Wanabodi,
Tanzania ni nchi inayozingatia haki za binadamu pamoja na utawala wa kisheria. Kuna hili suala la panuzi za barabara zetu sehemu mbalimbali nchini.
Cha kusikitisha na kushangaza ni kwamba kuna raia waliokwenda mahakamani kupata zuio japo la muda ili nyumba zao zisibomolewe, na mahakama kuridhia maombi yao, lakini cha ajabu nyumba zao zinabomolewa.
Hapa kuna hoja ya msingi Sana, kwanza mtu amejenga kwenye hifadhi ya barabara, huyu kaifuata barabara hivyo hanabudi kuvunjiwa bila kulipwa fidia, hii haina tatizo.
Kuna ambao barabara imewafuatta, naamini wale walio kwenye zile mita 121.5, hawa wanastahili kulipwa fidia na kupewa maeneo mengine ya kuendeleza shughuli zao.
Jamani msifanye mchezo na kubomolewa mjengo wako, wewe umejikimu miaka kumi kujenga mwnzio anabomoa kwa dakika mbili tu tena bila kukufidia, hii itakuwa ni zaidi ya laana kwa huu utawala.
Inakuwaje serikali haina hata utu tu wa kuwapatia maeneo mengine na uwezo inao? Na hili la kudharau mahakama halijakaa sawa hata kidogo, ifike mahali huu mhimili wa mahakama ujitafakari Kama sheria inazotafsiri zinadharauliwa na serikali kuna haja gani uwepo?
Wananchi pia sioni sababu yoyote ya kwenda mahakamani kuishtaki serikali wakati tunaona wazi kuwa haiheshimu hukumu zinazotolewa na mahakama huko ni kupoteza muda, ibaki mhimili huu wa mahakama uwe ni idara ndani ya serikali, sijui huko tuendako Kama tutafika salama maana huyu dereva wa hili Lori hazingatii sheria, kwenye zebra cross yeye anaongeza speed, kewye 50 km/ hr yeye yupo 120 speed, yangu macho tusubiri.
Sent using Jamii Forums mobile app