Hakika Gaddafi amenitoa machozi, upendo wake uliokithiri uzalendo ndio huo uliofupisha maishA yake

hyassin92

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
583
631
HAKIKA GADDAFI AMENITOA MACHOZI, UPENDO WAKE ULIOKITHIRI UZALENDO NDIO HUO ULIOFUPISHA MAISHA YAKE.

Leo nimeikumbuka hotuba iliyonisononesha sana mwaka 2011. Hotuba ya aliyekua kiongozi wa Libya Kanali Mu'uammar Qaddafi. Aliiandika siku chache kabla ya kifo chake.

Kwa kutambua kuwa humu wapo wanaojua Kingereza na wengine hawajui, nimeitafsiri kwa Kiswahili.

--QADAFFI ANAANZA HIVI:

"Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema....

Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.

Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.

Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.

Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.

Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.

Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).

Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.

Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.

Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.

Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.

Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"

Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.

Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.

Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.

Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!

Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.

Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule Sirte.

Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.

Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu.

Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru."

-- Mu'uammar Qaddafi.
 
Dikteta muuaji tu yule..ndio kasababisha Libya ikawa kwenye machafuko kwa kung'ang'ania madaraka

Wakati wa Arab Spring mbona Rais wa Misri, Hosni Mubarak aling'atuka na nchi ikasonga tu mbele japo naye alikuwa ameifanyia makubwa? Mbona wa Tunisia nae aling'atuka? Mbona wa Algeria naye juzi kang'atuka? Na nchi zao zinaendelea vizuri? hawa wote wangekataa kuondoka na kutumia jeshi kama Ghadafi alivyofanya nchi zao nazo zingechafuka na kubaki kama Libya au Syria, ila walijiona wao sio wakubwa zaidi ya nchi zao wakaondoka na sasa mambo yanaenda kama kawaida

Angeng'atuka mapema Libya ingekuwa vizuri na yeye angbaki hai kama kina Mubarak, Boteflika na yule wa Tunisia, ila kiburi ndio kilimponza..shenzy type
 
Tumekusikia
Dikteta muuaji tu yule..ndio kasababisha Libya ikawa kwenye machafuko kwa kung'ang'ania madaraka

Wakati wa Arab Spring mbona Rais wa Misri, Hosni Mubarak aling'atuka na nchi ikasonga tu mbele japo naye alikuwa ameifanyia makubwa? Mbona wa Tunisia nae aling'atuka? Mbona wa Algeria naye juzi kang'atuka? Na nchi zao zinaendelea vizuri?

Angeng'atuka mapema Libya ingekuwa vizuri na yeye angrbaki hai kama kina Mubarak, Bkteflika na yule wa Tunisia, ila kiburi ndip kilimponza..shenzy type
 
ametolewa mpaka kufa kabisa,haya niambie kwanini bado mambo hayajatulia?
 
Wengi wanadhani Gadafi aliondolewa na wapinzani wa serikali yake. Muamar Gadafi aliuliwa na mabeberu yaani mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Ufaransa

Libya kua hivi ilivyo sasa sio bahati mbaya, ni mpango ulipangwa na hao mabeberu kwa kushirikiana na vibaraka wao waliopo ndani ya Libyia ili nchi isiwe na serikali stable na wizi wa mafuta uwezekane kwa urahisi

Baada ya uvamizi na kuuliwa Rais Gadafi serikali ya vibaraka ya Libya ikaletewa invoice ya mabilion ya dollar eti gharama za mabeberu kuendesha vita ya kumng'oa Gadafi!

Nchi hiyo ambayo chini ya Muamar Gadafi ilikua haidaiwi na taasisi za fedha za mabeberu sasa hivi inalipa madeni ya kulazimishwa kupitia mafuta yake yanayochotwa kwa fujo na uroho mkubwa huko Benghazi! Mikataba yenyewe ni ya muda mrefu hadi miaka 50 mafuta yao yanachotwa kwa gharama ndogo sana!!!

Wala tusiwalaumu wananchi wa Libya maana hawakua na lakufanya. Hata AU walipotaka kuingilia kati na kusuluhisha mgogoro wa ndani wakaambiwa na NATO msithubutu kukanyaga Libya, ondokeni!!!

Mapigano tunayoyaona sasa na vitisho vya kuchinja watu ni mkakati wa haohao mabeberu Libya isitulie na Walibya wasiulize mustakabali wa nchi yao
 
Dikteta muuaji tu yule..ndio kasababisha Libya ikawa kwenye machafuko kwa kung'ang'ania madaraka

Wakati wa Arab Spring mbona Rais wa Misri, Hosni Mubarak aling'atuka na nchi ikasonga tu mbele japo naye alikuwa ameifanyia makubwa? Mbona wa Tunisia nae aling'atuka? Mbona wa Algeria naye juzi kang'atuka? Na nchi zao zinaendelea vizuri?

Angeng'atuka mapema Libya ingekuwa vizuri na yeye angrbaki hai kama kina Mubarak, Bkteflika na yule wa Tunisia, ila kiburi ndip kilimponza..shenzy type
Hata kusoma maneno yake hujayasoma...Huoni huzuni juu ya alichoandika? Huna utu? Huna moyo??

Aisee.
 
Yaani Libya ilikuwa ni raha mustarehe sasa hivi wengi ukiwauliza wanajuta walichokifanya baada ya kudanganywa kuwa wananyimwa demokrasia, wachota mafuta wamefurahi sanaa sasa hivi wanajichotea bila pingamizi... Sidhani kama Libya itakuwa sawa kama kawaida pindi cha Gaddafi
 
Libya haiwezi kua sawa tena kwasababu hiyo instability inaratibiwa na hao wachota mafuta kama walivyofanya kwa Iraq. Walivamia Iraq kwa sababu za uongo na bila kibali cha UN, wakauwa maelfu ya watu eti ili wawakomboe kutoka kwa Sadam Hussein! Unakomboaje watu kwa kuwaua!!!?

Sasa hivi meli za kusomba mafuta zinapishana tu huko Basra na Bandari nyingine kuiba mafuta ya Iraq
 
Dikteta muuaji tu yule..ndio kasababisha Libya ikawa kwenye machafuko kwa kung'ang'ania madaraka

Wakati wa Arab Spring mbona Rais wa Misri, Hosni Mubarak aling'atuka na nchi ikasonga tu mbele japo naye alikuwa ameifanyia makubwa? Mbona wa Tunisia nae aling'atuka? Mbona wa Algeria naye juzi kang'atuka? Na nchi zao zinaendelea vizuri?

Angeng'atuka mapema Libya ingekuwa vizuri na yeye angrbaki hai kama kina Mubarak, Bkteflika na yule wa Tunisia, ila kiburi ndip kilimponza..shenzy type
Kwani c wameshamuua huyo dicteta mbona hawapat hYo mafanikio acha chuki za kidini
 
Libya haiwezi kua sawa tena kwasababu hiyo instability inaratibiwa na hao wachota mafuta kama walivyofanya kwa Iraq. Walivamia Iraq kwa sababu za uongo na bila kibali cha UN, wakauwa maelfu ya watu eti ili wawakomboe kutoka kwa Sadam Hussein! Unakomboaje watu kwa kuwaua!!!?

Sasa hivi meli za kusomba mafuta zinapishana tu huko Basra na Bandari nyingine kuiba mafuta ya Iraq
Sawa sawa, na ndicho kinachoendelea Syria
 
Sawa sawa, na ndicho kinachoendelea Syria
Kabisa mkuu, huu uharabia na ubeberu unaoratibiwa kwa makini na NATO. Wale ni majambazi wauwaji wasio na chembe ya utu.

Libya haiwezi kua sawa tena, Irak hivyohivyo na sasa Syria inavurugwa pia. Iran nayo inaundiwa zengwe taratibu nayo pia itavamiwa na mafuta yake yataporwa kwa nguvu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom