Hakuna kurejewa uchaguzi Zanzibar!

Hakuna kurejewa uchaguzi Zanzibar!

Baraghash

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2012
Posts
2,713
Reaction score
1,790
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tumepokea taarifa kwamba Balozi Seif Ali Iddi amehojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Radio France International (RFI) na kusema kwamba eti viongozi wa CCM na CUF WAMEKUBALIANA UCHAGUZI ZANZIBAR URUDIWE, na kinachojadiliwa hivi sasa ni NANI ASIMAMIE UCHAGUZI WA MAREJEO kwa sababu ZEC ya JECHA INAONEKANA KUTOAMINIKA.

Tunapenda kuwawekea wazi Wazanzibari wote kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote, ni za uzushi na wazipuuze.
Msimamo wa CUF na Maalim Seif Sharif Hamad uko pale pale kwamba HAKUNA KURUDIWA UCHAGUZI na kwamba MSHINDI HALALI WA UCHAGUZI WA TAREHE 25 OKTOBA, 2015 ATANGAZWE NA KUAPISHWA.

Kauli za Balozi Seif Ali Iddi ni za kutapatapa zianzolenga kuwatuliza wana-CCM ambao wanaonekana kukata tamaa baada ya kushindwa vibaya na CUF kwenye uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Wabunge na Madiwani uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.
Kwenye uchaguzi mkuu wa Urais wa Zanzibar, mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alimbwaga vibaya mgombea wa CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, kwa zaidi ya kura 25,000.

Balozi Seif Ali Iddi mwenyewe akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya CCM anatuhumiwa na wana-CCM kushindwa kazi na kukisababishia chama chao kushindwa vibaya kuliko wakati wowote katika historia ya chaguzi za Zanzibar.
Lakini kama hilo halitoshi, wana-CCM wanamtuhumu Balozi Seif na wajumbe wengine wa Kamati ya Kampeni aliyokuwa akiiongoza kusimamia matumizi mabaya ya kiasi kikubwa cha fedha za kampeni za Chama hicho ambazo sehemu kubwa walimdanganya mgombea wao, Dk. Ali Mohamed Shein, kwamba zimetumika kuleta ushindi wa CCM kisiwani Pemba lakini kumbe ziliishia katika mifuko ya watu binafsi.

Haistaajabishi kwamba sasa Balozi Seif Ali Iddi ameamua kuja na njia ya kutoa taarifa za udanganyifu ili kujinusuru na mzigo wa tuhuma za kushindwa kazi na kusimamia matumizi mabaya ya fedha za kampeni kutoka kwa CCM wenzake.
CUF tunamtaka Balozi Seif Ali Iddi awache kudanganya umma na badala yake awajibu CCM wenzake kwa nini amekitia chama hicho aibu na fedheha kubwa ya kupata kipigo kibaya katika uchaguzi kilichopelekea CCM kupoteza majimbo tisa (9) kisiwani Unguja na Dk. Ali Mohamed Shein kushindwa uchaguzi wa Urais wa Zanzibar kwa zaidi ya kura 25,000 huku wakidai kutumia mamilioni ya fedha ambazo hawana maelezo zimetumika vipi.

CUF tunawataka Wazanzibari kutobabaishwa na kauli za kushindwa kazi za Balozi Seif Ali Iddi na watulie wakijua kuwa ufumbuzi wa haki wa uchaguzi mkuu utapatikana kwa kutangaza matokeo ya kura kwa majimbo yaliyobakia na hatimaye mshindi kutangazwa na kuapishwa.
HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
MKURUGENZI WA MAWASILIANO ? CUF
26 NOVEMBA, 2015

kwa hisani ya Mzalendo.net
 
Naufananisha uongo huu NA yule jamaa WA Iraq / aliokuwa akiiongopea dunia , Iraq itakuwa kaburi la waamerika sijui Nani yule?
 
Maalim Seif anaelewa yaliyojiri na baada ya kuchapwa za USO amekiri kuhalifu sheria na ili kulinda ustaarabu anakubali uchagizi urudiwe.
 
taarifa kwa vyombo vya habari

tumepokea taarifa kwamba balozi seif ali iddi amehojiwa na idhaa ya kiswahili ya radio france international (rfi) na kusema kwamba eti viongozi wa ccm na cuf wamekubaliana uchaguzi zanzibar urudiwe, na kinachojadiliwa hivi sasa ni nani asimamie uchaguzi wa marejeo kwa sababu zec ya jecha inaonekana kutoaminika.

Tunapenda kuwawekea wazi wazanzibari wote kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote, ni za uzushi na wazipuuze.
Msimamo wa cuf na maalim seif sharif hamad uko pale pale kwamba hakuna kurudiwa uchaguzi na kwamba mshindi halali wa uchaguzi wa tarehe 25 oktoba, 2015 atangazwe na kuapishwa.

Kauli za balozi seif ali iddi ni za kutapatapa zianzolenga kuwatuliza wana-ccm ambao wanaonekana kukata tamaa baada ya kushindwa vibaya na cuf kwenye uchaguzi mkuu wa rais wa zanzibar, wajumbe wa baraza la wawakilishi, wabunge na madiwani uliofanyika tarehe 25 oktoba, 2015.
Kwenye uchaguzi mkuu wa urais wa zanzibar, mgombea wa cuf, maalim seif sharif hamad, alimbwaga vibaya mgombea wa ccm, dk. Ali mohamed shein, kwa zaidi ya kura 25,000.

Balozi seif ali iddi mwenyewe akiwa mwenyekiti wa kamati ya kampeni ya ccm anatuhumiwa na wana-ccm kushindwa kazi na kukisababishia chama chao kushindwa vibaya kuliko wakati wowote katika historia ya chaguzi za zanzibar.
Lakini kama hilo halitoshi, wana-ccm wanamtuhumu balozi seif na wajumbe wengine wa kamati ya kampeni aliyokuwa akiiongoza kusimamia matumizi mabaya ya kiasi kikubwa cha fedha za kampeni za chama hicho ambazo sehemu kubwa walimdanganya mgombea wao, dk. Ali mohamed shein, kwamba zimetumika kuleta ushindi wa ccm kisiwani pemba lakini kumbe ziliishia katika mifuko ya watu binafsi.

Haistaajabishi kwamba sasa balozi seif ali iddi ameamua kuja na njia ya kutoa taarifa za udanganyifu ili kujinusuru na mzigo wa tuhuma za kushindwa kazi na kusimamia matumizi mabaya ya fedha za kampeni kutoka kwa ccm wenzake.
Cuf tunamtaka balozi seif ali iddi awache kudanganya umma na badala yake awajibu ccm wenzake kwa nini amekitia chama hicho aibu na fedheha kubwa ya kupata kipigo kibaya katika uchaguzi kilichopelekea ccm kupoteza majimbo tisa (9) kisiwani unguja na dk. Ali mohamed shein kushindwa uchaguzi wa urais wa zanzibar kwa zaidi ya kura 25,000 huku wakidai kutumia mamilioni ya fedha ambazo hawana maelezo zimetumika vipi.

Cuf tunawataka wazanzibari kutobabaishwa na kauli za kushindwa kazi za balozi seif ali iddi na watulie wakijua kuwa ufumbuzi wa haki wa uchaguzi mkuu utapatikana kwa kutangaza matokeo ya kura kwa majimbo yaliyobakia na hatimaye mshindi kutangazwa na kuapishwa.
Haki sawa kwa wote

ismail jussa
mkurugenzi wa mawasiliano ? Cuf
26 novemba, 2015

kwa hisani ya mzalendo.net

kaka maccm watafanya hujuma kurudia uchaguzi,subiri utaniambia
 
Maalim Seif akomae tu, hivi Balozi Seif Idd ndiye msemaji mkuu wa maridhiano yanayoendelea sasa?
 
Sasa hivi wameshikwa pabaya kwani pressure inatoka kwa jumuiya ya kimataifa pia.....Hawawezi kuforce lazima kuwe na makubaliano fulani...

kaka maccm watafanya hujuma kurudia uchaguzi,subiri utaniambia
 
Maalim Seif akomae tu, hivi Balozi Seif Idd ndiye msemaji mkuu wa maridhiano yanayoendelea sasa?

Maalim hana cha kukomaa. hivi sasa anatapia nafasi, na kama ustaarabu utawekwa kando ni MTU wakuburuzwa
mahkamani. yaani we we unafikiri hivi vikao ni vya nini? kumbuka tuna SUK Maalim ni janga!!!????
 
Naufananisha uongo huu NA yule jamaa WA Iraq / aliokuwa akiiongopea dunia , Iraq itakuwa kaburi la waamerika sijui Nani yule?
Umenikumbusha yule comedian anaitwa Al-Sahaf. Jamaa alikuwa noma hadi siku ya mwisho anasema... American are no where in Iraq..... kabla hajaendelea kombora la Amerika likapiga jengo alilokuwa anafanyia mkutano na camera zikaonyesha kupitia dirishani vifaru vingi vikubwa vikija kwa kasi. Akasepa na wamarekani walipomkamata wakamshukuru sana kwa kumdanganya Saddam na wakamwachia huru. Alienda kuwa mtangazaji al-jazeera sijui kwa sasa yuko wapi.
 
Naufananisha uongo huu NA yule jamaa WA Iraq / aliokuwa akiiongopea dunia , Iraq itakuwa kaburi la waamerika sijui Nani yule?

ALIITWA MHESHIMIWA AL.SAHAF, MSEMAJI MKUU WA SERIKALI YA IRAQ ENZI ZA SAADAM HUSSEIN, DUH SITAMSAHAU YULE MTU KWA PROPAGANDA NA SIJUI KWA SASA KM BADO YUKO HAI Ktk NCHI YA IRAQ ILOTIWA KIBERITI
 
Umenikumbusha yule comedian anaitwa Al-Sahaf. Jamaa alikuwa noma hadi siku ya mwisho anasema... American are no where in Iraq..... kabla hajaendelea kombora la Amerika likapiga jengo alilokuwa anafanyia mkutano na camera zikaonyesha kupitia dirishani vifaru vingi vikubwa vikija kwa kasi. Akasepa na wamarekani walipomkamata wakamshukuru sana kwa kumdanganya Saddam na wakamwachia huru. Alienda kuwa mtangazaji al-jazeera sijui kwa sasa yuko wapi.

Al Sahaf was really a comedian/msanii na ndiyo maana aliajiriwa na Al-jazeera moja kwa moja!

Zanziba hatuna vita kama vya George Bush na Saadam Hussein. Kilichotokea Zanzibar ni ubakaji wa Demokrasia kupitia Sanduku la Kura kwa Mahifidhina wa CCM kutokubali matokeo baada ya kuona wameshindwa.

Tunataka kumwambia Balozi Seif Ali Idd aache usanii wa kuidanganya dunia kama alokuwa akifanya Al-Sahaf wa Iraq.Marekani wameshatoa tamko tayari la kutaka kumalizwa kwa mgogoro Z'bar kwa maana ya kumalizia kutangaza matokeo yaliyokuwa yamebakia kabla ya kufutwa ili kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar 2015 kwa kumtangaza Maalim Seif ambaye ndiyo mshindi.

Uchaguzi ule ulikuwa HURU na HAKI na ulishuhudiwa na watu wote wakiwemo Waangalizi wa Kimataifa wakiwemo Wamerekani ambao ndiyo Wafadhili wakubwa wa nchi yetu. Nje ya hapo Tanzania ijiandae kukosa Tshs. Trilioni 1 za MCC(Millenium Challenge Cooperation).

Tunajua Rais Magufuli kwa sasa anahangaika kukaba mpaka penalti ili apate fueza ya kutimiza ahadi zake kwa Watanzania. Kwanza tutamshanga na kumpunguzia maksi kama kweli yuko tayari kuona hiyo fedha ikizuiliwa na Marekani kwa sababu za mtu mmoja mjinga anayeitwa Jecha Jecha wa CCM.
 
Ya Zenj tuwaachie Zenj, Amin

Zenj ni sehemu ya JMT hivo kusema eti ya Zenj tuwaachie Zenj ni upuuzi na ujinga.
Wakti munahesabu kura za Rais wa JMT mbona za Zenj hamkusema tuwaachie Zenj????
Mijitu mingine bwana.................ni shida!
 
Umenikumbusha yule comedian anaitwa Al-Sahaf. Jamaa alikuwa noma hadi siku ya mwisho anasema... American are no where in Iraq..... kabla hajaendelea kombora la Amerika likapiga jengo alilokuwa anafanyia mkutano na camera zikaonyesha kupitia dirishani vifaru vingi vikubwa vikija kwa kasi. Akasepa na wamarekani walipomkamata wakamshukuru sana kwa kumdanganya Saddam na wakamwachia huru. Alienda kuwa mtangazaji al-jazeera sijui kwa sasa yuko wapi.

Al Sahaf was really a comedian/msanii na ndiyo maana aliajiriwa na Al-jazeera moja kwa moja!

Zanziba hatuna vita kama vya George Bush na Saadam Hussein. Kilichotokea Zanzibar ni ubakaji wa Demokrasia kupitia Sanduku la Kura kwa Mahifidhina wa CCM kutokubali matokeo baada ya kuona wameshindwa.

Tunataka kumwambia Balozi Seif Ali Idd aache usanii wa kuidanganya dunia kama alivokuwa akifanya wa Al-Sahaf wa Iraq.Marekani wameshatoa tamko tayari la kumaliza mgogoro huo kwa maana ya kumaliza kutangaza matokeo yaliyofutwa ili kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar 2015 kwa kumtangaza Maalim Seif ambaye ndiyo mshindi.

Uchaguzi ule ulikuwa HURU na HAKI na ulishuhudiwa na watu wote wakiwemo Waangalizi wa Kimataifa wakiwemo Wamerekani ambao ndiyo Wafahdhili wakubwa wa nchi yetu. Nje ya hapo Tanzania ijiandae kukosa Tshs. Trilioni 1 za MCC(Millenium Challenge Cooperation).

Tunajua Rais Magufuli kwa sasa anahangaika kukaba mpaka penalti ili apate fueza ya kutimiza ahadi zake kwa Watanzania. Kwanza tutamshanga na kumpunguzia maksi kama kweli yuko tayari kuona hiyo fedha ikizuiliwa na Marekani kwa sababu za mtu mmoja mjinga anayeitwa Jecha Jecha wa CCM.
 
Kumbaro hana issue ..ni muendelezo wa drip tu
 
Fedha haitozuiliwa kwa sababu ya Jecha Bali ukweli itazuiliwa kwa sababu ya Maalim naye ni janga, nakeambia sehemu inayomfaa jinamizi huyo ni S EGEREA.
 
Back
Top Bottom