Hakuna kauli inayoniudhi, inayoniuma na kunikera kutoka kwa Dada zetu kama hii....

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Yaani unakuta kabisa Mwanaume umeshajikoki na umekokika kisawasawa na kuzipangilia vizuri sana Manifesto zako za Kutukuka za Kutongoza halafu unamtokea Demu unamuimbisha kadri uwezavyo hadi mishipa yote ya Ubongo inasimama na kukakamaa halafu yule Demu anakujibu kwa kukuambia " nipe muda nifikirie nitakujibu Kaka ".

Hivi Mimi wakati nakuja kukutongoza nilijifikiria au niliamua tu kujilipua dhidi yako na nikaamua Kiujasiri kabisa kujitoa mhanga na kuja Kukutongoza? Unaponiambia Mimi Mwanaume eti nikupe muda ujifikirie ndipo unijibu hapa huwa mnamaanisha nini hasa Kwetu sisi Wanaume?

Hivi kama unajua humtaki GENTAMYCINE yanini sasa uniambie nikupe muda unifikirie ndipo unijibu? Hivi na Mwenyezi Mungu nae angakuwa pale wakati tunamuomba angekuwa anatujibu kuwa tumpe muda ili atufikirie kama atupe baraka zake au atutose leo Wote tungekuwa na amani au mafanikio haya hapa duniani?

Dada zetu / zangu mnanikera / mnatukera sana sisi Wanaume na niwaombe tu kupitia uzi huu kwamba kama unajua fika kuwa humtaki Mwanaume fulani aliyekutongoza basi kuliko kumwambia akupe muda ufikirie ili umjibu rahisisha tu kwa kumwambia Kaka sipo tayari au sikuhitaji tutawaelewa.

Mnatutesa mno hakyanani na sijui kwanini Mwenyezi Mungu nae aliweka kitu Mapenzi duniani.

Eti " nipe muda nifikirie nitakujibu Kaka ". Hii kauli inaniudhi na kunikera kuliko kitu chochote duniani na msipobadilika kuna siku mkitujibu hivi tutakuwa tunawasindikizeni tu na Vibao vya nguvu ili mjifunze zaidi kuwa makini. Jibu ni Yes au No na siyo hilo la Kipuuzi.

Mwanamume nimemaliza kutema cheche na nawasilisha.
 
Mdogo wangu nategemea uko Olevel if not advance Secondary school,
Kwa kukusaidia siku hizi wanaume hawajipangi kwa mistari ila tunjipanga kwa hela,
Mchukue mpeleke shambani kwako kwenye mifugo, ukirudi mpitishe site kwako unakojenga baada ya hapo nenda mall fanya shopping ya nyumbani kwako rudi nae unakoishi ingia jikoni ili ajionee ulivyo a gentleman not a boy, Hakika Siku hiyo hiyo unakula Mzigo bila hata kutongoza.. Hii inaitwa making a lady comfortable while anafikiria your a husband material...
 
Kuzungushwa kidogo kuna ongeza thamani kwa mwanamke kijana, yani unataka uombe na kupewa kwani maji hayo zungushwa kidogo adi ushikwe na hasira ili siku ukipewa umalizie hasira sasa umeomba na hapo hapo umepewa hata wewe muombaji si utahisi ikinilicho pewa akina thamani,kitu rahisi kinapatikana kwa urahis kitu chenye thamani kina patikana kwa thamani
 
Mdogo wangu nategemea uko Olevel if not advance Secondary school,
Kwa kukusaidia siku hizi wanaume hawajipangi kwa mistari ila tunjipanga kwa hela,
Mchukue mpeleke shambani kwako kwenye mifugo, ukirudi mpitishe site kwako unakojenga baada ya hapo nenda mall fanya shopping ya nyumbani kwako rudi nae unakoishi ingia jikoni ili ajionee ulivyo a gentleman not a boy, Hakika Siku hiyo hiyo unakula Mzigo bila hata kutongoza.. Hii inaitwa making a lady comfortable while anafikiria your a husband material...
You are very intelligent yaani
 
Alafu mnachokosea nyie ni kukosa subira!!!

Yaani mwanaume utakuta umemchunguza mdada kama mwezi au ata wiki umejiridhisha kua anakufaa, unaenda kumtongoza unataka ndani ya dakika moja akukubalie tu!?

Mpe mwanamke mda wa kumfahamu kidogo mtu anaemtongoza... Ni ubinafsi wa hali ya juu kutegemea akupe tu jibu hapo hapo...
 
Hivi kama unajua humtaki GENTAMYCINE yanini sasa uniambie nikupe muda unifikirie ndipo unijibu? Hivi na Mwenyezi Mungu nae angakuwa pale wakati tunamuomba angekuwa anatujibu kuwa tumpe muda ili atufikirie kama atupe baraka zake au atutose leo Wote tungekuwa na amani au mafanikio haya hapa duniani?

Unadhani Mungu hachukui muda wake kufikiria kama unastahili hicho unachokiomba? Watu wanaomba kupata watoto na wanasubiri miaka hadi 20 ndo wanajibiwa maombi...

Katika kuomba kitu, kuna majibu matatu...

1. Ndio

2. Hapana

3. Subiri
 
Ndio
Hapana
Subiri

Hayo ndio majibu, hata kwa Mungu yapo, kwahiyo tuliza ball dogo.
 
Back
Top Bottom