bahati93
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 1,385
- 2,587
Asalamu watu wa jamii na jambo langu nataka niwe wasemeshe.
Ni kuhusu HAKI.
Haki ni kitendawili
Kadiri upeo wa mwanadamu inavyoongezeka na ndivyo hivyo inakuwa ngumu kutegua fumbo hili HAKI ni nini, nani asimamie HAKI.
Haki imekuwa ikifikiriwa na kutafsiriwa na jamii mbalimbali tangia zama za kale mpaka leo hii.
Jamii za kale nyingi zilisema na kuamini kutenda haki ni kuwa imara na kujali jamii yako tu wengine wote ni maadui hawafai hata kupata haki, waweza kuwaua, kupora mali zao, kuwafanya watumwa ni sawa tu kwenye mizani ya haki. Katika zama hizi jamii au mtu mwenye mamlaka ndiyo aliyekuwa akitoa maana ya haki na kusimamia utekelezaji wake. Ukisoma maandiko ya kale utakutana na viongozi mbalimbali walioheshimika kwa kuwa na utawala wa sheria: solomoni, nk pia utakuta story za wafalme wenye manyanyaso kupitiliza.
Jamii na serikali za wakati huu zinaamini haki zipo sawa kwa wote hamna aliyekuwa na haki zaidi ya mwanadamu mwenzake, mwanadamu yoyote aliyebahatika kwenda shule atakubaliana na maono haya. Na ili kufanyiza haki itendeke mihimili mitatu ya utawala ikasimikwa: bunge, mahakama na serikali katika zama hizi vuta nkuvute inaendelea kati ya wenye mamlaka na mihimili katika kutoa tasfiri ya HAKI. Endapo mtawala atazidi nguv mihimili bas atatenda yale anayoona ni haki ndani ya macho yake pasipo kuzuiliwa.
HAKI bado inasafari ndefu sana kuweza kufafanuliwa kwani katika ulimwengu huu inaonekana ni kitu kisichowezekana ambacho tunakiita haki ni mfano tuu wa haki. Kwani bado kuna watu wanaamini kwamba wanachoona kwao ni sawa ndo iwe haki na si vinginevyo.