Hahahahaha.
Mara ya kwanza kulima matikiti, nililima eka tatu. Yakawa mazuri, makubwa. Siku ya kukaribia mavuno yapo yaliyowahi kukomaa, nikachukuwa moja kwenda kujinafasi. Duh, nakata limetoka tikiti jeupe kabisa ndani, hakuna wekundu hata kidogo. Kulionja, hakuna utamu wala harufu ya tikiti hata chembe.
Ikabidi tuchukuwe lingine, hivyo hivyo. Nikachuma mawili matatu sehemu tofauti ya shamba, hivyo hivyo.
Nikachukua sample nikapeleka kwa bwana shamba Mkuranga wilayani. Akacheka, akanambia mama wamekuuzia mbegu siyo.
Nikawa hoi bin taabani.