Hakimu, Karani mahakamani kwa kupokea rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakimu, Karani mahakamani kwa kupokea rushwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]HAKIMU, Karani akiwemo na Mhasibu wa Mahakama ya Mwanzo Ukonga jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya kushawishi kupokea rushwa ya shilingi laki moja.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Hakimu huyo alifahamika kwa jina la Ndevera Kihangu, Karani alifahamika kwa jina la Eveline Mowo na mhasibu ni Victoria Mtasiwa.

  Washitakiwa hao walifikishwa Mbele ya Hakimu Mkazi, Ritha Tarimo na upande wa Mashitaka uliongozwa na Wakili wa Serikali Salha Abdallah

  Abdallah alidai kuwa washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na makosa matatu likiwemo la kushawishi na kuomba rushwa ya kiasi hicho cha fedha.

  Alidaiwa Aprili 24 mwaka huu, katika Mahakama ya Mwanzo Ukonga washitakiwa hao walimshawishi Joyce Msaki awapatie kiasi hicho cha fedha ili wampatie dhamana katika kesi inayomkabili iliyopo katika mahakama hiyo.

  Abdallah alidai kuwa, kosa la pili ambalo linamkabili mshitakwia wa kwanza pekee ni kupokea rushwa ya shiling 40,000 kama kianzio cha deni hilo
  Ilidaiwa Mei 27 mwaka huu washitakiwa hao walipokea kiasi cha fedha cha shilingi 60,000 kutoka kwa Joyce ikiwa ni malizio la deni hilo

  Kesi hiyo itarudi tena Juni 22, mwaka huu kwa kutajwa[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sheria ni nzuri pindi zikifuatwa! Mtazamo wangu kisutu pale panaongoza kwa rushwa ktk mahakama zote tz!!!!
   
 3. C

  CHRIS CM Member

  #3
  Jun 12, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  nina mashaka na mshahara wa huyu hakimu, au ni tamaa tu za dunia
   
Loading...