Manyerere Jackton
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 2,438
- 4,461
JF ni Jukwaa la maarifa,
Kwa muda sasa naona kuna kosa tunalifanya, ama kwa kujua, au kwa kutojua. Naomba niwashirikishe jambo.
Mwaka 2000, Spika wa Bunge wa wakati huo, Mzee Pius Msekwa, alitukosoa kwa kosa la kuandika "Mbunge Mteule". Hoja yake ilikuwa kwamba hakuna mbunge mteule. Akasema mbunge akishatangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi, basi moja kwa moja huyo ni Mbunge tayari, na si Mbunge Mteule. Hivyo hivyo kwa Diwani.
Mzee Msekwa, katika kuipa nguvu hoja hiyo, akasema ndiyo maana Wabunge wanapokutana katika Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge, kazi yao kwanza ni kumchagua Spika wa Bunge. Kama si wabunge, hawawezi kumchagua Spika. Wanamchagua Spika kwa sababu tayari ni wabunge, na kwamba kiapo wanachoapa ni kwa ajili ya kutekeleza dhima zao.
Mambo ni tofauti kwa Rais. Mshindi wa kiti cha urais, kabla hajaapishwa, huyo ni Rais Mteule.
Nimeona nilete hili jambo nikiamini kuwa humu wamo wanafunzi ambao haya mambo wanapaswa wayatambue.
Nawasilisha.