Amemteua Joyce Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu. Usiyempenda kaja ...
nguvu ya soda, mwalimu magu. ameshaanza kuchoka kabla ya miezi 3. badala ya kupeleka miswada bungeni ili kuzipa taasisi za utawala nguvu ya kiutendaji yeye anafukuzafukuza tu utadhani hao anaowateua ni malaika.
Nimekudharau kwa kusema Magufuli alimshinda Lowassa kwa kura milioni ishirini, ungekuwa umeendika tu kwa tarakimu ningejua umekosea kwa bahati mbaya, lakini ulichosema kwa maneno ndio hichohicho ulichoandika kwa namba! Idadi ya waliopiga kura nchi nzima wenyewe hawakufika milioni 20. Hata kama ni kulazimisha kile anachokifanya Magufuli ni lazima upotoshe na huo utetezi wako finyu.
Kila mtu anapenda sheria zifuatwe lakini inakuwaje sheria zinaangalia, nilitarajia wakwepa kodi waliogundulika wangechukuliwa adhabu kali, lakini inaonekana wameambiwa warudishe basi yakaishia hapohapo. Kwanza mchezo ulikuwa huuhuu tukambiwa kodi iliyokwepwa ni ya 80b lakini siku zilivyokwenda ikashuka mpaka 12.5b! Ni lazima mpate sifa kwa kutumia uongo?
Atakuwa ametubu dhambi zake, maana ngazi aliachia mwenyewe. Ni heri iwe ametubu kiukweli lakini kama ametubu kiuongo-uongo ataumbuka tu kama alivyoumbuka Lowassa.
Hii inawafaa zaidi akina Salum Mwalim na kundi lake linalodai Dr Magufuli anatekeleza sera zao. Siwashangai hata hivyo kwa sababu hawakuwahi kumsikiliza Dk Magufuli kwenye kampeni zake
Million 50 kwa kila kijiji au kata mbona hatuzioni?
nguvu ya soda, mwalimu magu. ameshaanza kuchoka kabla ya miezi 3. badala ya kupeleka miswada bungeni ili kuzipa taasisi za utawala nguvu ya kiutendaji yeye anafukuzafukuza tu utadhani hao anaowateua ni malaika.
Tanzania ya viwanda ipo wapi mahakama ya mafisadi ipo wapi anyway ni mwanzo ila tunavitaka
Amemteua Joyce Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu. Usiyempenda kaja ...
Acha kusambaza kasumba za udini. Kuwa na jina la Kikristu ni kosa?
Ile ya kufanya usafi na kulundika takataka katikati ya makazi ya watu hadi leo
Wamesamehewa wabeba sumu itakuwa wahujumu uchumi. Samehe hata saba mara sabini kama una uwezo huo. Fikiri.