumjibu Hamad Rashid kwa waandishi wa habari atuambie ilikuwa nini?

  Maalim Seif anatufanya mafala kabisa – kaita mkutano wa waandishi na hatujui iwapo aliwaita akiwa kama nani – Katibu Mkuu wa CUF au Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar?

  Maana siku hizi amepata mwanya wa kuwa popo – yuko huku au kule, hata katika ziara zake – haziwekwi wazi. Kwa mfano wiki iliyopita alipokwenda Kilwa alikwenda kama nani?

  Na kama jana aliongea kama Makamo wa Rais wa serikali ya Umoja Zanzibar kueleza mafanikio ya umoja huo basi Seif angekataa kata kata kuwajibu waandishi kuzungumzia yanayojiri katika chama hicho.

  Maalim Seif hapo katumia ujanja tu -- eti kaita waandishi wa habari kuzungumzia mafanikio ya serikali ya Umoja, kumbe hasa alipanga kumjibu Hamad Rashid kiaina, maana alipanga waandishi kumuuliza kuhusu hilo.

  Hata kuzungumzia mafanikio ya serikali ya umoja yalikuwa ilikuwa geresha kwani hilo nijambo tayari Dr Shein alilizungumzia mwezi uliopita).


   
Loading...