Hakuna Elimu ya Chuo ya Bure waliosoma vyuo kwa mkopo walipe!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna Elimu ya Chuo ya Bure waliosoma vyuo kwa mkopo walipe!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kamundu, Jan 12, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu huu ni mtandao wa kuandika ukweli hata kama ukweli hautakuwa na ushabiki.

  Kitendo cha kuna migomo kila siku kwenye vyuo vya Tanzania ni swala la kisikitisha na tatizo kubwa kwa mawazo yangu ni ukweli kwamba wanafunzi wengi na jamii yetu inafikiria elimu ya juu ni ya bure kama umefanya vizuri form 6 na kuchaguliwa. Ukweli ni kwamba elimu sio bure na nakumbuka miaka michache iliyopita niliambiwa gharama za kusoma Chuo kikuu cha Dar kwa miaka mitatu ni TSH 15,000,000 kwa mwanafunzi kuanzia kulipa walimu, vitabu, posho, nyumba, afya na vyakula. Kabla hatuja kimbilia kuwawekea hawa vijana wa vyuo madeni ni lazima tujiulize je Waliosoma mika ya nyuma kuanzia Kikwete wamelipa madeni? kama hawajalipa na pesa yao imetokana na nchi kuchukua mikopo je ni wakati wa wale waliosoma na wenye uwezo na kazi waanze kulipa madeni yao ili hiyo pesa itumike kwa mikopo ya wanafunzi wengine?. Ninashangaa Watanzania wengi waliosoma kwa mikopo ambayo hawajalipa kuweka ushabiki kwamba chuo ni bure au hawa vijana walipe wakati wenyewe hawajalipa madeni wakati wana uwezo.
  Sisi Watanzania wenzenu tuliosoma nje tumesoma kwa mazingira magumu sana na wengi wetu tumekuja nje kwasababu nafasi ya course nzuri za vyuo vikuu zilikuwa chache. Mfano mimi nilipata Div 3 nzuri tu lakini Course niliyopangiwa ya ualimu pale Mlimani sikuipenda nilitaka kusoma Economy au Finance. Nilikuja nje na baada ya miaka mingi nikafanikiwa kupata mkopo wa $20,000 wa kusoma na serikali ya USA inahakikisha mimi nalipa kwani wenyewe ni wa hisani. Sasa mimi ni lazima nilipe kwasababu nisikolipa inachukuliwa kwenye mshahara kama ilivyo kodi vile. Pesa nayolipa inaenda kusaidia wengine na riba yangu ni 3% tu kwa mwaka kwa miaka 20. Lakini elimu ni muhimu kipato cha mtu aliyemaliza chuo ni mara mbili ya mtu aliyemaliza sekondari tu!.
  Watu wenye uwezo na waliosomesha vyuo kwa mikopo ya serikali wanatakiwa kulipa lakini ni lazima tuhakikishe hiyo pesa inaenda kwenye mikopo ya vijana wetu wanaomaliza sekondari. Lakini tukikaa hapa tunawadanganya hawa vijana kwamba elimu ni bure na ukimaliza chuo unaingia mitini hatuwezi kusaidia jamii yetu kwani hatutakuwa na middle Class Tanzania.
   
 2. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,131
  Likes Received: 3,320
  Trophy Points: 280
  Watalipaje wakati ajira hakuna?
   
 3. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  uko sawa mkuu. walipe ili wengine nao wakopeshwe.
   
 4. M

  Makupa JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  acheni kuleta uzushi hapa mbona enzi za Nyerere elimu ilikuwa bureee issue ilikua ni akili yako tu na si vinginevyo
   
 5. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Ajira hakuna,mishahara midogo,kazi zenyewe hazieleweki,halipi mtu hapa!!!
  Mbona wao walisomeshwa bure na kupewa kila kitu bure enzi hizo!!!??
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mimi silipi mpaka nimalize mkopo wa bank kwa ajili ya biashara yangu, nimejiajiri mwenyewe, yale ma academic certificate yapo kabatini, no wonder waje yachukua
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wamekwambia hawalipi?
   
 8. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tutasonga mbele sana kama mambo muhimu na ya msingi yanawekwa wazi, kuhusu hili nakupongeza sana ikizingatiwa huku mitaani mambo haya yanapotoshwa sana
   
 9. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Makupa, ni kweli Nyerere alisomesha bure kwa kipindi fulani lakini wakati ule wasomi walikuwa wachache na siasa ya ujamaa ilishika hatamu upande mwingine wa dunia kisi ambacho wafadhili wa ncho wakati huo walikiwa ni waungwana kwelikweli. Leo sivo, dawa ni kulipa deni lako ili ndugu zako wa mikoa ya kusini wasome kwa urahisi.
   
 10. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Sina cha kulipa coz nlisomeshwa ha hela ya baba yangu! Period!
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Nani aliokudanganya ilikuwa bure? na zile kodi za watu zilizokuwa zikikatwa zilienda wapi?
   
 12. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nyie wote mnao sema enzi za nyerere wasomi walikuwa wachache ndio mana aliweza kusomesha bure nachelea kusema hamna tofauti na anayesema tanzania haiendelei kama rwanda kwa sababu nchi ni kubwa.
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  mkuu umesema vyema ..inabidi mliosoma kwa mikopo mlipe deni ili ndugu zenu wengine wasome..mimi nimesoma kwa kupiga box
   
 14. K

  Kanyigo JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kwani sasa hivi hatulipi kodi!?
   
 15. N

  Nyumisi JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  Tatizo la vijana kukosa mikopo si la kulaumu wahitimu kutorudisha mikopo. Ni suala la kulaumu serikali kutotumia rasilimali nyingi nchi ilizojaliwa kama madini, wanyamapori, n.k kukusanya mapato ambayo yangewezesha kutoa elimu kwa vijana. Badala yake madini yanagawiwa bwerere kwa wazungu ambao wanawahonga maafisa wa serikali vijisenti na kuwasomeshea watoto wao nje kwa gharama ya kuwasaliti watu zaidi ya milioni 42. Pia mapato mengi ya serikali ambayo yangesaidia elimu ya vijana yanaishia kufisadiwa na watu wachache na pesa nyingine kutumika kwenye anasa za serikali kama kununua mashangingi, safari za nje zisizoisha na vitu kama hivyo. Kipindi cha mwlimu serikali ilikuwa inakusanya mapato ya kutosha na kuyatumia kwa uadilifu na kipindi hicho akili yako tu ndo ilikuwa tiketi yako. Unagharamiwa kila kitu kuanzia nauli, mavazi, malazi, chakula, pesa ya matumizi, unanyooshewa nguo hadi unatandikiwa kitanda. Kwa hiyo ulichokiandika hapa ni frustrations ambazo unazielekeza kusikostahili. Chanzo cha hili kinajulikana na ndicho wananchi wanalia kila kukicha, UFISADI.
   
 16. clet 8

  clet 8 JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,065
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Walipe nn, wakati wakilipa zinaishia kujaz matumbo ya wachache na umma kuachwa ukitaabika!

  Halafu, ww sio mzalendo. Kwa nini ulikimbia ualimu? Je, waliokufundisha na wao wangefanya kama ww ungefika hapo ulipo?
   
Loading...