Hakuna faida ya wabunge wa upinzani!

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,669
40,917
Nilitegemea labda baada ya kuwa na vyama vingi vya siasa hapa nchini, basi nitaona kizazi kipya cha hoja na mawazo ambayo kamwe chama tawala kisingeweza kuyawaza!

Ajabu yake nimekutana na upinzani ambao agenda yao ni malalamiko na tuhuma tu bila kuwa na !awazo mbadala!
Nimeshindwa kuona faida ya kua na mpinzani ambaye hana la kumfanya tofauti na yule niliyemzoea!

Kama mwananchi wa kawaida analalamika na mbunge wake wa upinzani analalamika kwa jambo hilo hilo kuna faida gani ya kua na mtu ambaye anauwezo kama wangu?

Wabunge wa upinanzani wameshindwa hata kujitofautisha na wale wa chama tawala kwa kuhakikisha kua majimbo yao hayana changamoto zozote ukijumuisha na dalili za ukame!

Majimbo yote ya uchaguzi Tanzania yanafanana kwani vilio ni vile vile!
Naanza kujiuliza nini faida ya vyama vya upinzani kama na wao wanafanya Yale Yale wanayoyakosoa!
 
Katika nchi ya Demokrasia vyama vya upinzani vinakuwaga na UMUHIMU mkubwa sana na kazi yake kuu ni kuiweka serikali iliyoko madarakani katika UWAJIBIKAJI wake KITAIFA.

Na mara kwa mara inahitaji KIONGOZI aliye MWELEVU , UFAHAMU na SIYO MWOGA kuzungumzia sualo lolote ambalo serikali iliyoko madarakani INAKOSEA.

Ki demkrasia UPINZANI haupelekwi MAHAKAMANI kushtakiwa kwa TAMKO lolote ambalo ni CHANYA hata kama serikali iliyoko madarakani HAITAKI kusikia.
Bila kuwa na kiongozi ama viongozi SHUPAVU basi upinzani ni sawa na Meli isiyokuwa na NAHODHA.
Maana kubwa ya Upinzani ni SERIKALI MBADALA INAYONGOJA/Government in waiting. Inahitaji UJANJA wa KISIASA na wala SI FUJO za KISIASA!
 
Mimi pia sioni faida ya kuwa na rais kutoka CCM, kila kitu analalamika,mara sukari imefichwa na wafanya biashara,mara hela zimefichwa ndani,mara wapiga dili wamenunua magazeti kutangaza uongo,BORA NCHI ISIWE NA RAIS KILA MTU AJIONGOZE ANAVYOJUA MAANA HAKUNA UTOFAUTI NA TUKIWA NA RAIS.
 
Sasa wewe kada wa CCM unataka wabunge wa upinzani wa nini? Jamani unafiki huu
 
But unaona furaha Kwa kuwa na mbunge anayehongwa million 10 apitishe mwasada hatari Wa kwenda kumkandamiza aliyemchagua ?
Majimbo ya wabunge wa upinzani na Yale ya ccm hawana tofauti yoyote! Sasa Luna haja gani ya kua na vyama vya upinzani kama hawana input yoyote ile!
 
Unachosema ni kweli 100%. Hawana faida kabisa.
Kwanza waoga, pili wanachukulia ubunge kama ajira badala ya commitment yao kwa wananchi.
Kama Serikali wanaamini haiwasikii, Wanaweza kuja na mawazo chanya kwa wananchi wakatumia rasilimali za eneo lao kujenga uchumi wa mwananchi mmojammoja. Na hii ndio zawadi kubwa ya mbunge kwa wananchi wake.

Mbunge wa Moshi anatamani awe wa bukoba kwa sababu tu kuna vitu vya kuongelea huko.
Hii dhambi wataulizwa siku ya mwisho
 
Hawa watu wa ajabu sana, yaani MTU yupo radhi kusafiri miles away ili akapate media coverage! Anasahau hata changamoto za waliomchagua! Useless MP's!
 
Sasa wewe kada wa CCM unataka wabunge wa upinzani wa nini? Jamani unafiki huu
Mkuu unaweza ukawa uanakipinga kitu lakini kwa wakati huo huo unaona faida yake kwa namna flani!

Ila hapa kwa wabunge wa upinzani! Hamna lolote! Wapo tu alimradi wamekua wabunge!
 
Hawa watu wa ajabu sana, yaani MTU yupo radhi kusafiri miles away ili akapate media coverage! Anasahau hata changamoto za waliomchagua! Useless MP's!
wanaudhi sana. Unakuta wengine wanatembea geita wakati hata kijiji au mtaa wa jimbo lake hajawahi kuonekana.
Kuna wengine wanazidiwa thamani na wenyeviti wa mitaa.
Wako radhi kulia kuna njaa jimboni kwake hata kama kuna mito inayotililisha asali na maziwa. Useless
 
Lowasa pamoja na porojo zote za mafuriko feki alishakatwa na watanzania 2015.

Hao watetea mafisadi chadema wanapoteza muda wao
 
Nilitegemea labda baada ya kuwa na vyama vingi vya siasa hapa nchini, basi nitaona kizazi kipya cha hoja na mawazo ambayo kamwe chama tawala kisingeweza kuyawaza!

Ajabu yake nimekutana na upinzani ambao agenda yao ni malalamiko na tuhuma tu bila kuwa na !awazo mbadala!

Nimeshindwa kuona faida ya kua na mpinzani ambaye hana la kumfanya tofauti na yule niliyemzoea!

Kama mwananchi wa kawaida analalamika na mbunge wake wa upinzani analalamika kwa jambo hilo hilo kuna faida gani ya kua na mtu ambaye anauwezo kama wangu?

Wabunge wa upinanzani wameshindwa hata kujitofautisha na wale wa chama tawala kwa kuhakikisha kua majimbo yao hayana changamoto zozote ukijumuisha na dalili za ukame!

Majimbo yote ya uchaguzi Tanzania yanafanana kwani vilio ni vile vile!

Naanza kujiuliza nini faida ya vyama vya upinzani kama na wao wanafanya Yale Yale wanayoyakosoa!

Kwa hapa nchini kwetu chama tawala kinaendesha siasa za kishamba ile mbaya, wana wivu wa kipuuzi pindi wapinzani wakibuni jambo wanaona wapinzani watapata uungwaji mkono hivyo njia pekee ni kuhujumu wazo lao. Nakumbuka halmashauri ya moshi enzi Ndesamburo akiwa mbunge alitaka wanafunzi wote wa shule za msingi walioko ndani ya minispaa hiyo wasome bure. Kilichoendelea pale ilikuwa ni wivu wa kisiasa ili kuhujumu jambo hilo, leo hii wanafunzi wanasoma bure baada ya chama chovu kuiga. Hivi majuzi hapo jijini Dar wapinzani walitaka kuweka kiwanda cha mbolea kwa kukusanya taka, ona wivu uliojitokeza haijapata kutokea. Kwenye janga la tetemeko huko Kagera wapinzani walitaka kupeleka misaada kwa wahanga, kama kawaida hila ya wazi ikajitokeza eti misaada yote itaratibiwa na serekali, kilichoendelea kwenye misaada hiyo iliyosimamiwa na serekali ni aibu ya karne. Kwa hiyo wala usijifanye kuleta mada za kipuuzi ukidhani hatujui hila za ccm kisa wanamiliki dola wakati hawana uwezo. Halafu siku hizi mmejijua hamna ubunifu mmebaki mnalazimisha eti mtu akikosoa aseme ni nini kifanyike, kama hamjui ni nini kifanyike kwanini muibe kura ili muendelee kukaa madarakani?
 
Nilitegemea labda baada ya kuwa na vyama vingi vya siasa hapa nchini, basi nitaona kizazi kipya cha hoja na mawazo ambayo kamwe chama tawala kisingeweza k
Ajabu yake nimekutana na upinzani ambao agenda yao ni malalamiko na tuhuma tu bila kuwa na !awazo mbadala!

Nimeshindwa kuona faida ya kua na mpinzani ambaye hana la kumfanya tofauti na yule niliyemzoea!

Kama mwananchi wa kawaida analalamika na mbunge wake wa upinzani analalamika kwa jambo hilo hilo kuna faida gani ya kua na mtu ambaye anauwezo kama wangu?

Wabunge wa upinanzani wameshindwa hata kujitofautisha na wale wa chama tawala kwa kuhakikisha kua majimbo yao hayana changamoto zozote ukijumuisha na dalili za ukame!

Majimbo yote ya uchaguzi Tanzania yanafanana kwani vilio ni vile vile!

Naanza kujiuliza nini faida ya vyama vya upinzani kama na wao wanafanya Yale Yale wanayoyakosoa!

Upinzani Tz ni gunia la misumali. Nimecheka kuona mbunge anayeitwa Lwakatare anaongoza manispaa isiyo na route ya daladala za mjini hata moja mpaka wananchi wanafikia kulaani. Tukajaribu kumshauri lakini majibu yake ni sawa na mtu ambaye haijawahi hata kuvuka mipaka ya mkoa wake, hajuhi huwa wanafanyaje na aanze vipi. Hivi upinzani wa hivi usiyo na tija wa kazi gani?
 
Back
Top Bottom