Mwanaume mwenzenu huyo.............
Usijekuta hata rafiki/ndugu ya mtu hapa wa karibu..................
Mi hapa ndo huwa siwaelewagi viumbe wanaoitwa wanaume duniani.
Yaani ukiwahamisha wanaume wanawake wenzio watakushuhulikia. Kuna wanawake ambao hawawezi kupita siku mbili bila hiyo huduma!
LD si Wanaume wote wana mawazo ya kipumbavu kama ya huyu mshenzi/hayawani ambaye badala ya kutafuta wanawake watu wazima ili aweze kukidhi matamanio yake ya kimwili anakavizia kabinti kadogo ili akaharibu. Si ajabu huyu mshenzi ameshafanyia uhuni wake kwa vibinti vingi hapo mtaani. Ni vizuri huyu adhibitiwe kwa namna moja au nyingine ili kuepusha vibinti vingine visiharibiwe na huyu kichaa.
Pole kwa kupata baridi. Jenga sana urafiki na binti yako. Mimi naamini wazazi wakiwa marafiki wa watoto wao, watoto wanakuwa hawana siri, akiwa na tatizo anajua mtu wake wa kwanza kumweleza tatizo lake ni Mama/ Baba yake. We fikiria kama Kijana juzi angekuwa hana urafiki / ukaribu na binti yake angemwelezaje hicho alichofanyiwa na huyo babu mtu mzima hovyo? Wazazi wasiwatenge watoto wao. Waonyesheni mnawajali na kuwathamini. Mtoto inabidi siku zote ajue kuwa rafiki yake wa kwanza huku Duniani ni Baba / Mama yake. Hatatokea wa kumdhuru / kumdanganya kwa chochote. Mungu awatangulie watoto wote humu duniani. Amina.Hii thread imenipa baridi kabisa yaani, nimechoka hata sielewi, masikini binti yangu. Hebu nijifunze kuanza kuzungumza nae mwe! nitaanzaje sasa kuzungumza nae kuhusu haya mambo ya mapenzi wajameni kwamba ............................ jamani mtihani hebu nipeni mwongozo maana wangu ana 10 sasa ila huwa naona kama bado mdogo sana.
Asante mleta mada, shukrani kwa wachangiaji kuhusu malezi ya watoto kwani nimejifunza mengi kwa hii thread. Ila hilo la kuanza kuzungumza na binti wajameni mtihani, Nisaidieni ndio naanza anza anzaje?
Hii thread imenipa baridi kabisa yaani, nimechoka hata sielewi, masikini binti yangu. Hebu nijifunze kuanza kuzungumza nae mwe! nitaanzaje sasa kuzungumza nae kuhusu haya mambo ya mapenzi wajameni kwamba ............................ jamani mtihani hebu nipeni mwongozo maana wangu ana 10 sasa ila huwa naona kama bado mdogo sana.
Asante mleta mada, shukrani kwa wachangiaji kuhusu malezi ya watoto kwani nimejifunza mengi kwa hii thread. Ila hilo la kuanza kuzungumza na binti wajameni mtihani, Nisaidieni ndio naanza anza anzaje?
Aisee!
Nimemkumbuka Matesha wangu....almost same age.
Haki Ya Mungu Ntaua mtu. Nimesemaje? and I mean it!
Kwanza nakupa pole kwa hilo na hongera kwa hatua ulizochua. Mara nyingi hasira huwa ni hasara, huenda ungempiga mtoto wako paleplale kwa hasira tu. Lakini pia naomba huyo fataki muwekee mtego halafu mfundushe mtoto wako ili asimuambie kwamba amewekewa mtego kisha ukimkamata mpige picha tena uwe na mashahidi watakaosaidia kumkamata na kutoa ushahidi halafu mpeleke kituo cha polisi na hatimaye mahakamani.Habari wana JF!!
Kama title inavyosema ni kabinti kangu yaani katoto kangu ka kike kenye umri wa miaka 9.5 sasa.
Majuzi nimekaa nako kwenye gari nikisubiri bidhaa nilizoagiza huku nataniana nae, kiukweli nampenda sana mwanangu ndiyo maana akawa rafiki yangu mkubwa!!!
Katika kucheza cheza pale akanitupia swali, namnukuu `Hivi baba kwanini yule baba dukani kwa kina Robu hupenda kuniita ita kule uani kwao halafu anapenda kunishika shika matakoni na kifuani?` Kwani ndo nini hivyo?
Kidogo nianguke kwa presure.....huyo baba mwenyewe ni mtu mzima sawa tu na mzazi wangu mimi!!! Na sikumjibu kitu ila nikamwambia nitakuelezea nyumbani tukifika, mama mtu akataka kumpiga but nikamwambia no!! Mwache
Nilijaribu kumdadisi kama kuna anachopewa na huyo mzee akajibu hajawahi kupewa kitu chochote zaidi ya pipi na gumz basi.
Natafuta namna ya kumjibu na kumwelekeza madhara yake na kuweka mtego wa kumnasa fataki!!
Mama hataki mtoto aelekezwe kwa sasa juu ya swala zima la mapenzi kisa bado mdogo sana!!! Wana JF mnadhani ni sahihi?
Nimeweka hapa pia kama tahadhari kwetu wana JF coz najua wengi wetu hapa ni wazazi na sikujua jambo kama hili lingeweza linitokee kwangu ila ndiyo hivyo limenifika!! So take care na watoto wetu jamani