Nawakumbusha ndugu zangu wapinzani kwamba watanzania ambao mmetumia muda wenu mwingi kuwatetea hawaoneshi kutambua kazi na sacrifice mnazofanya. Kwamfano mnawatetea watumishi waboreshewe maslahi yao lakini wenyewe na vyama vyao hata hawapazi sauti pale ambapo nyie mnawaongelea wenyewe.
Pale mnapiga kelele kuhusu kuminywa kwa haki za binadamu kwa vitendo kabisa mkawaonesha pale polisi wanaua bila ushahidi, wanawaweka mahabusu watu nje ya masaa na taratibu za kisheria. mmewaonesha na wameona maiti kadhaa zikiokotwa au watu kupotea na kila jambo. mmewakumbusha juu ya umuhimu wa uhuru wa habari na democrasia ya kweli pamoja na katiba mya lakini hakuna anyestuka kuwaunga mkono mapambano haya.
mmewaambia watu juu ya uchumi na utawala bora. mmewapa takwimu za wapi tupo na tunaelekea wapi. mmewaonesha kasoro kwenye deni la taifa, kufungwa kwa shughuli nyingi za biashara. mmewaonesha kiza kinachotukaribia huko mbele tuendako na wapo ambao wameyaona kwa matendo lakini bado hawajasikia na kushirikiana nanyi katika kulitatua hili.
Nimewaza tu, kwakua kila mmoja anaisoma namba kwa verse na chorus zake binafsi. Kwanini tusiwaachie tu waendelee kuyaona mpaka siku wakipiga kelele tushiriki kuwaonya kwamba wamechelewa na hawakuchukua fursa mapema? Mnawahangaikiaaaaa lakini wabongo kila mmoja anafyata mkia anasubiri zitto uuliwe, au ufungwe na hawatakuja kukukumbuka kamwe. Tanzania sio tunisia ambapo tukio la kijana kujichoma moto liliibua hasira ya kutaka mabadiliko. mnawatumikia watu dhaifu na zezeta hata wakiambiwa watembee uchi wapo ambao watasema "kwanza kwa joto la TZ nguo za nini bwana, nilikuwa nakerwa na maguo" badala ya kuchalange udhalilishaji.....
Why tuendelee kuwatetea wasiojali na kuthamini harakati za utetezi? Nimeamua kuwashangaa tu hawa watanzania na wala siwachukii kwani maisha yangu ni bora sana. Siishi maisha yao ya mlo mmoja kwasiku, wala siishi maisha yao kwamba kupanda kwa gharama nabanwa, shughuli zangu zinanilipa na familia yangu itaendelea kuwa well-off zaidi ya hao wanaokesha kusifia hali ingawa wanateseka.... Binafsi nimesitisha harakati za ukombozi nawashangaa tu mnahama na kurudi na wengine mtahama. But siwezi kufia mtanzania tena. Unapatwa na ya mawazo na bensaanane hao uliowatetea kimyaa wanakula bata tu...
Kila la kheir wapambanaji, Nimeamua kufunika kombe, ................................
"In the End, we will remember not the words of our enemies, but the silence of our friends. " Martin Luther King, Jr.
Read more at: Martin Luther King, Jr. Quotes