Hakimu kesi ya Abdul Nondo agoma kujitoa kuisikiliza; adai sababu za kutakiwa kujitoa hazina msingi

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
776
1,330
Hakimu anayesikiliza kesi ya Abdul Nondo amegoma kujitoa, akisema kuwa kufanya hivyo ni kusababisha usumbufu kwa Mahakama itakayolazimika kumpanga Hakimu mwingine kwani malalamiko ya mshitakiwa na sababu alizozitoa kutaka hakimu huyo kujitoa hazina msingi.

Hii ni kufuatia Nondo kuwasilisha Mahakamani barua siku ya Jumatatu Mei 14, akitaka Hakimu Mpitanjia ajitoe kuendesha kesi hiyo kwa hoja 5.

Zaidi >> Abdul Nondo amkataa Hakimu anayesikiliza kesi yake Iringa
 
Huyo hakimu kwa hilo jina lake tu, hata mimi ningemkataa, na kuomba ajitoe. Kwa nini anang'ania kuendesha hiyo kesi? Kuna nini nyuma ya pazia?
 
Mie nadhani huyo Hakimu kama hana interest na hiyo kesi ajitoe na kauli ya eti Mahakamani itapata usumbufu yeye inamhusu nini? Au anataka kuwa kama Hakimu wa mh.Sugu?
 
Hakimu anayesikiliza kesi ya Abdul Nondo amegoma kujitoa, akisema kuwa kufanya hivyo ni kusababisha usumbufu kwa Mahakama itakayolazimika kumpanga Hakimu mwingine kwani malalamiko ya mshitakiwa na sababu alizozitoa kutaka hakimu huyo kujitoa hazina msingi.

Hii ni kufuatia Nondo kuwasilisha Mahakamani barua siku ya Jumatatu Mei 14, akitaka Hakimu Mpitanjia ajitoe kuendesha kesi hiyo kwa hoja 5.

Zaidi >> Abdul Nondo amkataa Hakimu anayesikiliza kesi yake Iringa
Nondo asubiri alimwe nondo zake tu.
 
Mawakili wa serikali (state attorneys) wakati mwingine uomba mahakimu kujitoa wiyj flimsy reasons na mara nyingi sana hujitoa. Hii pia ni kuonyesha haki inatendeka. Au kuna nguvu nyima ya maamzi haya ya hakimu
 
Yale yale ya kesi ya Sugu, hawa mahakimu wahuni hawatufai, wanachafua taswira ya Mahakama.
 
Abdu Nondo ajiandae tu kisaikolojia kwani hawa jamaa wameamua kumfunga tu, hata afanye nini, ni lazima wajione wameshinda na huyo hakimu ameshapewa maagizo ya nini cha kufanya.
 
Ni kawaida mbona hata mwenyekiti hakimu kagoma kujitoa kwa sababu uchwara.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom