Hakuna kitu kigumu duniani kama kukubaliana na ukweli

Hakuna kitu kigumu duniani kama kukubaliana na ukweli

Ni kweli kabisa, kukubali ukweli mara nyingi ndiyo kazi ngumu zaidi maishani. Huwa inaumiza kwa sababu ukweli unakulazimu uache yale matamanio au picha uliyojitengenezea kichwani.

Hata hivyo, unavyozidi kuukimbia ukweli, ndivyo unavyochelewesha nafasi ya kupona na kusonga mbele. Ni hatua yenye maumivu makali, lakini ndiyo njia pekee ya kukupa uhuru wa kweli.
Unakataa ukweli ilihali ndo uhuru wako.
 
1: Tumuombe Mungu atupe mwisho mwema.

2: Kuna siku itaanza bila wewe kuwepo.Tujiandae na hii siku kwani haikwepeki.
Sahihi sote tunapita ndio maana tunahimizwa kuishi kwa upendo maana sote njia yetu ni moja tajiri na masikini sote tutazikwa chini
 
Ndio nani huyo huku jf kutoka tu Kuna mtu amekuwa malkia?
Ni mshangazi furani hivi mjuaji humu jukwaani alitamba sana wakati wadau wengine wamekula kifungo kwa muda mref
Dogo nimegeuka signature yako? naona unanipa credits kila kona na mimi sio main author!
Utaelewa tu wewe si unajua kunichafua me nakulipa mema kwa kukupamba
 
Maisha ni safari yenye mafanikio, majaribu, furaha na huzuni. Mara nyingi tunawaona watu wakitabasamu mbele yetu na kudhani kwamba kila kitu kinaenda sawa katika maisha yao, lakini ukweli ni kwamba kila mtu ana vita yake anayopambana nayo kimya kimya.

Usimhukumu mtu kwa mwonekano wake, mavazi yake, kazi yake au hali yake ya sasa. Wapo wanaocheka mchana huku wakilia usiku, wapo wanaosaidia wengine huku wao wenyewe wakihitaji msaada, na wapo wanaoonekana wenye nguvu huku mioyo yao ikiwa imejaa maumivu makubwa.

Maisha yanaweza kubadilika ndani ya muda mfupi sana. Leo unaweza kuwa juu, kesho ukawa chini. Leo unaweza kuwa na kila kitu, kesho ukajikuta ukianza upya. Hivyo basi, jifunze kuwa na huruma, upendo na heshima kwa kila mtu unayekutana naye.

Usiwe sababu ya kuongeza maumivu kwa mtu ambaye tayari anapitia kipindi kigumu. Badala yake, kuwa sababu ya tabasamu lake, tumaini lake na nguvu yake ya kuendelea mbele. Maneno mazuri hayagharimu chochote, lakini yanaweza kubadilisha maisha ya mtu kabisa.

Kumbuka, kila mtu ana hadithi yake ambayo huijui. Chagua kuwa mwanga badala ya giza, kuwa faraja badala ya maumivu, na kuwa baraka badala ya mzigo kwa wengine. Mwisho wa yote, utu wetu kwa watu ndiyo urithi mkubwa tunaouacha duniani.

Mwenyezi Mungu atujalie mioyo ya huruma, hekima ya kuelewa wengine, na nguvu ya kusimama pamoja katika nyakati zote za maisha. ❤️

Tafakari na Mjusia.
Ukweli mtupu!
 
Back
Top Bottom