Hakuna mbadiliko katika sheria msingi ya ndoa

Hakuna mbadiliko katika sheria msingi ya ndoa

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
(Vatican Radio) Baba Mtakatifu Francisko wiki hii alitoa nyaraka mbili za "Motu proprio"zinazolenga kufanya mabadiliko katika Mfumo wa Mahakama ya Kanisa Katoliki juu ya uendeshaji wa kesi zinazohusiana na sheria ya ndoa.

Papa alitoa nyaraka hizo siku ya Jumanne, Motu proprio, "Mitis Iudex Dominus Jesus"au Bwana Yesu, Hakimu mwenye huruma", ambayo inarekebisha kanuni za mahakama ya sheria ya kanisa (CIC) kwa Makanisa ya Amerika, na barua nyingine, "mitis et misericors Jesus"Msamaha na huruma ya Yesu", ambayo inafanya inarekebisha Kanuni za Makanisa za Kanisa katika uendeshaji wa kesi za kubatilisha ndoa kwa Makanisa ya Mashariki (CCEO).

Profesa katika Sheria za Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa ya Gregorian Rome, Padre James Conn, SJ, akizungumzia marekebisho hayo ameiambia Redio Vatican kwamba, kuna mabadiliko maalum matatu , hasa katika uharakisha wa kushughulikia kesi za wanaondoa wanaotaka kubatilisha ndoa; kuondolewa kwa haja ya mahakama kutoa hukumu mara mbili kwa tukio na kisha tena kupelekwa katika mahakama ya rufaa, kwa maana kwamba, inatosha kuzingatia maamuzi yaliyotolewa na mahakama kwa mara ya kwanza, iwapo yanayoona kwamba , kuna ushahidi wa kutosha kwa ndoa kutanguliwa, na wahusika wanaweza kufunga ndoa ndoa mpya kwa mujibu wa sheria Kanisa (au katika kupokea miungano ya ndoa ilifungwa kwa sheria za kiraia , wakati huo huo kutambuliwa na Kanisa).

Pia kuanzishwa kwa uwezekano wa kesi kusikilizwa na hakimu mwenye uzoefu mara moja, kama hatua ya kupunguza mzigo wa wingi wa kesi katika mahakama za majimbo, ambako watu wenye ujuzi ni wachache); Na uundaji wa kueleka mchakato wa kesi katika baadhi ya kesi , kutolewa maamuzi moja kwa moja na Askofu mahalia, kwa kesi ambazo zina ushahidi wa kutosha kutolewa hukumu ya kubatishwa na pande zote mbili zinaamini muungano wao ulikuwa batili. Katika mchakato huu hasa unaonyesha dhamira Papa Francisco kugawana madaraka na Maaskofu wa majimbo duniani kote.

Prof Conn, SJ, aliendelea kufafanua kwamba - kinyume na uvumi uliotolewa na baadhi ya vyombo vya hata katika vyombo vya Kanisa, mabadiliko yamefanyika katika misingi ya uelewa wa Kanisa la asili na muundo wa kimsingi wa ndoa, na hivyo hakuna mabadiliko kaika Madhumuni msingi na katika wigo wa mfumo wa Mahakama wa Kanisa. Na wala hakuna mabadiliko katika mafundisho ya Kanisa juu ya kutengua ndoa, alisema Prof. Conn, SJ. Na kwamba, nyaraka mpya za mabadiliko hazibadilishi kanuni zinazofuatwa na Mahakimu katika kubatilisha ndoa na wala hazibadili uhalali wa ndoa, hivyo, ndoa kubatilishwa linabaki ni jambo linalohitaji uwepo wa ushahidi wa kutosha .

Chanzo:
Radio Vatican
 
Back
Top Bottom