Hakuna faida ya wabunge wa upinzani!

Hawa watu wa ajabu sana, yaani MTU yupo radhi kusafiri miles away ili akapate media coverage! Anasahau hata changamoto za waliomchagua! Useless MP's!

Kula karanga kijiweni
Kwenda kupiga kengele shule aliyosoma

sijawahi mkubali wala sintokaa nifanye hivyo
 
unategemea nini kwa mbunge anayepewa mikopo na mashirika ya pensheni halafu awatetee wastaafu au azuie fao la kujitoa ni heri ya demokrasia ya chama kimoja kuliko hivi sasa kumejaa wasanii
 
Nilitegemea labda baada ya kuwa na vyama vingi vya siasa hapa nchini, basi nitaona kizazi kipya cha hoja na mawazo ambayo kamwe chama tawala kisingeweza kuyawaza!

Ajabu yake nimekutana na upinzani ambao agenda yao ni malalamiko na tuhuma tu bila kuwa na !awazo mbadala!

Nimeshindwa kuona faida ya kua na mpinzani ambaye hana la kumfanya tofauti na yule niliyemzoea!

Kama mwananchi wa kawaida analalamika na mbunge wake wa upinzani analalamika kwa jambo hilo hilo kuna faida gani ya kua na mtu ambaye anauwezo kama wangu?

Wabunge wa upinanzani wameshindwa hata kujitofautisha na wale wa chama tawala kwa kuhakikisha kua majimbo yao hayana changamoto zozote u tvkijumuisha na dalili za ukame!

Majimbo yote ya uchaguzi Tanzania yanafanana kwani vilio ni vile vile!

Naanza kujiuliza nini faida ya vyama vya upinzani kama na wao wanafanya Yale Yale wanayoyakosoa!
Tungekuwa hatupati faida ya kuwa na vyama vya upinzani msingehangaika kugawa milungula ya tsh. Mil.10 kwa wabunge kupitisha misaada wa habary
 
Kwani wabunge wa upinzani wana budget ya maendeleo? au budget inatoka selikalini baada yakuidhinishwa na bunge? Kama haongei kitu hana maana. Lkn kama anaongea na kuiambia selikali matatizo yawananchi na hakuna kinachoendelea yeye angefanyaje. Angetoa pesa kutoka mfukoni mwake?
 
Upinzani Tz ni gunia la misumali. Nimecheka kuona mbunge anayeitwa Lwakatare anaongoza manispaa isiyo na route ya daladala za mjini hata moja mpaka wananchi wanafikia kulaani. Tukajaribu kumshauri lakini majibu yake ni sawa na mtu ambaye haijawahi hata kuvuka mipaka ya mkoa wake, hajuhi huwa wanafanyaje na aanze vipi. Hivi upinzani wa hivi usiyo na tija wa kazi gani?

hiyo manispaa ya bukoba imeanza lini kuwa haina route unaweza kumshangaa mbunge ambaye hana hata miezi 18 tangu achaguliwe? huku ukishangilia kila ukisikia mbunge fulani yuko polisi we haya Mungu anakuona.
 
Miezi 18 mnaona ni midogo na mnaona ni sawa mambo kuwa yalivyo, ruti tu miezi 18 je kujenga soko itatumia miaka mingapi? Msiwe mnapenda kuonewa huruma hata kwenye vitu vidogo kiasi hiki. Na mbona nyinyi wenyewe kila siku mnatathini kazi ya Magufuli kwa mabaya mengi wakati na nyie ndo wale wale? Mkiona rais kuwakosoa wenzenu basi kubalini pia kusahihishwa na kupewa vidonge vyenu
 
Nilipokuwa darasa la pili kuna rafiki yangu alikuwa ukimshinda marks kwenye somo anaanzisha maada yenye maudhui na kiwango kama hiki... No context!... wee hata mpira hujui kucheza. Leo sikumegei kitumbua nk. Eti upinzania hakuna maana yeyote! seriously!
 
Mimi pia sioni faida ya kuwa na rais kutoka CCM, kila kitu analalamika,mara sukari imefichwa na wafanya biashara,mara hela zimefichwa ndani,mara wapiga dili wamenunua magazeti kutangaza uongo,BORA NCHI ISIWE NA RAIS KILA MTU AJIONGOZE ANAVYOJUA MAANA HAKUNA UTOFAUTI NA TUKIWA NA RAIS.
wametaka jiji dsm wamepewa hadi sasa hakuna jpya
 
Nilitegemea labda baada ya kuwa na vyama vingi vya siasa hapa nchini, basi nitaona kizazi kipya cha hoja na mawazo ambayo kamwe chama tawala kisingeweza kuyawaza!

Ajabu yake nimekutana na upinzani ambao agenda yao ni malalamiko na tuhuma tu bila kuwa na !awazo mbadala!
Nimeshindwa kuona faida ya kua na mpinzani ambaye hana la kumfanya tofauti na yule niliyemzoea!

Kama mwananchi wa kawaida analalamika na mbunge wake wa upinzani analalamika kwa jambo hilo hilo kuna faida gani ya kua na mtu ambaye anauwezo kama wangu?

Wabunge wa upinanzani wameshindwa hata kujitofautisha na wale wa chama tawala kwa kuhakikisha kua majimbo yao hayana changamoto zozote ukijumuisha na dalili za ukame!

Majimbo yote ya uchaguzi Tanzania yanafanana kwani vilio ni vile vile!
Naanza kujiuliza nini faida ya vyama vya upinzani kama na wao wanafanya Yale Yale wanayoyakosoa!
hasara zote tunazo hesabu kama taifa ni kwasababu ya ccm isiyo jua kuongoza bali kutawala.
 
Kwani wabunge wa upinzani wana budget ya maendeleo? au budget inatoka selikalini baada yakuidhinishwa na bunge? Kama haongei kitu hana maana. Lkn kama anaongea na kuiambia selikali matatizo yawananchi na hakuna kinachoendelea yeye angefanyaje. Angetoa pesa kutoka mfukoni mwake?
Yale mamilioni wanayopewa wabunge kwa ajili ya maendeleo majimboni mwao, nioneshe hata mfereji wa umwagiliaji uliochimbwa na mbunge wa upinzani! Yaani hawa jamaa wamegeuka waajiriwa wa bunge badala ya kuwajibika kwa wananchi, kazi yao ni kukopa mabenki tu na kufanya maendeleo binafsi wakirudi majimboni wanawadanganya wapiga kura wao!

Ajitojeze hapa mbunge wa upinzani aliyekopa fedha benki kwa ajili ya maendeleo ya wapiga kura wake! Nitamwona shujaa!
 
Mtoa mada inawezekana hauna uzoefu na siasa, mbona kwa sas mambo mengi anayotekeleza CCM ni sera za wapinzani, ni mara ngapi wapinzani wamelalamika na kutoa ushauri?
 
Ukiacha wabunge nafikiri vyama vya upinzani vimefanya kazi kubwa sana ambayo mtu asiejielewa hawezi kujua,kwanza kabisa ni elimu ya uraia au kumfanya mwananchi ajue wajibu wake na kujua pia haki zake kama mwananchi,hili ni jambo kubwa sana sio la kubeza maana nadhani hali ingekuwa mbaya zaidi ya ilivyo sasa bila ya upinzani,wananchi wanazidi kupata uelewa isipokuwa kuna mambo mengi yanakwamisha jitihada hizi ikiwemo kukosekana kwa katiba inayoendana na wakati huu tuliopo ambao mambo mengi yamebadilika kisiasa kiuchumi nk,lakini bado tunatumia katiba iliyopitwa na wakati matokeo yake ndio haya,
kuhusu ubunge kazi yake kubwa ni kutunga sheria na kuisimamia,kukosoa na kuiwajibisha serikali iliyo madarakani haijalichi iwe ya ccm au cuf hiyo ndio kazi kuu ya bunge na wabunge,haya mambo sijui ya kutegemea mbunge ajenge barabara,achimbe kisima haya yanatokana na mipango ya serikali,kama serikali haitaki/haina mpango wa kuleta umeme kwenye jimbo fulani basi umeme kuja hapo ni majaliwa lakini sio waziri mkuu,cha muhimu ni kuona wabunge wakikataa kupitisha miswada ambayo haina maslahi kwa taifa kama mikataba ya kinyonyaji,miswada mfano wa kuchaji shilingi elfu moja kwa kila laini ya simu ambayo unamiliki kila mwezi wabunge wa upinzani waliisusia wa ccm wakaipitisha,miswada kama ya cyber crime ambayo upinzani waliigomea unataka nini zaidi ya hayo?tumeona miradi na mipango mingi ya wabunge na vyama vya upinzani ikihujumiwa,watu wanachangia damu japo kuna uhitaji damu inakataliwa kisa imetoka upinzani,mbuge anajitolea hadi ambulance hospitali haipokei,mfano wa mradi wa taka kinondoni tumesikia ya kusikia na mengine mengi tu,je unataka nini zaidi ya hapo?au tunajitoa ufahamu
 
Back
Top Bottom