Haki elimu; wadau wa elimu mjini lindi wamenena!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haki elimu; wadau wa elimu mjini lindi wamenena!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, Apr 13, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Mimi si miongoni mwa watu ambao nimepata kutokukubaliana na tangazo lolote la HakiElimu! Hata hivyo, lazima nikiri wazi kwamba wadau wa Elimu Lindi wamenena, na sasa kazi kwenu HakiElimu kuifanyia kazi kauli yao! Kwa mujibu wa wadau wa Elimu Mjini Lindi, ni kwamba matangazo ya HakiElimu inaangalia upande mmoja na kusahau upande mwingine wa shilingi! Madai mara kwa mara yamekuwa yakitolewa na wadau wa kila aina kwa nyakati tofauti kulingana na dhima ya tangazo husika! Mathalani, serikali imeshawahi kuyalalamikia matangazo hayo pale yanapoonekana kuisakama zaidi serikali! Lakini wadau wa Elimu Mjini Lindi wanauliza kulikoni HakiElimu kusahau upande wa pili wa shilingi ambao ni WANAFUNZI WENYEWE?! Wadau hawa wanauliza, je ni kweli WANAFUNZI/VIJANA WETU wanafahamu wajibu wao wa kuwa wanafunzi? Je, HakiElimu wanafahamu kwamba kuna wanafunzi kibao wanatoka home wakielekea shule lakini wanaishia chimbo( hawaingii darasani)! Unaweza kumlamu, lakini what abt mzazi sawa na wazazi wetu wengi?! Kuna mtoto wa kaka yangu ambae ni miongoni mwa wanafunzi ambao bado hawajui wajibu wao!! Baada ya kumuona kazidisha usela, nikamlazimisha anioneshe matokeo yake shule. Ktk matokeo ya Form II, dogo kakung’uta C moja na zilizobaki ni D chache na F!!!!! Ni form II huyo!! Mimi sikai pamoja na familia hii, lakini nilipohulizia pale kwao nikakuta kumbe mama mtu anafuatilia sana maendeleo ya mwanae- na kwa kauli yake mwenyewe shemeji yangu akaniambia “mimi mara kwa mara huwa naenda shuleni kwao kuulizia maendeleo yake na wananiambia kwamba hakosi shule na maendeleo yake darasani ni mazuri!” Shemeji yangu anaamini kwamba maendeleo ya kijana wake ni mazuri-ni mbaya zaidi hata akiyaona hayo matokeao hawezi kuelewa what is all about C, D, or F! Hawa ndio wazazi wengi wa wanafunzi wetu wa mjini na vijijini!Wazazi wengi wa aina hii wanachojali ni mwanafunzi kwenda shuleni; hiyo ndio kusema mtoto anaendelea vizuri! Je, HakiElimu mnaliangalia vp suala hili?! Serikali ishakumbushwa sana, kama wana masikio wamesikia na kama hawana basi mtaendelea kupoteza resources bure ingawaje ni wajibu kukumbushana. Ni wakati umefika sasa kuwakumbusha na wanafunzi kufahamu wajibu wao wa kuwa shule. Kila penye haki, lazima pawe na wajibu. Mmejitahidi kutetea haki za wanafunzi, sasa wakumbusheni wajibu wao ili badala ya kuwaona ni WATETEZI WAO sasa wawaone ni WAPIGANAJI WA MAENDELEO YAO YA ELIMU. Hata kama tutakuwa na maabara kama za New York au Tokyo! Hata kama tukipata best teachers kuliko wengine wowote duniani! Hata kama kila mwanafunzi atapatiwa Helikopta ya kumpeleka shuleni! Hata kama kila mwalimu atajengewa kasri lake na kupewa Benzi la kumfikisha shuleni! Hata kama akina Issack Newton, Archimedes, Einstein wakifufuka na kuja kufundisha shule zetu; bado itakuwa ni sawa na hakuna endapo bado wanafunzi hawafahamu wajibu wao!
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  kwanza kabla sijaanza kudadavua hoja hapa, nielewe unavyosema wadau wamenena, unamaanisha wewe au? ni mawazo yako binafsi au ulichosema kinawakilisha mawazo ya wadau wengine wa Elimu mkoani Lindi?

  Bnafsi nafikiri, HakiElimu wanafanya vizuri tu! kumbuka kwamba wana mission na vision amabyo inawasukuma kufanya hayo wanayoyafanya. kwa sababu tu wewe hupendi wanachokifanya, haiwezi kuwafanya wabadilishe the way they do business. kama wewe ni mwanaharakati basi advocate for what you stand up for......tell them students to be serious, concentrate, make goals and see the value of education.

  I completely disagree with you on putting yourself aside and want HakiElimu to do what every mdau wa elimu should do.
   
 3. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Naamini unakifahamu vizuri Kiswahili hivyo ni bora usijibu kwa kuangalia personal interests. Nimeshakuambia WADAU WAMENENA, hiyo ni obvious wao!! Nilichofanya mimi ni kuendeleza tu, au kukidadavua zaidi kile walichodai kwamba HAKIELIMU wanaangalia upande mmoja na kusahau kuwakumbusha wanafunzi wajibu wao. Endapo usingejibu hoja kwa kuwa bias basi ungegundua mara moja kwamba nimeanza kwa kusema kwamba mimi si mmoja wa watu ambao nimeapata kutokukubaliana na tangazo lolote la HakiElimu- Hii maana yake ni nini Madam?! Kama usingekuwa bias ungejuwa kwamba mara zote nimekuwa nikikubaliana na matangazo ya HakiElimu. Hata hivyo, hilo haliwezi kunifanya kutoangalia upande wa pili wa shilingi. Hoja yangu ni kwamba, pamoja na mara kwa mara HakiElimu kutetea haki ya kupatikana kwa elimu bora, ni vizuri vilevile wakiwa wanawakumbusha na wanafunzi wajibu wao!! Bigirita, umeshawahi kuishi maeneo ya pwani na kuona wanafunzi wanapokacha shule na kwenda kuvua samaki huku wazazi wao wakiona ni sawa tu (kutokana na upeo wao?)?! Ni kwanini basi HakiElimu waijaribu kuwakumbusha na wanafunzi hawa wajibu wao? LOOK this, Haki ya mfanyakazi ni kupata mshahara lakini wajibu wake ni kufanya kazi kwa tija. Kiongozi yeyote wa wafanyakazi anayeona wajibu wa mwajiri tu wa kulipa mshahara na kusahau wajibu wa mfanyakazi wa kufanya kazi basi kiongozi huyo hafai!!!! Wewe kama mzazi ni wajibu wako kumuhudumia mtoto gharama za elimu, lakini nae ni wajibu wake kuzingatia kile kinachompeleka shule!! Bigirita, sijasema HakiElimu hawafanyi kazi vizuri, ninachosema wanapaswa pia kuwakumbusha wanafunzi wajibu wao ili kuwasaidia wazazi ambao wanachukuwa suala hili kirahisi. Mimi si mdau wa Elimu, nipo tu kitaa lakini hilo halitanifanya kukosoa pale ninapoona panafaa kufanya hivyo. Mkuu, kama wewe ni mtu fulani pale HakiElimu, please angalieni uwezekano wa kutoa matangazo ya kuwakumbusha wanafunzi wajibu wao-Hapo tutafika otherwise, ni kama nilivyosema kwamba hata kama kila mwanafunzi atapewa helikopta, itakuwa ni kazi bure endapo hawatafahamu wajibu wao. Kama wewe ni mwana HakiElimu, basi RELAX KIDOGO kisha anza kuisoma upya thread yangu huku ukila BIG G!!
   
 4. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani mkuu hujaekewa hoja yake suala ni kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu nchi, ili kuboresha sekta ni vyema maeneo yote yenye upungufu yakawa addressed bila kuegemea upande mmoja kama wafanyavyo Haki Elimu.
   
 5. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  That is what i really mean MKUU!!!
   
Loading...