Mungu nifundishe kunyamaza
Uhispania wanarejea kazini, vilevile Italy na marekani baada ya muda.Marekani imewashinda wanawaza kuachia watu wafanye kazi.
Sasa Tz mtakuwa mnaokota watu barabarani waliokufa kwa njaa na vipigo vya polisi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hawawez omba ushauri isipokuwa kulazimisha Nguvu ya umma isikike.Niliwahi mwambia mdogo wangu wakike miaka ya nyuma, gauni halijakupendeza, akanuna na kutoka hivyo hivyo, kufika alikokuwa anaenda mashoga zake wakamuuliza vipi shosti hukutokea home nini? akawauliza kwann? wakamjibu mbona upo normal sana hujadamshi. Akaelewa kuwa ni kweli hakuwa amependeza, aliporudi akaniambia. Nikanyamaza.
Siku nyingine akanifuata na mchoro wa gauni anataka akashone, nikamwambia huu umekaa kibibi sasa, ngoja nikutafutie mshono online, hakungoja, huyooo kwa fundi, baada ya wiki akarudi na gauni lake, kulivaa, mama akamwambia loooooooo yaani kitenge kizuri umeenda kukiharibu mwanangu, ndo umeshona kituko gani hicho. Akaniangalia, nikafumba macho.
Kuanzia siku hiyo, akawa akija na jambo lake, mi naunga mkono hoja tu, mpaka akajua kuwa bro hana time tena na mimi, akaamua kujishusha na kuacha ujuaji, ikawa akiomba ushauri kama yupo sahihi namwambia, kama kabugi namwambia na anachukua ushauri.
So tuendelee kujikinga wenyewe mpaka hapo watakapoona kuwa sisi nasi watu sio mifugo.
Haa!!Kufika July mosi kila nyumba itakuwa na at least mgonjwa mmoja
Wana jamvi
Nilitamani niandike haya maoni yangu mapema wiki hii ya kwanza ya paska lakini nashukuru Leo nimeandika.
Maambukizi yanaendelea kupaa kwa kasi tofauti na mtazamo WA awali licha ya waziri Ummy kueleza maambukizi ya ndani yameanza lkn hakutuonyesha mipango madhubuti.
Pia waziri Mkuu alipoongea ikulu ya DDM bado hakuonyesha mbinu wezeshi na nyongeza ktk kukabiliana na hali hii.
Lockdown kwa dunia yote ilionekana na njia madhubuti ya kukabiliana na maambukizi ya ndani lkn hapa kwetu si madhubuti.
Wengi tulifikiri na kuomba lockdown kama sehemu ya kujisalimisha kuwa hatutaki kuugua. Pia zuio LA kutotoka ndani nalo tuliona linafaa lkn serikali na bunge haionyeshi kujali mawazo ya umma.
Lockdown na curfew ni njia madhubuti hasa kwenye nchi zenye mifumo mibovu ya kiafya.
Kama hatuitaji kufunga mipaka ya miji na majiji vilevile zuio LA kutotoka nje kwa kigezo cha umaskini WA Tanzania, biashara na mazoea ya umma basi serikali tuonyesheni mipango.
Tunataka kuona mipango madhubuti ya nyongeza ktk kukabiliana na maradhi ya corona ya 2019 tofauti na hizi zinazoendelea; tunaomba haya kwa kuwa hamtaki kutufungia ndani na mipaka kwani hamtaki inawezekana kugawa chakula, kutoa posho, kutikisa biashara na uchumi ili kuhifadhi mwenendo WA mapato ya umma.
Hapo awali tuliwahi kumsikia wazir Mpango akiwaelekeza BOT kufanya tathimini ya uchumi na corona lkn hatujapata majibu.
Bunge linaendelea lkn hatujasikia msimamo WA bunge au wabunge wakitaka mipango ya kukabiliana na corona katika afya na uchumi WA watu na Taifa. Bajeti zinaendelea lkn si bunge Walioitaka wizara au wazir kurevise budget yao kutokana na mtikiso WA uchumi uliopo duniani kwani fedha za misaada na ruzuku zinaweza kupungua au kutowepo hivyo ofisi za umma zingeanza kupunguza matumizi na kuelekeza fedha hizo kwenye kuimarisha uchumi na miradi ya maendeleo au binge linakwenda kupitisha bajeti ambayo mwakani tunalaumiana kwa utekelezaji wake? Si muda wa viongozi wetu kuwa realistic?
Tunatamani tuone mipango ya kuimarisha kwelikweli kipato na uchumi WA sekta binafsi kwani tunaamini wameathirika. Marekani wameshapitisha bajeti hiyo na sisi hatuoni haja hiyo kwani tunabenki kuu, mfuko WA hazina na sheria ya fedha za dharura na katiba inaruhusu.
Wanajf wengi walishatoa na wanaendelea kutoa mapendekezo yao ni vema mkuu wa nchi na wa kila muhimili kuonyesha mahitaji ya kuinusuru nchi yetu kwani tunajua roho zetu si muhimu kuliko uchumi wetu na siasa yetu.
Naomba niishie hapo
Karibuni, tuendelee