Haki na Amani

Haki na Amani

Tman900

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
969
Reaction score
3,065
Haki na Amani.

Wanasiasa wa Africa, au Tanzania malazote Kwenye majukwaa utakuta wanazungumzia tudumishe Amani.

Swali Huwa najiuliza, Mbona awazungumzii swala la Haki na Usawa, Maana Palipo Na Haki Amani utamalaki pia Haki ni ngao kubwa ya Amani, Kwa Nini Amani Imekua kama kichaka cha kujifichia, pia Kuna Umuhimu wa kutungwa Sheria ambazo zitakua na Haki sawa kwa wote. Maana Tanzania ni ya kwetu wote.
Tanzania sio ya Kikundi cha watu Fulani, au Tanzania ni ya Chama Fulani.

Why kusiwe na Umoja wa Kitaifa unaosimamia Haki sawa kwa wote pasiwepo upendeleo.

Pia Kuna Kila Haja ya kulitazama Jeshi la Polisi, Pia kuna kila sababu ya kulifumua na kuliunda upya Jeshi la Polisi maana Kuna Mengi yaliofichika ndani ya Jeshi, Kwa Nini Comment nyingi za wananchi zinaonyesha kutokua na Imani na Jeshi la Polisi na Utendaji kazi wake.

Kuna swali la kujiuliza Jeshi la Polisi kujichunguza lenyewe kua Lina makosa sio kweli ingetakiwa kuwa na Chombo ambacho kingekua na mamlaka ya kulichunguza Jeshi la Polisi maana wananchi walio Wengi Hawana imani na Jeshi la Polisi.
 
Back
Top Bottom