Hakuna kuingia Dodoma bila kitambulisho

Hakuna kuingia Dodoma bila kitambulisho

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 17(1)

17.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya
kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika
sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya
kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.

________________________________________________________
Tamko la Mkuu wa mkoa wa Dodoma kwa Watanzania wote wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni hivi:-

"Itakua ni marufuku kwa Mtanzania asie na Kitambulisho cha Utaifa, kinacho onyesha uraia wake na mahali anapotokea, kuingia mkoani Dodoma mara baada ya zoezi hilo la utoaji vitambulishi kukamilika nchi nzima" Dk Binilith Mahenge
________________________________________________________
Hapa ndipo CCM MPYA INATUPELEKA, Ikumbukwe pia Nchini North Korea kwa Dogo Kim, ni marufuku kwa Mwananchi kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine bila kua na passport maalumu na barua ya viongozi ya kuidhinisha safari hiyo.

MKUU WAMKOA WA DODOMA.jpg
 
Apo itafanya wana dodoma wote wakajiandikishe kupata kitambulisho,ata kama agizo lake anajua haitakua hivyo lakini approach anayotumia itasaidia kW kiasi kikubwa ata wale raia wenye kupuuzia kitambulisho vya taifa
 
hapa ndipo unapokuja kuona ule usemi wa ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni!!.
kuna baadhi yamikoa wananchi bado hawajapata vitambulisho,akiitwa kikazi dodoma hivyo hawezi kwenda ama..? wakumbuke kuna wafanya biashara n.k
hata hivyo zoezi la kitambulisho pia huchukua muda kwanini wasifanye utaratibu mambo yakaenda sawa.
 
Hilo tangazo ni batili lipuuze. Aliyelitoa hana mamlaka kikatiba wala kisheria kufanya hivyo!
Kwa sasa, endelea kufurahia haki yako ya msingi iliyoainishwa kwenye katiba na sheria za Tanzania ijulikanayo kama;
FREEDOM OF MOVEMENT
 
Halooooooo hiyo Dodoma ina nn cha special mpk paendewe na kibali?????????

Sent using Jamii Forums mobile app

Mama kwani haujui huo ndio mji mkuu umetawadhwa karibuni kuwa jiji. Vilevile ndio makao makuu ya chama kubwa.

Hauoni pembeni kwenye picha yupo mzee wa "utapata tabu sana...kipigigo cha mbwa mwizi"?
 
Hiyo 17(1) si Maneno, ni lazima kutambulika kuwa wewe ni Mjamhuri kisheria!! Sioni kosa kwenye hilo tamko. Pia na wewe kuanzia point hiyo anza kuelewa misingi ya facts beyond words.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 17(1)

17.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya
kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika
sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya
kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.

________________________________________________________
Tamko la Mkuu wa mkoa wa Dodoma kwa Watanzania wote wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni hivi:-

"Itakua ni marufuku kwa Mtanzania asie na Kitambulisho cha Utaifa, kinacho onyesha uraia wake na mahali anapotokea, kuingia mkoani Dodoma mara baada ya zoezi hilo la utoaji vitambulishi kukamilika nchi nzima" Dk Binilith Mahenge
________________________________________________________
Hapa ndipo CCM MPYA INATUPELEKA, Ikumbukwe pia Nchini North Korea kwa Dogo Kim, ni marufuku kwa Mwananchi kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine bila kua na passport maalumu na barua ya viongozi ya kuidhinisha safari hiyo.

View attachment 844302
me nafikili angepiga marufuku kuingia Dodoma kama huna kadi yakijani
 
Yupo sahihi, pale ni makao makuu ya nchi lazima kuwe na mbinu mbalimbali za kiusalama.
Kuna watu watakuwa miaka 17 siku zoezi la kutoa vitambulisho litakapo kamilika nchi nzima.
Sasa baada ya miezi michache anafikisha miaka 18 na anaenda Dodoma kwa ndugu yake au kikazi au kibiashara huku akisubiri ID yake.
Je huyo utamzuia au utamuweka korokoroni?

Mambo mengine wapunguze kuropoka matamko bila kupima uhalisia.
 
Jiwe anafanya watu wawehuke....

Kila mteuliwa anakuna kichwa afanye nini cha kumfurahisha "mteuzi" walau watoto wake wasogeesogee japo kidogo.
 
Tanzania mpya hiyo mazoea yatatukondesha maana ukijifanya unataka sana sheria utapata taabu sana
 
Back
Top Bottom