Hakimu wa kesi ya Mbowe, Matiko ateuliwa kuwa Jaji

Joined
Apr 18, 2012
Posts
95
Reaction score
213
50949553_1852515244860760_1506585565779197952_n.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Dar es salaam Wilbard Mashauri kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo jana kupitia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwatangaza baadhi ya majaji wengine wa mahakama ya Rufani na mahakama kuu.
Miongoni mwa Majaji walioteuliwa ni Jaji Wilbard Mashauri ambaye ni Hakimu katika kesi inayowakabili viongozi 6 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lakini pia anasimamia kesi inamkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Jamal Malinzi.
Katika kesi ya inayomkabili Freeman Mbowe na Esther Matiko, akiwa Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri aliwafutia dhamana viongozi hao wawili kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa na Mahakama.
Kesi nyingine ambayo inasimamiwa na Wilbard Mashauri ambaye kwa sasa ni Jaji, ni kesi inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU, Godfrey Gugai ambaye anatuhumiwa kwa kutakatisha pesa pamoja na kumiliki mali ambazo haziendani na na kipato chake.

SOURCE:EATV
 
Sasa hapa itaonekana kateuliwa kisa maamuzi ya hiyo kesi.

Kumbe unaweza kuta alistahili kuteuliwa tangu miaka kadhaa nyuma kwa hiyo sasa hivi anaona hatimaye katendewa haki na yeye aanza kula kuku kwa mrija.
 
Hakua na vigezo?

Au ukiwafunga mbowe na matiko unakosa vigezo vya kuteuliwa?
 
Majaji walioteuliwa wapo 21, ukimtoa Mashauri ambaye mnadai kesi ya Mbowe na Matiko ndio imempa ujaji, je hao 20 waliobaki ni kesi zipi zimewapa ujaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii case ya Kamanda Mbowe ni ulaji tosha

I wish ningekuwa wale askari...ningehakikisha siku ya mahakamani wanaenda kwa kichura chura...halafu ubandidu kwa sana kumzidi yule Kibakuli aliyem bastola Nape!

halafu hii style ya kuwashukuru kwa kuwatunuku vyeo Mzee wa Malofa aliitumiaga sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
50949553_1852515244860760_1506585565779197952_n.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Dar es salaam Wilbard Mashauri kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo jana kupitia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwatangaza baadhi ya majaji wengine wa mahakama ya Rufani na mahakama kuu.
Miongoni mwa Majaji walioteuliwa ni Jaji Wilbard Mashauri ambaye ni Hakimu katika kesi inayowakabili viongozi 6 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lakini pia anasimamia kesi inamkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Jamal Malinzi.
Katika kesi ya inayomkabili Freeman Mbowe na Esther Matiko, akiwa Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri aliwafutia dhamana viongozi hao wawili kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa na Mahakama.
Kesi nyingine ambayo inasimamiwa na Wilbard Mashauri ambaye kwa sasa ni Jaji, ni kesi inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU, Godfrey Gugai ambaye anatuhumiwa kwa kutakatisha pesa pamoja na kumiliki mali ambazo haziendani na na kipato chake.

SOURCE:EATV
Dah Mpaka Yesu arudi tutakuwa tumekwisha. Lkn tusikate tamaa, ukiona shida nyingi zikitokea ujue ukombozi karibu unakuja. Hizi ni hongo
 
Back
Top Bottom