Hakuna jipya bungeni: Cdm tokeni humo mjengoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna jipya bungeni: Cdm tokeni humo mjengoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wagaba, Jun 19, 2012.

 1. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mwenendo mzima wa vikao Bungeni hakuna tija yoyote kwa CDM kuendelea kukaa humo mjengoni kwa kuwa ubaguzi na uonevu ndo order of the day (hata wiki moja haijatimia vizuri.)
  Ni bora wabunge wa CDM na wapinzani wengine wanayoitakia mema nchi hii, wapange ratiba maalum na yenye mikakati madhubuti ambayo itawezesha wabunge pinzani kuendelea kuhamasisha ukombozi wa hii nchi ktk majimbo yao.

  Kuendelea kukaa mjengoni ni kupoteza muda na kuwakosesha wapiga kura haki yao ya msingi ya kupata serikali inayowajali na kulinda masilahi yao.

  wajiandae kwa mabadiliko makubwa ktk nchi hii in the near future. Hata kama si urais hata majority MPs mjengoni! itasaidia sana, kuliko kuburuzwa namna hii.
  Wameshajipanga bajeti ipite tu kama ilivyo, come sun come rain!

  Chama tawala imeshajaza sumu ktk vichwa vya wabunge wake. Tusitegemee changes zozote ktk bajeti hiyo. Mfano mzuri ni pale mbunge wa sisiem anachangia hoja na kuiunga mkono mapema na baadae anatoa matatizo lukuki ktk jimbo lake (Komba na wenzake)! Unaunga mkono nn!? Bajeti kama ina mapungufu unasema ili wapiga kura wafaidike na mchango wako (or rather wafaidike na kura zao walizokupa)
  Tabia ya kushabikia chama sijui itakwisha lini?

  Uzalendo hakuna. Nyambaf moja anaropoka 'vua gwanda vaa uzalendo' huku chama chake kikimaanisha tofauti kabisa.
  Wapinzani msipoteze precious time yenu hapo mjengoni. Kuna mengi ya kufanya majimboni kwenu ambayo yana tija zaidi.

  'Bunge 2012 is just another silly season' - alishasema kamanda Lissu
   
 2. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wasitoke nje wabaki kuendelea kuwatetea wananchi kama tulivyo watuma mjengoni
   
 3. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa bora kutoka mtu anasema na hunga mkono hoja alaf anapinga katikati,huu ni utoto
   
 4. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  wanawatetea wananchi kwa lipi wakati hand brake zimeshavutwa hadi mwisho. Usitegemee cha ajabu hapo. walishateta mida kitambo!
   
Loading...