Hakuna anayepoteza muda bali unapoteza nguvu ya kufikia mafanikio yako

Nov 2, 2023
62
63
Tunapenda kutumia msemo wa kupoteza muda kwa kumanisha kufanya kitu kisicho na faida kwetu. Ila ukweli hakuna anaye weza kupoteza muda bali unautumia kwa kutenda tofauti na malengo yako yenye mafanikio yako kwa kujua au kutojua.

Na unaweza pia ukawa unaishi ndani ya giza bila kujua kwa kuendeshwa na kutafuta matokeo ya vitu zaidi au kufanya kitu kwa ajili ya fedha tu kuliko manufaa makuu ya kitendo yanayo weza kupanda mbegu kwenye kila utendaji wako na kukuletea matunda ya kudumu. Siku yenye mafanikio si uliyoingiza kiasi kikubwa cha fedha hapana, bali uliyoweza kutoa ufanisi wako unao ufurahia pia na kutenda kwa moyo wote kwa kukiachia baraka ukitendacho. Yani akili na mwili kushirikiana kwa pamoja kwenye utendalo bila kuwa na uhusika wa kulazimisha chochote kwa kuwa amani na furaha yako yote imehamia kwenye utendaji wako.

Muda kwa vyovyote vile upo hauna mwenyewe wa kuudhibiti "neutro" kwa watu wote huwezi kuufanya chochote. Ila nishati yako ya utendaji wa mwili katika siku ina kikomo. Ukijichosha kwa kufanya vitu visivyokuwa na uhalisia na wewe kwa kujua au kutojua utaishia kuwa na shida kubwa ya kutokuwa na muendelezo wa kupanda ngazi kuelekea kuwa bora katika utendaji wako na kufanikiwa kwenye chochote.

Unaweza ukawa unajiona uko kwenye mbio sahihi za mafanikio kumbe unajichosha mwenyewe kwa kuwa unacho kimbilia hakipo bali ni matarajio tu yakupata faraja kuziba shida zako tu. Itakufanya ukanasa kwenye mtego usio na uhalisia wa kukufanikisha bali kukupotosha kwa kukupa matarajio yasiyo ya kweli ya kufanikiwa.

Ukiona unaishi kwa kufanya vitu kwa ajili ya matokea pekee bila kujali njia na kugemea furaha kwenye matokeo zaidi ujue upo kwenye giza bado la kujichosha. Kwa chochote unachofanya kama hakina furaha ya kutoka ndani wakati unakitenda basi hakiwezi kufanikiwa na hakina mahisiano na wewe ni unajilazimisha na hutokuwa na furaha ya maisha ya kiutendaji.

Na kwanini uishi kwa kujigiza na kulazimisha matendo ulipo kwa ajili tu ya kuonekana na watu wengine bila kujua unajitesa undani wako. Huhitaji kuendana na jamii una hitajika uishi kwa kuendana na kipawa na kipaji chako na uwezo wako ulio barikiwa ndio uakisi mazingira yako. Na maisha yatakuwa ya furaha, kwa nguvu zako kwenda kwenye njia yako ya mafanikio kwa matendo kutoka moyoni na kufungua ufanisi wako wote bila kujishurutisha mwenyewe.

Nb: Hatuhitajiki kuwa kama kila mtu aliyefanikiwa, tunatakiwa tuwe kama tulivyo bila kuficha kwenye nafsi zetu wenyewe kwa kuwa kila mtu ana thamani kubwa kwa alichobarikiwa nacho akikitenda kiwe maisha yake na lazima atafanikiwa.
 
Gazeti lote hili unaelezea maana ya kupoteza muda.

Binafsi naona kama hujui maana ya "Kupoteza muda"
 
Sahihi kabisa.

Watu wengi wanafuata mkumbo kwa kufanya vinavyo wapa Amani na furaha wengine huku wao wakiangua kilio kimya kimya, Pia huko ni kupoteza mda.
 
Back
Top Bottom