NdasheneMbandu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2012
- 940
- 308
Wakuu,
Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 nilipata kuisikia kauli maarufu ya Dr. Slaa kuhusu madhara ambayo nchi hii ingepata endapo kikwete angechaguliwa mara nyingine tena. Dr. Slaa alisema kwamba kumchagua kikwete na CCM yake ni kukaribisha janga la kitaifa na wananchi watakuja kujutia uamuzi wao.
Leo hii, ikiwa ni mwaka mmoja na miezi kadhaa, wananchi katika kila kona ya nchi wanalalamika ugumu wa maisha. Maisha yamekuwa magumu na kadri siku zinavyokwenda ndivyo bei za bidhaa zinavyozidi kupaa.
Wakati hali ikiwa hivyo kwa wananchi, kikwete anaendelea na utekelezaji na nadhiri aliyojiwekea ya kuvunja na kuweka rekodi ya kuwa rais wa kwanza Duniani kutembelea nchi nyingi kama si zote ndani ya kipindi cha miaka kumi tu ya uongozi.
Juzi tu baada ya kutoka Switzerland alikotoa kauli ya kusisitiza umuhimu wa misaada, alirudi nchini na baadaye kidogo aliekea Uingereza. Hivi ninavyopost thread hii, yupo Botswana eti kwenye sherehe ya chama tawala. Akiwa kwenye safari hizo, tumeshuhudia wagonjwa wakifa kwa kukosa matibabu kutokana na mgomo wa madaktari, wananchi Songea wanauawa na polisi na karaha mbalimbali lakini yeye kwa raha zake anaendelea na safari na matanuzi yake.
Kwa mwenendo huu, sina budi kuamini kuwa Kikwete ni janga la kitaifa.