Watu wengi wana roho mbaya na unafiki sana, ubaguzi, hawaelewi kuwa kutofautiana kiitikadi sio uadui.
Wanadhani wanaoamini waaminicho wao ndio wana akili, wajanja na majembe ila wanaoamini tofauti na wao ni wakufa tu, wajinga na pengine hawana akili kabisa.
Kibiti kumetokea mauaji ya watu wengi sana ila baadhi ya watu tena humu ni wengi wanashangilia eti wafe waishe, ili hicho chama kife!!! Wengine ooohhh ndo wadhalimu!! Wamekufa viongozi wa CUF juzi watu haohao pia eti ni dhambi sijui nini wanaua cuf wafe tu.
Hivi hao sio binadamu wenzetu?? Kutofautiana na sisi kimtazamo ni sababu ya baadhi kushangilia vifo vyao?
Jana Mh. Mbunge kapigwa risasi baadhi ya watu wanashangilia kweliiii???
Lakini cha kushangaza zaidi wengi waliozodoa waliokufa kibiti na ajali ya CUF wanataka wote tuungane nao tumlilie Lissu??? Kwamba ndie mwenye moyo tu na kuliko wengine???
'Lets Pray for Lissu' Mungu amponye arejee kufanya kazi zake.