Hakuna hata anayeniambia nimefanana na mtoto wangu

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,258
KWA WABABA

Nimeombwa ushauri na kukoleza.

Inawezekana hii ikakugusa wewe na huenda hujawahi kutafakari ama umechukulia poa na hasa kama dhahiri mtoto amefanana na mama.

Inatokea kuna baadhi ya features ambazo hata kwa mama huzioni mfano mtoto ana mwanya na mama hana mwanya na wewe kadhalika huna hata mwanya wala nduguyo yeyote.

Kila maisha yanavyozidi kwenda, unatembelewa na wageni lakini haijatokea hata siku moja unapomtambulisha mtoto wako UKAAMBIWA KAFANANA NA WEWE...


Tujadili tu...
 
Hayo mambo ya Mkemia yanahusika, mwanzo utafanana nae tu, hata ukucha au meno. Kuna baba mmoja alikua analalamika ameshawahi kumtazama na kumchunguza mwanae kuanzia utosi hadi unyayo anasema hakuna hata punje moja anafanana nae, hua hana raha kabisa na kijana wake.
 
Mtoto anamiaka mingapi? ask him to give time some time hizo mambo hubadirika. wakat anazaliwa binti yangu hakuwa amefanana na mimi chochote, alikuwa bibi yake mzaa mama kila kitu, kila kitu bro, yani mpaka aliibua gumzo kwetu nilikaza tu kwa makusudi na kuwa upande wa mke wangu lakin sikuwa na grounds. miaka baadae mtoto karud kwangu, sura, mwili(features) had tabia. mbaya zaid ni zile tabia zangu ambazo watu hawazijui (ninazozificha since nimekuwa) ye ni mtoto hawez zificha. nikimuangalia sina haja ya mtu kuniambia she looks like me, mwenyewe naona na hata Mamaangu alishaniita na kukiri walikua wrong akaomba radhi.
 
Hiyo ipo, c lazma mtoto afanane na wewe.
Hiyo kauli ni mbinu msikata watoto, au watoto wakakosa malezi ya baba, ila ukweli nikwamba mtoto lazima atafanana na baba yake kwa namna moja au nyingine, kama sio sura basi sikio au alama za viganja vya mikono nk
 
Back
Top Bottom