Hajuna mjinga zaidi

Hajuna mjinga zaidi

Joined
Mar 4, 2015
Posts
13
Reaction score
12
SI MCHEZO duniani kuna watu. Juzi juzi nilihadithiwa mkasa nikagundua kuwa binadamu tunapishana barabarani lakini akili zetu tofauti. Jirani yangu juzi kanambia alikwenda kwao, si unajua ndugu zetu wengine wakiona dili zinakataa wanarudi kwao kusafisha nyota, sasa alipokuwa huko kusafisha nyota alikutana na mkasa ambao ni aibu kwa wote wanaotoka eneo lile. Sikutajii eneo hilo kutokana na aina yenyewe ya mkasa, nikitaja kuna watu wa huko watanishukia na mvua ya ngumi.
Basi jirani yangu mjanjanja flani wa mjini alipokuwa kwao akanambia siku moja alikuwa kakaa sehemu moja kilabuni akinywa pombe ya kwao. Pombe yenyewe ni ile ambayo kabla hujaanza kunywa unapewa kamba mbili za kufunga chini kwenye suruali karibu na visigino, maana ukishalewa lazima ujiharishie, wenyewe wanaaita pingu. Basi wakati anakunywa akawa anawasikiliza jirani zake wawili walikokuwa wamekaa jirani na wanakunywa hiyo pombe yenye masharti magumu, iliyokuwa kwenye bakuli kubwa. Akamsikia mmoja wa wale walevi akilalamika, “ Aise Tino, mimi mke wangu ananidharau sana”, mwenzie akamuuliza ,”Kivipi?” Yule mlevi wa kwanza alinyanyua lile bakuli la pombe akanywa kama funda tatu hivi kisha akashusha bakuli na kucheua ndipo akajibu, “Bwana mke wangu eti ananiambia hajawahi kuona mwanaume mjinga kama mimi, hili jambo limeniuma sana sijajua nimfanye nini. Kunitukana mwanaume mzima tusi kama lile unajua inauma sana”. Ilionekana kwa mbali machozi yana mlengalenga. Tino akampigapiga bega kirafiki mlevi mwenzie na kumwambia, “ Unajua Kidoa, huyu mkeo hajawahi kutembea, angetembea ndio angejua duniani kuna wajinga, hapahapa kijijini kuna wajinga mpaka utashangaa” Kidoa akabaki akimwangalia rafiki yake huku akisubiri maelezo zaidi. Basi Tino nae akanyanyua lile nakuli na kuvuta funda, kisha akakohoa kidogo na kusema,” Ngoja nimuite yule dreva wa boda boda ndio ujue duniani kuna wajinga”, basi akamuita yule dereva wa bodaboda, baada ya salamu akamwambia, ”Nataka nikutume”. Kijana wa Bodaboda akajibu yuko tayari. Basi Tino akamwambia yule dreva wa bodaboda,” Hebu nenda pale kwangu nenda kaangalie kama niko kwangu sawa? Haya chukua na hela yako kabisa”. Kijana akapiga honi kwa mbwembwe na kutimka kwa lesi kali akielekea nyumbani kwa Tino. Tino kamgeukiwa Kidoa, ”Unaona mambo hayo?” Kidoa akakubali, “ Kwa kweli nimeona na kweli nimeamini kuwa kuna wajinga wengi hata hapahapa kijijini kwetu” Basi marafiki hawa wawili waliendelea kunywa kwa furaha. Haukupita muda mrefu Bodaboda akarudi na kijana kutoa taarifa yake,’ Mzee nimefika kwako sikukukuta, hata mkeo nimemuuliza kasema haupo”. Tino akamshukuru yule kijana na kumruhusu aende, Bodaboda alipogeuka tu walevi hawa wawili wakaanguka kicheko. Kidoti ndie alionekana kufurahi zaidi maana hata machozi yakuwa yakimtoka kwa furaha. Kisha kidoti akamwambia mwenzie,”Yaani leo hii lazima nimwambie mke wangu, ili ajue kuna wajinga zaidi ya mimi. Leo ndio nimeona ujinga wa hali ya juu” Baada ya kunywa kimya kwa muda kila mtu akionekana na mawazo yake ghafla Kidoti akarudia tena kwenye ule mkasa, “Unajua yule mtoto mjinga sana. Ningekuwa mimi kwanza ningepokea ile hela, halafu nisingekwenda mpaka kwako, ila ningempigia simu mkeo na kumuuliza kama upo, halafu ningerudi kukupa jibu” Tino alimuangalia rafiki yake kwa mshangao kisha akasema, “ Sasa nimeelewa kwanini mkeo anasema hakuna mwanaume mjinga kama wewe”
 
Nafikiri kwenye heading ulitaka kuandika HAKUNA na si HAJUNA

Halafu habari ndefu kama hii ilifaa iwe na paragraphs
 
Back
Top Bottom