Haki za kidigitali ni haki za Kibinadamu

Jun 30, 2015
18
15
1.Haki za kidigitali ni haki za kibinadamu.

1.1. Haki ya mtandao
Kila mtanzania ana haki ya mtandao kupata mtandao kwa gharama nafuu.

Kuongezeka kwa gharama za data na ukosefu mzuri wa mtandao umekuwa changamoto katika nyanja mbalimbali. Kwani haki ya kimtandao wananchi wanashindwa kuitumia ipasavyo katika shughuli mbali mbali.

Wananchi hutumia mtandao katika shughuli za Elimu, biashara na burudani na habari. Kuongezeka kwa gharama za kununua bando au data na kukosekana kwa mtandao umeleta madhara katika sehemu zifuatazo.

A. Kiuchumi
Gharama ya data kuwa kubwa imesababisha wafanyabiashara wanapata changamoto sana katika kutangaza biashara zao mtandaoni.

Mfano Tsh 500 inakupa 150mb kwa saa 24. Je inatosha kutangaza biashara katika mitandao ya kijamii kama Facebook,Instagram nakupatana, zoom Tanzania, n.k

Hayo ni baadhi ya maeneo ambayo mfanyabiashara anaweza weka tangazo na akapata wateja wengi sana.
Inasemekana mteja kununua bidhaa anahitaji kuona tangazo lako mara saba ili aweze kukuamini, kukupenda, kukujua na kununua (KLTB PRINCIPLE).

Je, kwa bando hilo inawezekana?

Mtandao kuwa mgumu kupatikana maeneo ya vijijini.

Pia imechangia sana kwa jamii zilizopo kijijini kushindwa kutumia vizuri haki yao ya kimtandao kwa sababu ya mtandao kupatikana kwa shida na gharama kuwa kubwa wao kumudu.

Mfano.Kuna mkulima mmoja yupo kijiji cha mbali sana na Ana mazao ambayo anatamani kuyaleta mjini kwenye masoko makubwa lakini inamuwia vigumu kuweza kuwasiliana na wachuuzi waliopo mjini kutokana na ukosefu na mtandao.

Mkulima huyu kama angekuwa na uwezo wakupata mtandao kwa gharama nafuu kabisa ,angeweza kutuma video au picha ya mazao au bidhaa aliyonayo nakutuma kwenye mitandao ya kijamii ambayo ni rahisi kuwafikia wateja wengi waliopo sehemu mbalimbali ambao wanauhitaji na bidhaa /mazao yake na ikawa rahisi kwake kufanya hiyo biashara kwa bei nzuri itakayo mletea faida ya ukulima wake.

Na karne ya hii ya 21 tuliyopo (21st century)mitandao ya kijamii imekuwa na nafasi kubwa sana kibiashara.
Gharama yabkununua bando inapokuwa kubwa kuna jamii ambayo haitaweza kwendana na mabadiliko hayo kwahiyo biashara zinarudi nyuma na pia haki ya mtandao wanashindwa kuitumia ipasavyo.

Gharama data inapokuwa kubwa, Mfanyabiashara anaona hana sababu yakutafuta wateja wengine kwakutumia mitandao ya kijamii ambapo ni hasara kwake kwani husindwa kutimiza malengo ya kibiashara yake kwa wakati. Dunia imekuwa ya kidigitali imekuwa kama kijiji, njia za kufanya biashara zina hama kutoka njia ya zamani na kuhamia kidigitali (traditional marketing to digital marketing ).

B. Elimu
Tumekuwa mashuhuda namna mtu anaweza kujifunza au kusoma kwa njia ya mtandao.

Tumeona makala mbalimbali za kufundishia na kuelekeza vitu tofauti tofauti zinnawekwa mtandaoni ,chochote unachotaka kukijua au kujifunza ukiingia mtandaoni basi ukitafuta unakipata.

Gharama ya data inapokuwa kubwa basi kuna jamii itashindwa kutumia au kufurahia haki yao ya kimtandao katika elimu.

C. Burudani
Wapo watu wengi hutumia haki yao ya kimtandao katika kupata burudani. Gharama ya data kuwa kubwa jamii hii inashindwa kufurahia haki yao ya kimtandao.

D. Habari
Hapa tunazungumzia kizazi kinaitwa Millenials.

Hii ni aina ya watu ambao chanzo Chao cha habari ni mitandao ya kijamii.

Watu hawa hutegemea asilimia kubwa mitandao ya kijamii kupata habari mbalimbali, kwahiyo gharama inapokuwa kubwa basi jamii hii hushindwa kupata taarifa kama ilivyokawaida yao, na haki yao yakimtandao hawaifurahii vizuri.

UCSAF (Mfuko wa mawasiliano kwa wote)

Upatikanaji wa mtandao unahitajikanlwa kiwango kikubwa sana maeneo yote. UCSAF tunaomba iweze kuhakikisha mikongo ya mitandao inafika hadi vijijini ili waweza kufurahi nakutumia haki yao yakimtandao kwa manufaa mazuri katika maendeleo yao na yanchi pia.

MNOs (mitandao ya simu)

Kuangali kwa mara nyingine suala la data kuongezeka kwasababu kwakufanya hivyo hii itawaongezea wateja wengi watakao hitaji kutumia huduma zao.

Kila mtu anahaki sawa na anaruhusiwa kufurahia haki yake ya kimtandao kwa njia iliyosahihi.

#MitandaoNidata
#digitalRightTZ

IMG-20220916-WA0182.jpg
IMG-20220916-WA0183.jpg
IMG-20220916-WA0194.jpg
 
Back
Top Bottom