Hakimu aburutwa kortini kwa rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakimu aburutwa kortini kwa rushwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bagwell, Sep 25, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Pamela Kalala amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mke wa mmoja wa washtakiwa aliokuwa akisikiliza kesi yao.

  Hakimu Kalala alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana asubuhi na kusomewa mashtaka matatu ya kuomba rushwa ya Sh3 milioni na kupokea rushwa ya Sh900,000 kwa nyakati tofauti.

  Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Allen Kasamala alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti Februari, mwaka huu.
  Katika kosa la kwanza, Kasamala alidai kuwa mshtakiwa huyo aliomba rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa Josephine Omar ambaye ni mke wa mmoja wa washtakiwa katika kesi namba 703 ya mwaka 2008 inayohusu kujipatia fedha kwa njia zisizo halali.

  Kasamala alidai kuwa mshtakiwa alimwomba Josephine kiasi hicho cha rushwa ili kumshawishi ampendelee mumewe katika kutoa uamuzi wa kesi hiyo aliyokuwa akiisikiliza.

  Katika shtaka la pili, Kasamala alidai kuwa Februari, tarehe isiyofahamika, mshtakiwa alipokea rushwa ya Sh800,000 kutoka kwa Josephine na katika kosa la tatu, alidai kuwa Februari 6, mwaka huu mshtakiwa alipokea rushwa ya Sh100,000 kutoka kwa mwanamke huyo.

  Kasamala alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo akiwa mwajiriwa wa Idara ya Mahakama kwa wadhifa wa Hakimu Mkazi.

  Alisema Kalala alitenda makosa hayo kinyume cha Kifungu cha 15 cha Sheria ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
  Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashtaka yote na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

  Hakimu Katemana alimwachia mtuhumiwa huyo kwa dhamana, baada ya kutimiza masharti ambayo ni pamoja na kusaini bondi ya Sh1 milioni na kuwa na mdhamini mmoja anayefanya kazi katika taasisi inayotambulika, ambaye pia alisaini bondi ya Sh1 milioni.

  Hakimu Katemana aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 23, kwa ajili ya kutajwa.

  Mahakimu na rushwa
  Kalala anakuwa hakimu wa nne kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu kwa tuhuma za rushwa, katika kipindi cha miaka mitano.

  Desemba mwaka 2007, aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Jamila Nzota alipandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo akituhumiwa kupokea rushwa ya Sh700,000.

  Nzota alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kuomba rushwa hiyo kutoka kwa Mollel, aliyekuwa Mwakilishi wa Kampuni ya Amanarth Enterprises Ltd iliyokuwa na kesi ya madai namba 33/207 mbele yake, ili amsaidie.

  Katika kesi hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Hanzron Mwankenja (mstaafu kwa sasa), alimhukumu Nzota kwenda jela miaka kumi na moja kuanzia Mei 22, 2009, baada ya kupatikana na hatia katika makosa manne yaliyokuwa yakimkabili.

  Hata hivyo, Hakimu Mwankenja alisema mshtakiwa atatumikia adhabu zote kwa pamoja, hivyo alitumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

  Nzota hakuridhika na hukumu hiyo na kupitia kwa Wakili wake, Majura Magafu alikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, lakini katika hukumu iliyotolewa na Jaji Emilian Mushi, Aprili 30, 2010, alishindwa tena.
  Wengine ni aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Adolf Mahai, (2007) na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Ukonga, Ndovela Kihenga, (Juni 2011).
   
 2. baba junior

  baba junior Senior Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2012
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  imeandikwa,hakimu mkaz mahakama ya ilala,pamela kalala apandishwa kizmban kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.cha kushangaza eti februari,tarehe isiyofahamika mshtakiwa alipokea rushwa ya sh 800000/=then tar 6 alipokea tena sh 100000.swali,je ni ushaid hafifu au uandish dhaifu kusema tar isiyofahamika m2 fulan kapokea rushwa?
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Na wewe unarudia kosa lile lile la uandishi dhaifu, m2 ndo nini?
   
 4. baba junior

  baba junior Senior Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2012
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimeabbriviate Baba V
  V.
   
 5. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  hakimu Kalala


  sidhani kama kuna kesi ya msingi hapa tayari hati ya mashtaka ina mashaka
  itakuwa ngumu kwa upande wa mashtaka kuthibitisha haya pasipo kuacha mashaka
  walitakiwa kupeleleza kwanza wajiridhishe kisha ndio wampeleke mahakamani.
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,092
  Likes Received: 5,560
  Trophy Points: 280
  Hakimu wa mahakama ya wilaya ya ilala pamelala kalala amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mke wa mmoja wa washtakiwa aliekuwa akisikiliza kesi yake
  hakimu huyu ameshtakiwa kw akuomba million 3 na kukabidhiwa laki tisa kwa nyakati tofauti huku akitegewa bila kujijua ...kwa mara ya kwanza mshtakiwa aliomba million 3 kutoka kwa josephine omar ambae ni mke wammoja wa washitakiwa kesi namba 7003 ya mwaka 2008 inayohusu kujipatia fedha kwa njia zisizo halali

  mshitakiwa hakimu pamela aliomba hela ili ampendelee mumewe katika kesi hiyo aweze kumaliza mapema vinginevyo kesi ni nzito na itamzungusha sana na kuchukua muda wake kushinda mahakamani kila siku.....baada ya hapo ndipo josephine alipojipanga na mumewe na mtu aliekuwa kama shahidi wakampelekea laki 8, feb 6 akapokea laki 1, kwa habari zaidi nunua mwananchi vinginevyo wafanyakazi waatakosa mshahara

  tuudi kwenye mada kamili
  hivi huyu jaji mkuu anahisi kesi kucheleshwa ni tatizo la pesa ??kama anavyosema kila siku
  nahisi hapo juu tunaweza kujua na kupata src ya hali halisi ya mahakamani kwa nini kesi aziiishi kwa kweli ..inasikitisha sana sana ..na kutia aibu nitamuweka hapa hadharani lunch time kama ni ndugu yako umwambie akome kutunyanyasa kama amepewa majukumu atumie kihalali na si kutafuta utajiri picha na habari zaidi saa nane mchana
   
 7. Rohombaya

  Rohombaya JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 8,257
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Aibu sana pale vyombo vya kutafutia haki vinapohusishwa na rushwa. Twende wapi sasa kudai haki zetu?
   
 8. L

  La Voz Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama haelewi m2 ni nini atwambie baba v ndo nini.
   
 9. baba junior

  baba junior Senior Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2012
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ajabu, hajajibu.!
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  sio mahakama peke yake kila idara imeoza.
  PCCB nao wanaongoza kwa kuomba na kupokea rushwa
  na ndio hao hao wanaochunguza na kupeleka mashtaka ya rushwa mahakamani.
  fanya kautafiti kama wamjua mtu wa takukuru wana mali za kutisha na maisha yao halingani na mishahara yao
  mahakimu nao ndio usiseme. wabunge nao wanakashfa za rushwa, mawaziri na mikataba feki
  sijui tukimbilie wapi. polisi ndio usiseme. landa Nyerere peke yake ndie alikuwa msafi
   
Loading...