Hakika sasa nimeamini alichosema Dr. Slaa kuhusu Kikwete

Kwanza chuoni pale mliman alipata degree kiwango cha PROBATUS yaani ikimaanisha alikua natoa necessary company kwa wenzake alafu leo ndo anaongoza nchi mnategemea nini? Ndo mkome!
 
Wakuu,
Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 nilipata kuisikia kauli maarufu ya Dr. Slaa kuhusu madhara ambayo nchi hii ingepata endapo kikwete angechaguliwa mara nyingine tena. Dr. Slaa alisema kwamba kumchagua kikwete na ccm yake ni kukaribisha janga la kitaifa na wananchi watakuja kujutia uamuzi wao.

Leo hii, ikiwa ni mwaka mmoja na miezi kadhaa, wananchi katika kila kona ya nchi wanalalamika ugumu wa maisha. Maisha yamekuwa magumu na kadri siku zinavyokwenda ndivyo bei za bidhaa zinavyozidi kupaa. Wakati hali ikiwa hivyo kwa wananchi, kikwete anaendelea na utekelezaji na nadhiri aliyojiwekea ya kuvunja na kuweka rekodi ya kuwa rais wa kwanza Duniani kutembelea nchi nyingi kama si zote ndani ya kipindi cha miaka kumi tu ya uongozi. Juzi tu baada ya kutoka Switzland alikotoa kauli ya kusisitiza umuhimu wa misaada, alirudi nchini na baadaye kidogo aliekea Uingereza. Hivi ninavyopost thread hii, yupo Botswana eti kwenye sherehe ya chama tawala. Akiwa kwenye safari hizo, tumeshuhudia wagonjwa wakifa kwa kukosa matibabu kutokana na mgomo wa madaktari, wananchi Songea wanauawa na polisi na karaha mbalimbali lakini yeye kwa raha zake anaendelea na safari na matanuzi yake.

Kwa mwenendo huu, sina budi kuamini kuwa kikwete ni janga la kitaifa.

Nyie mlioko huko Tanzania hamjui anachokifanya KIKWETE simsifii sana lakini ukiangalia nchi yetu kabla ya mwaka 2006, kuna baadhi ya mataifa yalikuwa hayaijui TZ, na hata fursa za uwekezaji (sio kuuza mashirika awamu ya 3) umeongezeka kipindi hiki cha JK 2, tujaribu kuelewa kuwa maisha ni Magumu hata hapa MAREKANI hili sio TZ peke yake, jaribu ku analyse issue vizuri,Nyanja nyingi zimebadilika leo Tanzania,
msiweke itikadi za chuki na vyama.
 
Narrow minded,hacha kudanganya watu na kufananisha western na Tanzania,i ve been Us na Uk pia,kwa nchi hizo serikali zinahakikisha wananchi wake wanapata basic needs,je hiyo kitu ipo Tanzania?huko Western mnaotahabika ni nyie foreigners tena wa third world countries,maana nyie ndio mnaochukuliwa wa mwisho kabisa baada ya eastern europe na asia,ila mbona unang'ang'ania huko kua kitchen porter kama ni sawa na Tanzania na kwa nini usirudi kwenu?unapokwenda job centre wewe ni mtu wa mwisho kupewa kipaumbele!hizo ni nchi zilizoendelea sana kiviwanda,tanzania ni nchi iliyoua sana viwanda!hao unaowaita wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini kwetu umefanya utafiti wa kutosha ukaona kweli ni wawekezaji ambao watanzania wananufaika na uwekezaji wao au ni wachukuaji wa rasilimali zetu tu kutokana na udhaifu wa uongozi wetu?nakushauri urudi ukafanye tafati ya kutosha kabla ya kukurupuka
 
quote_icon.png
By Rejao
Nyerere alitoa hicho kisingizio kutokana na udini. Kwa wakati ule alitaka Mkatoliki mwenzake aongoze nchi, ikabidi atumie udikteta kumweka Mkapa.

Kikwete katufanyia mengi mazuri sana. Mkuu wetu halali, anaihangaikia nchi, anasafiri huku na kule kututafutia sisi wananchi maisha bora. Baba mwenye nyumba siku zote ni mwangaikaji, hawezi kukaa tu nyumbani! Lazima akatafute!!

Rejao sikutegemea hii kutoka kwako.............basi mama.........hata hivyo Mkapa sio Mkatoriki bana. yule KKKT....
 
Tuje kwa wananchi hivi wale wanaume huwa wanapenda kukaa kwenye vijiwe vya kahawa na kupanga vikosi vya Madrid, man u, arsenal na stars siwatofautishi na huyo walio mchagua

Inaniuma sana sana eneo ili ulikuwa ugonjwa wa wale watu wenye uwezo mdogo/kawaida wa utambuzi kwenye maswala muhimu kama watu wa maeneo ya gerezani, kariakoo.Lakini leo inasikitisha sana sana kwamba hata wale wenye uwezo mkubwa wa ufahamu kwa maana wenye elimu ya juu yani watu wa level ya corporate,nao wameingia kwenye ***** huu wa man u,arsenal, madrid na mengineyo.Ningekuwa na uzwezo sio siri ningefunga channell zote za kipuuzi zinazopumbaza na kuwatia wazimu watanzania.

Wanasaikolojia wanasema watizamao mpira wa miguu wote ni wendawazimu,kwa kuwa haiwezekani binadamu wakakaa kuwatizama watu ishirini na mbili wanafukuza kingozi kilichojazwa upepo,uku watu wapatao maelfu nao wakisherekea kwa kukenua meno 32 nje kwa uppuzi huo lazima kuna tatizo na ndio maana kuna watu wanaitwa hooligans.[If you describe people, especially young people, as hooligans, you are critical of them because they behave in a noisy and violent way in a public place.]

Na kwa tulipofika anyathing too much is harmfull,hakika kama hakuna wa kuliona hili la watanzania kuwa limbukeni wa mpira wa mguu hakika Taifa huko mbele ya safari sana linazalisha na kuzalisha Taifa la Wajinga na malimbukeni baada ya kujali kujadili mambo muhimu kwa ustawi wa maisha yao wao kutwa nzima mitaani,majumbani,maofisini,vyuoni,viwandani na sasa inaelekea mashambani.

Wanajf fanyeni utafiti mdogo wa kawiada,wakati wa asubuhi wakati unasubili daladala asubuhi angalia pembeni yako ni watanzania wanangapi wanaangalia na kununua magazeti ya ufahamu na habari muhimu.Wengi ununua magazeti ya udaku na michezo kwa wingi sana,kati ya watu kumi ni wanaonunua magazeti ni watu wawili tu wanaonunua magazeti ya taarifa muhimu.Hakika njoo mida ya mchana mpaka jioni uko maaofisni na mitaani mambo muhimu hayajadiliwi kwa kuwa kati ya watu kumi walionunua magazeti ni watu wawili wenye Taarifa mahususi kuhusu maisha yao,wengine wote yani watu nane [8] wako kwenye ufahamu wa mambo ya mapenzi,udaku na michezo.Yani kati ya watu kumi vichwa vya watu nane kwa siku nzima zinaufahamu wa mambo yasiyo na tija bali yamejaa burudani hawana tofauti na watumiaji wa opium drugs.

Leo hii Taifa limekwama aliendi sio kwa sababu ya Kikwete ni kwa sababu ya mfumo,watu hawana uthibiti wa kuongozwa kwa kuwa waongozaji hawatuonyeshi tunakwenda wapi na tunatoka wapi na tunataka nini na kwa faida ya nani.Mbaya sana walioathirika ni wote kwa kuwa upande wa wanaume wako kwenye soka na taarifa zake wakati upande wa wanawake wako kwenye taarifa za mapenzi na udaku.

Waongozaji wetu ambao ni system wanapaswa kutuludisha kwenye ufahamu,hakika yanawezekana,sio kuwa kwa uwepo wa taarifa za soka na udaku ni haki ya mtu kuchagua laini ni haki ya mzazi kumchagulia mtoto asikilize nini,asome nini na kwa wakati gani.Kama hatuoni ni tatizo tuangalie ulaya wao wamekwisha athilika kwa mambo waliyoyakumbatia toka miaka ya sabini,kwanini sie tusijifunze kwa kuona na kusoma historia ya athali zake kuliko kuiga kila kitu.

Natumaini ujio wa digital utatutatulia tatizo hili kisai kuwa haya mambao ya kugeuza watanzania maskini kuwa waingereza na waspain kufikia kulogana na kutoana uhai kisa huyu ni mpenzi wa man united na huyu asernal hakika yataisha na uwenda Watanzania watarudi kutoka uingereza na kuijenga Nchi yao kwa kuwa watakuwa na nafasi ya kusoma na kusikiliza taarifa muhimu zinazohusu maisha yao na hatima ya Taifa lao.

Mbaya kichwa cha familia ambae ni mwanaume kamezwa na kaaamua kuamia mji wa manchestra na viunga vyake na kuacha familia mama na watoto wakiangaika kufuatilia habari za daimondo sound kaachana na umemaa aliegeuzwa na wasomaji wake ulemaa.Hakika tunaweza kubadilika ni system kuamua kukaa chini na kuona nini kinalikwaza Taifa pamoja na kuwa ufisadi ni moja ya vitu vinavyolikwaza Taifa,lakini pia mamilioni ya Watanzania ni mafisadi wa Taifa kupitia visingizio vya kupumzisha akili ya udhohofu wa umaskini kwa kuangalia soka na kusoma habari ya udaku.Kumbe ni kuua akili ambayo ilipaswa kusoma na kuangalia vitu vyenye kuongeza ufahamu wa raia wake huyu apate mbinu na maarifa ya kujikwamua toka kwenye umaskini na hatimae kulikwamua Taifa na yeye kujikwamua.
 
Waliomchagua Kikwete kweli wametukomesha watanzania,na wapongeza kwa huo ujinga walioufanya ju yetu watanzania.Mungu awasamehe.
 
Nyerere alitoa hicho kisingizio kutokana na udini. Kwa wakati ule alitaka Mkatoliki mwenzake aongoze nchi, ikabidi atumie udikteta kumweka Mkapa.

Kikwete katufanyia mengi mazuri sana. Mkuu wetu halali, anaihangaikia nchi, anasafiri huku na kule kututafutia sisi wananchi maisha bora. Baba mwenye nyumba siku zote ni mwangaikaji, hawezi kukaa tu nyumbani! Lazima akatafute!!

Baba mwenye nyumba wako?
 
quote_icon.png

Rejao sikutegemea hii kutoka kwako.............basi mama.........hata hivyo Mkapa sio Mkatoriki bana. yule KKKT....

Mkapa ni mkatoliki mkuu,ila mkewe ndio mlutheri!ila nachukia sana watu wanaoingiza udini katika kuchangia hoja kama mkuu rejao,tubishane kwa hoja na si kwa vigezo vya udini,rangi au kabila!tusiwe kama watu tuliofilisika kichwani,hayo mambo hayana faida kwetu
 
kama hukai nyumbani kwako ww mwenyewe unategemea nyumbani kwako kuwe na maendeleo kweli?mkuu wa nchi hakai nchini kila siku nje ya nchi tuu ,kama hii safari ya kichama itasaidia nini ktk nchi yetu?hiyo hela ya kwenda nje ya nchi angeipeleka ktk shule zetu za kata zingenunua madawati mengi tuu,lakini kiongozi wetu tuliye mchagua hakufanya hilo.
 
Kwani hao wanawake hawakuwa watanzania?

ni wadanganyika walioongozwa na hisia za mahaba juu ya mume wa mtu. Wakadhani kwa kumpigia kura wataonja fungu la mahaba kwa kupitia BB (Ballot Box), wasijue wanapanda upepo na sasa wanavuna katrina.
 
Mkubwa, unajua watanzania tunachanganya siasa na hali halisi ya maisha.Heri umemwambia ukweli.

Kwani siasa ni nini Mkuu?
Mbona tunakuwa makasuku kwa kuimba kila tunachowekewa na wababaishaji na wachambuzi feki!
Katika muhtadha wa MAENDELEO YA TAIFA na WATU,
kila kitu ni siasa ndugu yangu, namaanisha "kila kitu".
 
mleta nadhani hujui kabisa kwa nini kikwete anasafiri, upunguani wako wa muono na uhaba wako wa kusafiri unakufanya uone kuwa safari ni matanuzi.

Hivi, wewe unajuwa isingekuwa hizi safari leo ungekuwa katika dhiki mara 10 zaidi?

Hivi haya ma gesi yanayovumbuliwaa kila kukicha, haya matalii yanayozidi kila kukicha, haya mahoteli mpaka imefikia kuwa tanzania ndio imetowa hoteli bora duniani, unafikiri inakuja tu yenyewe? Hata bajeti yetu, ingawa kikwete kapunguzi sana utegemezi wa bajeti kutoka nje, lakini still tunahitaji kujazilia, mpaka hapo mambo yatapokuwa mazuri.

Tafadhali kama hauna cha kusema bora ukae kimya.

Kila siku huwa nasema humu, hebu tuchambuwe mambo muhimu tuone ni rais yupi aliefanya zaidi ya kikwete? Nakuhakikishia huna hata moja.

Si bora kikwete anakwenda kikazi, mkapa alienda kupunguza unene switzerland akaiacha ofisi zaidi mwezi. Kuna hata mmoja alinyanyua sauti aksema kwii.

Nyinyi mnajulikana chuki zenu kwa kikwete ni kwa nini. Lakini kwa utendaji bora na uchapa kazi, nawapa challenge, hakuna aliyemfikia hata robo. Tusiandikie mate na woino upo.

Barabara? Km ngapi kwa awamu zote? Km ngapi kwa kikwete? Amma zimeshajengwa au mikataba imesha sainiwa.

Mtarusha hili kama kawaida yenu.

are you serious or are you some sort of a comedian??
 
Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili,Hapo ndipo akili za wabongo zipime na kugundua kuwa walifanya makosa kumchagua kikwete na CCM yake iunde serikali ya nchi hii.Maisha ni magumu kila kona wa2 wanalalamika,hili liwe fundisho kwe2 2sifanye makosa tena 2015 kwani kosa sio kosa bali kurudia kosa ni kosa.

Mungu akuangazie nuru yake na akusamehe kwani hujui ulitendalo...
 
Wakuu,
Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 nilipata kuisikia kauli maarufu ya Dr. Slaa kuhusu madhara ambayo nchi hii ingepata endapo kikwete angechaguliwa mara nyingine tena. Dr. Slaa alisema kwamba kumchagua kikwete na ccm yake ni kukaribisha janga la kitaifa na wananchi watakuja kujutia uamuzi wao.

Leo hii, ikiwa ni mwaka mmoja na miezi kadhaa, wananchi katika kila kona ya nchi wanalalamika ugumu wa maisha. Maisha yamekuwa magumu na kadri siku zinavyokwenda ndivyo bei za bidhaa zinavyozidi kupaa. Wakati hali ikiwa hivyo kwa wananchi, kikwete anaendelea na utekelezaji na nadhiri aliyojiwekea ya kuvunja na kuweka rekodi ya kuwa rais wa kwanza Duniani kutembelea nchi nyingi kama si zote ndani ya kipindi cha miaka kumi tu ya uongozi. Juzi tu baada ya kutoka Switzland alikotoa kauli ya kusisitiza umuhimu wa misaada, alirudi nchini na baadaye kidogo aliekea Uingereza. Hivi ninavyopost thread hii, yupo Botswana eti kwenye sherehe ya chama tawala. Akiwa kwenye safari hizo, tumeshuhudia wagonjwa wakifa kwa kukosa matibabu kutokana na mgomo wa madaktari, wananchi Songea wanauawa na polisi na karaha mbalimbali lakini yeye kwa raha zake anaendelea na safari na matanuzi yake.

Kwa mwenendo huu, sina budi kuamini kuwa kikwete ni janga la kitaifa.

Nakuunga mkono 100%
 
Back
Top Bottom