The Boss shida ya criteria ni shida kubwa. kila mtu anakuja na criteria ambazo zinasaidia kupendekeza Uni zao katika mia bora. Sina shaka kua hii hapa imetafitiwa na wamarekani wenyewe. Kumbuka kua model nzima ya Wallstreet, IMF WorldBank, NSEx TSEx, NasDaq, cac 40 na wengine wanategemea research za Havard, Oxfor, Cambridge kwa inovation na predictions zao. Hapo unadhani itakua rahisi kusema tatu hao wapo kwenye 100 kwenda chini? Lazima waseme these guys are the best you'll ever see.
Shida nyingine mfano ni pale wanapo tumia "citation" kama kigezo. Leo ni rahisi kupata researches za Havard mtandaoni. Na wanao tumia mitandao bado ni hao hao, kutafiti kuhusu context yao. mimi naweza tafuta research kuhusu dengue na nisipati wakati chuo kikuu cha Dar Es Saalam kina research nyingi na nzuri tu kuhusu topic yangu. Shida ni internet access, shida ni availability of the research on internet. Hii haina maana kua chuo kimeshindwa kutoa tafiti nzuri ila tu ni costs, logistics, management na mengine.
Mimi nina mfano hai. Kuna watu wanasomea Sheria UCB Bukavu tu hapa DRC wanaenda kupata PhD Belgium on a sister University (#191) na huko akaweza Cum Laude. Foundations ni nzuri sababu kwanza waalim ni wale wale wanakuja huku seasonally. Sasa hapa utasemaje hizi Uni huku sio nzuri? Hao surveyors walifika huku kuchunguza na kuweka research into context au they went for the easiest way?
A lot can be said. But as we wait to come up with our own list, there's no way mwanangu atasomea huku wakati uwezo wa kumtuma nje unaweza patikana... NO WAY
Ndugu m_kishuri na Xfactor, nakubalina nanyi kua data zina vary. But I challenge you to bring me a list where Tanzania ipo katika mia bora. Any list...
My point is: pamoja na kua kuna bias kibao, na kila mtu anavuta shuka upande wake, bado in any ranking sisi tumechelewa. Sasa wakati tukisubiri kuboresha elimu yetu ya vyuo vikuu, tuhakikishe watoto wetu wanapata elibu ilio bora ili waje kusaidia elimu yetu, na maendeleo yetu kwa jumla.
CC The Boss
True but hao wa tz waliosoma huko mbona hatuonani impact yao...? Wengi wanaburuzwa still na hawa hawa waliosoma udsm na vingine...
Vichwa vinabakishwa hukohuko huvioni hapa. Makanjanja na walio boogie ndio wanarudi.
UDSM kuna vichwa? kuna nusu vichwa, saa ngapi watakaa wafukuze mbu saa ngapi watakaa wafanye researches za maana?
Mara mjomba hana fees, mara dada anakuja mshughulikie kumfanyia mpango wa hospitali, mara babu kafa na lazima uende, mara jirani ana harusi unatakiwa kwenye kikao, kama hukwenda hata ukiingiliwa na mwizi ukipiga mayowe hawatoki kukusaidia, kisa hujenda kwenye kikao cha harusi cha mtoto wa The Boss. Kutabaki vichwa hapo? mimi nasema ni nusu vichwa, tena wala si nusu, ni shingo tu tulizonazo hapa.
Hapa hata research za maana hakuna kuna papers tu, na nyingi ukizisoma unaweza pata kichefu chefu, amini usiamini.
Kuna hizo funds za research? mawee!
Sisi bado sana kwa sasa, lakini tunaelekea kuzuri na InshaAllah gas tuliyojaaliwa nayo ije kutubadilisha.
True but hao wa tz waliosoma huko mbona hatuonani impact yao...? Wengi wanaburuzwa still na hawa hawa waliosoma udsm na vingine...
Vipi wale wa spesho skulz? Impact yao inaonekana?
mimi sioni chochote...watu hata kukosoa tu wanaogopa...
Teh teh teh.....Watanzania bado sana...kuna mengine hufanyika mtu ubanaki unashangaa tu.
Ukijaribu kuhoji wanaanza kukunyooshea kidole eti unajifanya unajua...mara ooh sijui uko nje ya mguso (out of touch).
Mtu unajikuta unapotezea tu.