Mkuu Baba ni mfano wa Mungu. Anapooa tayari anajua Mke wake atakula nini, atavaa nini na mambo mengine. Atakapo hitaji watoto tayari ameshajiseti kuwa hao watoto wataishi vipi iwe kwa kula, kuvaa na mambo mengine. Mzazi kuzaa watoto wengi si kigezo cha yeye kuwategemea watoto wake uzeeni kiuchumi.
Hata Mungu kabla hajakuumba amekuwekea Fursa nyingi ili ukizaliwa unaamua ufanye ipi. Ukiamua kuwa mkulima utajua mwenyewe, ukiamua kuwa mwindaji, mfugaji, mhubiri, mfanyabiashara ni wewe tuu. Embu fikiria kama Mungu angetuumba bila kuwepo Ardhi unafikri maisha yangekuwaje? Bila kuwepo maji. Mungu ni Baba anayetutegemea katika kusimamia huu mradi wake hapa duniani. Hahitaji chochote zaidi ya usimamizi mzuri. Ndivyo hata sisi tunavyotakiwa kufanya kama Baba huku duniani. Tuandae miradi mingi kusudi watoto na wajukuu waamue nini wafanye kupitia miradi ya Baba yao('wewe/mimi).