Echolima1
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 9,426
- 7,851
- Thread starter
- #41
Umedanganywa na Wafuga Midevu na Majini wafiristi si Wapalestina hawa walioanza kuitwa hivyo 1967 na Yasser Arafat!!!!
Je! Wapalestina ni watu gani, na sehemu yao katika biblia ni ipi?
Jina Palestina limetoka na Neno la kiyunani Filistia, lenye maana ya ardhi ya wafilisti. Kwahiyo ile Filisti inayotajwa kwenye biblia ndio Palestina unayoisikia sasa.
Lakini Jambo ambalo wengi wanachanganya ni kudhani kuwa wafilisti walikuwa ni waarabu. Si kweli, kwani waarabu walikuwa ni watoto wa Ishmaeli kutoka kwa Ibrahimu, lakini wafilisti walikuwepo kabla hata ya Ibrahimu, na walitokea katika uzao wa Hamu.
Watu hawa walikuwa ni wapagani moja kwa moja, na waliabudu miungu yao mikuu mitatu iliyoitwa Ashtorethi, Baal-zebubu, na Dagoni.(Waamuzi 16:23, 2Wafalme 1:2, 1Samweli 31:10,)
Wafilisti walikwenda kuweka makazi yao, katika nchi ya Kaanani. Upande wa kusini, kutoka mto Yordani mpaka ule wa ile habari kubwa (Bahari ya Mediterenia). Na baadaye kipindi cha akina Samweli wakawa na miji yao mitano imara iliyoitwa Gaza, Ashdodi, Gathi, Ashkeloni, Ekroni (1Samweli 6:17, Yoshua 13:3)
Hivyo Ibrahimu alipoitwa na Mungu na kuambiwa aindee nchi ile aliwakuta tayari wapo, na wameshajiwekea ngome zao (Mwanzo 21:32, 34, 26:1).
Rudi shule Wapalestina hawa ambao ni Magaidi ni waarabu kama walivyo waarabu wengine wala si Wafiristi kama ulivyodanganywa!!