haki pekee itazuia ulipaji kisasi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

haki pekee itazuia ulipaji kisasi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JAYJAY, Oct 28, 2011.

 1. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,486
  Likes Received: 822
  Trophy Points: 280
  tumeshuhudia yaliyotokea Libya baada ya kuuawa kwa mtawala Gaddafi. wapo wanaopinga kuuawa kwake na wapo wanaounga mkono pia, kila mtu ana sababu yake. kwa mtu aliyetawala kwa mkon wa chuma miaka 42 ni wazi kuwa alitumia nguvu kubwa pia kuzima chokochoko zozote za kuhoji uhalali wa yeye kutawala ikiwa hata kwa kumwaga damu ya baadhi ya watu. licha ya mazuri ambaye wengine wanayaona wapo ambao walipoteza ndugu zao (mfano wazazi na jamaa) na ambao hawakupata hata kujua hatima yao kwa kutopewa hata maiti zao wazizike. kwa watu wa aina hiyo huwezi kuwashawishi kwa chochote kuondoa chuki yao hasa ukizingatia hawa ni Waarabu wanaoamini kuwa kisasi ni haki. hivyo nafasi yoyote mtu wa aina hiyo akiipata ya kuwa karibu na yule mhusika zawadi atakayompatia ni kummaliza kwa risasi, hata mimi ningefanya hivyo tu, na ndivyo ilivyokuwa. huu ni ujumbe kwa viongozi wetu, wananchi wanataabika huku wao wakiendelea kuiba mafedha bila kuchukuliwa hatu mfano rada, epa na uozo mwingine. hiii ni kupandikiza chuki ambayo itazua visasi baadae vya kupelekea watu kutolewa uhai bila kupenda. waliangalie hilo! maana hata mimi sitawaonea huruma watu wa aina hiyo wao na familia zao kwa watakayoyapata.
   
Loading...