Haki na Amani ni kitu kimoja

Mwana kondoo 2025

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2025
Posts
495
Reaction score
580
kwa sasa hoja kubwa nchini ni HAKI kwanza kabla ya Amani, mimi ninakubaliana na hilo popote pale kama hakuna haki automatic Amani haipo. Wana falsafa wote enzi za kale walihubiri Haki kisha Amani. Koran na Biblia mitume wote wilihubiria Amani . Sisi waislam dhana muhimu kabisa ni HAKI na vivyo hivyo kwenye ukristo. Sasa vita na machafuko chimbuko lake kubwa ni maonezi na ugandamizaji wa haki. jambo hili tuliangalie sana kwa vile wananchi wameanza kuelewa haki zao za kiraia. serikali iwe makini mno hususani kwenye masuala ya uchaguzi ili tusitumbukize nchi kwenye machafuko.
 
Mzani uheshimiwe...upo mahakamani, upo TRA, wamisri waliamini unyoya ukiwa mwepesi kuliko moyo wako Mungu Anubis anakugrant eternal life.

Tuheshimu mzani (haki)... Amani ni matokeo ya haki kutamalaki.
 
Gentleman haki huambatana na wajibu,
kinyume na hapo ni fujo, vurugu, uharibifu na usumbufu.

mimi na wewe tuna haki ya kutoa haja kubwa kila moja kwa wakati wake muafaka. Inakua ni usumbufu ikiwa ukijiskia tu kutoa haja kubwa basi popote pale utakajiskia basi uitekeleze, na kwamba ukiwa kanisani unasali na wenzako ukijiskia kushusha mzigo ushuhe tu, right? si haki yako?

ukijiskia kufanya hivyo hotelini mkiwa mnakula supu ya samaki unashusha mzigo juu ya meza kabisaa, right? si haki yako na ya haki kila mtu kushusha mzigo?

ukijiskia hivyo darasani wakat Mwalimu anafundisha wewe unatumia haki yako ya kibinadamu kushusha mzigo n.k n.k

Kistaarabu,
ukijiskia kutumia haki yako hiyo ni lazima uwajibike kutafuta mahali sahihi kwa kujisitiri na si vinginevyo.

Zingatia ukweli huo gentleman, ni muhimu sana 🐒
 
Mzani uheshimiwe...upo mahakamani, upo TRA, wamisri waliamini unyoya ukiwa mwepesi kuliko moyo wako Mungu Anubis anakugrant eternal life.

Tuheshimu mzani (haki)... Amani ni matokeo ya haki kutamalaki.
SAHIHI

Usafi wa Moyo -- Ufaulu wa Konsayansi : Maadili na Uadilifu kwa 'Shauri UTU'

ANUBIS na Mizani...

Mizani na 'Ma'at'...

Hizo alama picha zote haziko kwenye hizo taasisi kwa 'Bahati Mbaya'... Zina asili ya 'Hekima' ya Zama hata Zama....

Hata Katiba iliyopo kuwa na 'tamko' la Mraba wa uadilifu kwa 'Uhuru-Udugu-Haki-Amani' kwenye 'Usovereini wa Nchi-Dola' siyo 'Bahati Mbaya'... Ni asili kuu ya Miundo, Vitendo yenye kuakisiana na 'Mifumo'--kwa kuwa asili ya mfumo wowote ni 'Shauri'... Shauri kwa Unyoofu na Mapenzi mema.

- Mraba katika upumzi wa 'Ontolojia ya Taasisi' ni asili ya 'Unyoofu' wa Utu na Matendo : Miundo na Utendaji...

- Uduara wa Ushawishi kwa kadiri ya 'Ontolojia ya Taasisi' ni asili ya 'Mapenzi Mema' katika 'Mapana ya Ustawi wa Jamii' na 'Nyakati zake'...

- Uweza-Utayari-Umahiri wa wanajamii ndiyo 'Ngao ya Ustawi' -- Vesika-Paisisi ya 'Mazazi ya Utu Bora'...

Ni suala la Wanajami kuwa macho tu... Kila kitu kimeshategeshwa kwa ajili ya 'Kumbukumbu' zao na 'Mafahamu'...


'Haki' ni mama wa Utamaduni / Ustawi wenye Afya--Rushwa ni adui wa Haki.


Itatokea sana wakati huu--watu wengi wataamka na kujifahamu kuhusu 'Haki', si Tanzania tu--hili ni Duniani kote; ndani ya hii miaka 25, kufika 2050, litaleta mabadiliko makubwa kwa 'Sura za Nchi na Tawala'...


Unaloliona sasa, namna fulani kama wanajamii wanaanza kuhoji uhusiano wa 'Haki' na 'Amani' kwa namna fulani kama vile hawababaishwi na 'siasa' ama 'utamaduni wa uoga', ni mwanzo wa 'Roho ya Uhuru' inayoingia Wanajamii wote wenye Usentienti-Konsayansi-Nuru ya Ufahamu.

Bado lipo hitaji la uwajibikaji zaidi wa kiraia, kwa kuwa tatizo 'si serikali khasa'--tatizo ni 'watu'... Uweza-Utayari-Umahiri, kuyamudu mageuzi makubwa ya kiutamaduni na maendeleo...

Siasa haina 'Maajabu', daima si suluhu ya kudumu ya matatizo ya kijamii yenye kuhusiana na 'Ujinga'; mchezo wa kujifurahishia 'makuzi'...

Maajabu yapo kwenye 'Kujitambua' na kupeana mwangaza...

Hmmm
 
Amani ni sawa na kunyamaza ama kukaa kimya naweza kukaa kimya kwasababu ya kupenda kufanya hivyo lakini pia naweza kukaa kimya kwa kunyamazishwa kumbe kukaa kimya siyo maana halisi ya amani


Silence surrenders public responsibilities
 
Usisahau WAJIBU
 
A very good analysis

Our biggest downfall has been kuweka diasa kwenyr kila kitu

Na hilo limetuletea extreme bias

Thr day we separate siasa nq social norms tutakua tumetoboa

Personally kusikiliza wanasiasa ni sawa na kushabikia simba au yanga…. We become emotional and blind to the core

Untangle diasa kwenyr haki, wajibu na ukweli…. Amani itakua ndefu zaidi
 
SURE!

Siasa ni kofia kwa wale wanaodhani hiyo huwatosha...

Uzalendo ni 'Dini'; hii daima hujumuisha Utu na Utamaduni ambavyo utamaduni ni mambo mengi katika 'Shauri'... Shauri ilivyo ni mbegu ya u-JUA-ji : Uono Mifumo...

Yakianza kuzungumzwa kiufundi mambo ya asili ya siasa za chama kimoja -- chama dola kimoja cha siasa katika 'Majenzi ya Taifa Changa' na rafu za 'Kudesa/Kushinikiziwa Demokrasia za Kimagharibi'--wengi humu wenye nasibu ya kujua ilivyobora wataanza kufahamu 'wamekuwa hawajui na hali wakidhani wanajua'...

Alhamdullilah, kama wanajamii wenye kulifanya Taifa, tunaingia kwenye 'daraja' : Treni Kilimanjaro...

Hmmm

====

View: https://www.youtube.com/watch?v=8Xg7abZRihs
 
Uchambuzi mujarabu wenye maonyo mtambukwa kwa maslahi mapana kwa jamii yoyote yenye kutaka kuchanua, kinyume chake ni mnyauko.

Kazi kwao wasiotaka kuruhusu mwangaza kupenyeza hadi kwenye vungu za malalo yao, pasi kujua muhanga nambari moja wa nyoka uvunguni yupo juu ya kitanda.
 
Uchambuzi mujarabu wenye maonyo mtambukwa kwa maslahi mapana kwa jamii yoyote yenye kutaka kuchanua, kinyume chake ni mnyauko
NI ELIMU 2.0...

Sisi sote tunayo mbegu yake kwa 'Akili' na 'Dhamiri'...

'Kuwa' ama 'Kuto-kuwa' katika 'Mwangaza wa Utu Bora' hilo ndilo Swali (!)

Yohana 15​

1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.

3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.

4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.

5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.

6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.

7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.

9 Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu.

10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

11 Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.

12 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.

Penye 'Nia pana Njia'...
'Mkasi wa Akili yenye Uaminifu : Shika Neno tenda Neno' na 'Msalaba wa Uzima'...

Uhuru-Udugu-Haki-Amani ni 'Ukadinali Mbegu' ya 'Dhama : Maarifa ya Kumcha Mungu'...

+++

Mithali 1​


1 Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.

2 Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu;

3 kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili.

4 Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari;

5 mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.

6 Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao.

7 Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.

8 Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,

9 Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako.

10 Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali.

11 Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu;

12 Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni.

13 Tutapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka.

14 Wewe utashirikiana nasi; Tutakuwa na vitu vyote shirika.

15 Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.

16 Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu.

17 Kwa kuwa mtego hutegwa bure, Mbele ya macho ya ndege ye yote.

18 Na hao hujiotea damu yao wenyewe, Hujinyemelea nafsi zao wenyewe.

19 Ndivyo zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali; Huuondoa uhai wao walio nayo.

20 Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu, Hutoa sauti yake katika viwanja;

21 Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, Mahali pa kuyaingilia malango, Ndani ya mji hutamka maneno yake.

22 Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?

23 Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu.

+++

View: https://www.youtube.com/watch?v=gN9RVnVC-iw
 
Mzani uheshimiwe...upo mahakamani, upo TRA, wamisri waliamini unyoya ukiwa mwepesi kuliko moyo wako Mungu Anubis anakugrant eternal life.

Tuheshimu mzani (haki)... Amani ni matokeo ya haki kutamalaki.
Kuna watu wanatutoa kwenye reli... Wanachomekea parameters 2 za Uzalendo na Utii wa mamlaka!
 
Kuna watu wanatutoa kwenye reli... Wanachomekea parameters 2 za Uzalendo na Utii wa mamlaka!
Uzalendo ni kupigania haki ya kila mmoja, utii ni kwa mamlaka iliyowekwa na umma pekee, sio iliyojiweka yenyewe. Kifupi ni kuwa either hawaoni ama wanajipofusha maksudi.
 
Nilikuwa najua kweli una matatizo gentleman lakini si kwa kiwango hiki. Hoja yako yote umeishia kwenye kushusha mzigo!!
 
Nilikuwa najua kweli una matatizo gentleman lakini si kwa kiwango hiki. Hoja yako yote umeishia kwenye kushusha mzigo!!
relax na kujali hoja bila makasiriko wala mihemko gentleman 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…