Haki za wanawake alaumiwe nani?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,428
13,936
Kazi za mwanamke na mwanaume zinatokana na miundombinu ya kiumbaji waliyokuwa nayo. Miundombinu hii iko kwa jinsia zote bila kujali aina ya kiumbe. Mfano, wanyama wote wanaonyonyesha akiwemo binadamu wanawake huwa wanashinda na kukesha wakihudumia watoto wao, na wanaume wanafanya shughuli za kuzalisha tu na kujihudumia wenyewe kwa chakula. Majike ya ndege nayo yanakesha mchana kutwa yakihudumia watoto wao wakati madume yakifanyakazi za kuzalisha tu majike mengine mitaani na kujihudumia wao wenyewe kwa chakula na kila kitu. Hivyohivyo kwa wadudu pia. Hii inaonyesha kuwa mungu ana mpango unaofanana kwa viumbe wake wote kuhusu majukumu ya kila jinsia kutokana na miundo mbinu aliyowawekea. Hii ina maana kuwa mwanaume kudai kupikiwa na kufuliwa nguo na mwanamke sio sawa hata kidogo. Lakini mwanamke nae kudai kutunzwa na mwanaume sio sawa kabisa. Lakini mwanamke kunyimwa haki ya kufanyakazi sio sawa kabisa. Lakini mwanaume kunyimwa kuwa na wanawake wengi sio sawa kabisa kwakuwa anayo miundombinu (nguvu na mbegu nyingi sana) ya kuzalisha wanawake wengi kwa wakati mmoja. Na mwanamke kunyimwa kutembea na mwanaume mwingine sio sawa kabisa kwa sababu wako wanaume ambao ni wagonjwa, wenye kasoro za kurithi na wasio na uwezo wa kutia mbimba hivyo kung'ang'ania awe ndio mume wako tu sio sawa kabisa. Hivyo basi haki za mwanamke na mwanamume hazitoki kwa binadamu bali zinatoka kwa MwenyeziMungu mwenyewe kwa kuwekewa miundombinu ya kuzitekeleza. mfano, ubongo, mwili na viungo vya mwanamke vinahimili kubeba mimba, kuzaa bila kusaidiwa, na kulea watoto bila kusaidiwa kitu ambacho mwanaume hawezi hata kidogo. Lakini miundombinu ya mwanaume inamuwezesha mwanaume kumudu kufanyakazi zile ngumu sana, za kikatili na kuishi na wanawake wengi bilq shida.
Kama hatujui Mungu anataka nini kwa wanawake na wanaume tujikumbushe kwa kuviangalia viumbe vingine vinavyofanya na vinavyoishi, maana sisi wote ni wa mungu na tumeumbwa na Mungu. Kama alitufanya viumbe vyote viwe na mifumo yenye mahitaji sawa kama vile uzazi, chakula, hewa, sauti, nerves, damu, ubongo, nk. kwanini tuwe na mashaka juu ya kazi zetu?

Binadamu anajidanganya kwa kudhani kuwa yeye ana akili kuliko viumbe wengine kumbe ndiye mjinga kuliko viumbe wengine duniani. Ushahidi wa ujinga wake ni kuyaharibu mazingira mulemule anamoishi, ushoga, kujenga magorofa yanayowaporomokea, kutengeneza ndege zinazo waangusha, kutengeneza mabomu yanayowaua wenyewe, n.k
Shida ya mwanamke ilianzia tangu pale alipokubali mahari iwe kipengele muhimu katika mahusiano yake na mwanaume. Hapo ndio balaa lake lilipoanzia. Futeni mahari ili mfanane na viumbe wengine
 
Back
Top Bottom