Hakuna "kukosea kuoa"

StudentTeacher

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2019
Posts
7,063
Reaction score
8,499
Unaweza ukaoa 'Malaika' halafu akaamua yeye kama yeye kugeuka na kuwa 'Shetani'. Hapo utajilaumu kwa lipi sasa kama sio kujinyanyapaa bure?.

Ni kama vile Mungu alimuumba "Lucifer" akiwa safi kabisa lakini Lucifer akaamua kuitumia "haki yake ya kikatiba" ya uhuru wa kuamua alitakalo na kujigeuza kuwa Shetani rasmi.

Kama umeamua kumpenda mtu we mpende sana, mtendee mema sana kadiri uwezavyo tena bila kuweka matarajio yoyote kutoka kwake.

Tutendeane mema tungali bado tupo hai maana tukifa nafasi hiyo hufa pia. Tenda mema, tembea kifua mbele
 
Hakuna uhusiano usio na faida, unampenda mtu huku ukitarajia na yeye kukupenda pia...

Kwa jinsi unavyoshauri, kama ndoa ni one way traffic, je ni nani mwenye jukumu la kupenda?
 
Mwenye uwezo wa kumudu hilo sina hakika kama yupo hapa duniani
 
Hakuna uhusiano usio na faida, unampenda mtu huku ukitarajia na yeye kukupenda pia...

Kwa jinsi unavyoshauri, kama ndoa ni one way traffic, je ni nani mwenye jukumu la kupenda?
Ulishawahi kumpa mtu kitu pasipo kutarajia kitu kutoka kwake?. Ulijisikiaje?
 
Mwaka huu mambo yamekua mengi mapema huku kukosea kuoa huku hakuna kukosea kuoa huku msioe huku muoe uchaguzi ni wako,,ushindwe wewe tu yan[emoji2957]
Watu bilioni 7 na ushee sio kidogo. Lazima mambo yawe mengi tu. Hamna namna.
 
Hakuna uhusiano usio na faida, unampenda mtu huku ukitarajia na yeye kukupenda pia...

Kwa jinsi unavyoshauri, kama ndoa ni one way traffic, je ni nani mwenye jukumu la kupenda?
Je, ukitarajia kisha kikaja ambacho hujakitarajia itakuaje?. Jifunze kujitendea haki. Nafsi ikikutuma kumtendea mtu wema we mtendee kisha tembea kifua mbele
 
Hakuna uhusiano usio na faida, unampenda mtu huku ukitarajia na yeye kukupenda pia...

Kwa jinsi unavyoshauri, kama ndoa ni one way traffic, je ni nani mwenye jukumu la kupenda?
Unamaanisha uhusiano ni Uwekezaji?
 
Kubadirika kwa mwanadamu kupo tu siku zote, ila kuna mabadiriko mengine hata unaweza kusema shetani na ushetani weke ni mbaya ila anaowatumikisha kuwatendea wanadamu wenzao nizaidi ya ushetani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…